DOKEZO Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM

DOKEZO Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Jitihada za pamoja zinamaliza kunguni wote.... Nia ajabu wewe kuja kulalamika humu....

1.Siamini kama Kuta za udom zinaweza kutunza kunguni unless mseme chuo kina Hali mbaya Kwa sasa.
2. Kama namba Moja Iko sawa basi mnateswa na mnapolala Yani vitanda na magodoro.
3. Kama ni namba mbili basi jitihada za pamoja zinamaliza tatizo kabisa tieni hasara chuo kwenye umeme.

Mwaka 2017 au 18 makuyuni boys ARUSHA ilibadilishwa na kuwa kambi ya JKT so baadhi tulitolewa kambi fulanifulani kwenda kuandaa mazingira pale... Ebwanaaaa kulikua na KUNGUNI kuliko mchanga nje ya mabweni (mahanga) walipuliza dawa zaidi ya mara 3 hapakua na mabadiliko yoyote...

UNTIL TULIPOAMUA KUPAMBANA WENYEWE
1. Kuta zilipigwa plaster rough baadhi hazikupigwa kabisa hivyo kuwa maficho ya kunguni

2. Bomba za vitanda zilijaa kunguni Yani ukigonga chini unajaza sahani

3. Magodoro yalikua yamechakaa na hivyo kuwa maficho ya kunguni.

KAMPENI IKAANZA.

1. Tulisafisha Kuta zote Kwa sabuni kama tunafua nguo Kwa wiki mbili mfukukizo tukafumua dari (boards) zote tukachoma

2. Yaliandaliwa mapipa ya maji moto na muda wote yalikua namaji.

3. Kila asubuhi Kila mtu atatoa godoro na kulianika kwenye Jua Kali na utaligeuza mara kadhaa Kwa siku

4. Usimuache kunguni popote na hakikisha huna mazalia kwenye kitanda chako (mayai) Kwa hapo chuo hii ni rahisi sana mkiamua.

5. Kila juma mosi na jumapili Kwa wakati wako ilibidi kuchoma moto vitanda na kuvimwagia maji ya moto. Vitanda vya mbao vyote tulivifanya Kuni, kumaliza kunguni kwenye mbao ni KAZI sana

Tulifanikiwa kuwamaliza Kwa zaidi ya 99.5% Kwa muda WA miezi miwili tu.

Jitihada za pamoja ni suluhisho na sio kulalamika Jf. Na kama unajiandaa kuja KUPAMBANA mtaani hiyo ni CHANGAMOTO ndogo kuliko tulizonazo huku kitaaa.
 
Nenda duka la vifaa vya kilimo Kuna dawa ipo kwenye kichupa kidogo sana ni kwa ajili ya hao bugs bei 3,500, nunua hand pump zinauzwa 8,000, mafuta ya taa nusu Lita, changanya na maji Lita moja piga kila kona na hakikisha sehemu zote na vitu vilivyomo kwenye room hasa kwenye kona za vitanda na Meza unapiga. Mchanganyiko huo mnapiga hata room 6 na hilo tatizo mnalimaliza.

Alafu hebu acha uvivu mambo madogo kama hayo yakuja kulamika na lenyewe serikali iingilie kati uchafu wenu kweli?
Na hizo boxer mfue sasa na maji ya moto
 
Acha kudeka,

Chukua heater, chemsha maji mengi ya moto, osha hivyo vitanda kwa maji moto kila kona,

Chukua godoro lako, kung'uta vizuri kabisa, toa folonya ulifue, fua mashuka yako then pasi kwa moto mkali,
You are good to go,

Short cut, nunua dawa za kuua wadudu, pulizieni humo ndani, hazizidi buku 5, kwa watu wanne ni 1250 each,

Tuache kulalamikia vitu vidogo tunavyoweza solve wenyewe, sisi sio toddlers bana
Yaani room wako wanne tu na wana majagi ya kuchemshia maji, ni suala la kuamua tu kuamka jmosi wamwagie maji zile chaga, kona zote za kitanda then wakazianike juu kule ghorofani. Case solved.

Nashangaa kijana anaeyetegemewa kutunukiwa shahada anasubiri serikali itenge pesa kwa ajili ya kunguni ambao wanakufa kwa maji ya moto.

