Kungekuwa na sumu ya kujidunga kisha unakufa usingizini wengi tungeshatoweka duniani

Kungekuwa na sumu ya kujidunga kisha unakufa usingizini wengi tungeshatoweka duniani

Sensei Tai

Senior Member
Joined
May 26, 2022
Posts
168
Reaction score
466
Hali ya maisha ni ngumu sana

Kuna wakati unatamani hata kungekua na simu ambayo unajidunga wakati unaingia kulala kisha inakuondoa baada ya masaa matatu baada ya kupitiwa na usingizi

Tatizo tunawaza wanaotutegemea tutawaacha kwenye hali gani

Unakuta familia inakutegemea lakini wewe unaetegemewa ukiangalia mbele unaona kiza tu mana kila siku afadhali ya jana

Wale mliojaliwa vipato vya kumudu maisha yenu mshukuruni sana mwenyezi Mungu

Kuna wakati unawaza kwanini hata ulizaliwa kutokana na mateso unayopitia ya maisha

Wakati mwingine unajiuliza kwanini na mimi sikuzaliwa familia ya kitajiri lakini unapata jibu kwamba yote ni mipango ya Mungu.

Anyway acha niishie hapa.
 
Pole sana mkuu, kama wewe ni mwanaume, pambana na uache kutamani kuwa mfu.

Tafuta pesa kwa nguvu zako zote, familia ya kitajiri itoke kwako. Kama hao waliozaliwa kwenye familia za kitajiri baba zao wangekata tamaa na wangewaza kujiua kama wewe huo utajiri ungekuwepo?

Pambana, na acha kuwaangalia wengine. Acha kujilinganisha na watu wengine. Tupo katika Dunia moja lakini tunafanya mitihani tofauti kabisa.
 
Hali ya maisha ni ngumu sana

Kuna wakati unatamani hata kungekua na simu ambayo unajidunga wakati unaingia kulala kisha inakuondoa baada ya masaa matatu baada ya kupitiwa na usingizi...
Usiishi kwa kuamini vitu ni vikubwa kuliko wewe jifunze kushukuru kwa hatua ya kuwa hai kwanza .

Kuwa mtu wa Kujitazama ndani Sana usisubiri watu wayape Maisha yako maana ila wewe ndo mtu pekee wakuyapa Maisha yako maana .


Vita ya akili, Mwili na hisia ukitaka kuishinda hakikisha unaishi zaidi katika wakati uliopo Usiwaze kuhusu Kesho na usiwaze kwa yaliyopita.

Be authentic

MAISHA ni zawadi na ili ufurahie hii zawadi hakikisha unakuwa postive na mambo yataanza kubadilika .
 
Yaani kama sio mila na dini zetu hakika vijana wengi wangejimaliza kwa ground mambo magumu sana ..
Vijana wanapitia changamoto sana, zaidi ni hawa waliosoma na hawana ajira.

Lakini shida zaidi kwa vijana ni kujilinganisha na watu wengine na kutamani maisha ya watu wengine waliofanikiwa. Ukiishi maisha yako bila kujilinganisha na wengine utaishi kwa amani sana.
 
Sasa mkubwa kama familia inakutegemea wewe alafu unatamani tena kuwe na sumu unywe ufe dah!

Si sawa mkuu. Wafikirie familia utaiacha katika hali gani.

Pambana uwezavyo, kufa kwa kujiua ni fedheha
 
Vijana wanapitia changamoto sana, zaidi ni hawa waliosoma na hawana ajira...
Ushuhuda kuna marafiki zangu kadhaa walishafanya attempts za kujiua kwa nyakati tofauti ,wote ni ishu za maisha magumu kuna jamaa alipigwa na maisha mpaka demu wake akaenda kuolewa na jamaa mwingine alifanya kunusurika watu walivunja mlango huko uswazi la sivyo angejimaliza...

Wapo watu wapo makazini na wana stress kutokana na utegemezi mkubwa .
 
Mkuu pole lakin nikushauri tu kitu ndugu, hayo mawazo hayasaidii kubadil mambo kuwa bora.

Haya ni aina ya mawazo ambayo yatakuongezea maumivu, jitahidbsana usiyawaze haya zaid ni bora ukajifunza zaid namna ya kumudu kujituliza nafsi nafsi yako unapopitia nyakat ngumu hizi.

moja ya kitu kinachonisaidoa sana binafsi katika time kama hiz, huwa nina weza ku shut off kabisaa mindset yangu nisiwaze kitu chochote..Yan nakua kama sina nachpotia kwa kutoruhusu kabisaa kini disturb.
Hasa pale napokua nimeshafanya kila namna but nothing happens, bas kama ndege vile, huwa najiweka auto-pilot. I dnt think too much..

Kitu kingine simetimes jitahid usijionee huruma sana. Haya mawazo unayowaza ni dalili utafika pabaya zaid sio muda mrefu usipoangalia. Achana nayo.

MWaka huu ni moja kati ya vipindi sitakaa nivisahau maishani.

But here we go. Usione watu wanatabasam na kucheka huko barabarani ukajilinganisha nao, ni vile kila mtu ana apply ubunifu wake wa kutomezwa na mawazo ya kushindwa, everyone ia fighting their battle na whatever faces you, just trust God , u have the ability to overcome it..JUST A MATTER OF TIME
 
Back
Top Bottom