Old moshi pale tulisumbuliwa sana na kunguni wayback nasoma advance, ila ilitengwa siku mara 2 kwa mwaka ya kuchemsha maji moto na kuua kunguni. Hiyo siku ilipewa jina la msanii mmoja wa wasafi.
Tulikuwa tunaishi poa tu karibia term nzima.
 
Sina haja ya kutaja jina langu wala kuandika maelezo mengi, lakini kwa ufupi mimi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwakweli suala la kunguni UDOM limekuwa linasumbuwa na lina kera kwa muda mrefu.

Ajabu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sasa wadudu hao wamekuwa wengi sana yaani nahisi hata Ufaransa tunaposikia wamefunga vyuo hawajafikia huku, ni kero sana.

Kunguni hao wanapatikana kwenye mabweni tunapolala, mfano kwenye college ya Education ndio balaa.

Siku za nyuma uongozi wa chuo ulikuwa na kawaida ya kupuliza dawa kwenye mabweni, lakini ndani ya miaka hii miwili hali imekuwa tofauti.

Tulipofunga Chuo Juni na Julai 2023 tulitegemea tukirudi tutakuta wamepuliza dawa lakini hali imekuwa tofauti, matokeo yake watu tumeanza kulazimika kutandika na kulala chini kwani vitandani hakulaliki.

Changamoto hii sio kwenye college yetu pekee bali karibia zote Wanafunzi tumekuwa tukilalamika kunguni.
Poleni sana, kunguni ni mdudu anayetokana na hulka za uchafu.
1. Safisha chumba vizuri.

2. Zoa uchafu na hakikisha umechoma moto ili mayai na kunguni walio katika huo uchafu wafe.

3. Hakikisha godoro lako halijatoboka au kuchanika, kama ndivyo lishone au badili cover ila hakikisha cover imeshonwa kote ili godoro liwe ndani.
4. Nunua mafuta ya taa na brush ya 1", anza kupaka katika maungio yote ya kitanda, chaga na ktk mapindo ya godoro. Kunguni na mayai vyote vitakufa, rudia zoezi baada ya wiki 2.
5. Nguo zote zilowekwe katika maji yenye povu jingi la sabuni at least for 30 mins, zisuuzwe na kuanikwa.
6. Safisha chumba baada ya masa 3 ya kufanya hiyo kazi na fungua madirisha ili kuruhusu hewa safi kuingia.
7. Kama kuna vitanda vya chuma na vina matundu katika frames, ziba kwa sabuni, plaster au celo tape.
8. Kwa matokeo mazuri zaidi, wote katika chumba fanyeni kwa pamoja zoezi hili.
9. Usafi uwe zoezi endelevu.
 
Nenda duka la vifaa vya kilimo Kuna dawa ipo kwenye kichupa kidogo sana ni kwa ajili ya hao bugs bei 3,500, nunua hand pump zinauzwa 8,000, mafuta ya taa nusu Lita, changanya na maji Lita moja piga kila kona na hakikisha sehemu zote na vitu vilivyomo kwenye room hasa kwenye kona za vitanda na Meza unapiga. Mchanganyiko huo mnapiga hata room 6 na hilo tatizo mnalimaliza.

Alafu hebu acha uvivu mambo madogo kama hayo yakuja kulamika na lenyewe serikali iingilie kati uchafu wenu kweli?
Na hizo boxer mfue sasa na maji ya moto
uki-fumigate chumba kimoja haisaidii
watakaoingia hiyo room toka kwengine watawaleta wapya, na mduara utaanza upya
 
Mkuu, hao kunguni ni mtu unatembea nao, hawahami toka room moja kwenda nyingine,

NB. Nimesoma UDOM, nimekaa hapo COED anaposema mtoa mada, nishawahi kutana na adha ya kunguni room kwetu, (room za majirani hawakuwa nazo)
Tukapiga usafi wa maana wa vitanda, mara moja tu na mwaka mzima tukaishi vema bila kuandika uzi jf au X,
Sijui kizaz cha sasa kimetoka ufaransa 😂😂😂😂 kinataka Kunguni tu serikali iingilie kati 😂😂😂😂 sijui exile mtapigaje madogo na kunguni hao 😂😂😂😂
Education again, mbona education wapo hivi lakini?? College za humanities na informatics sina uhakika kama wapo.
 
uki-fumigate chumba kimoja haisaidii
watakaoingia hiyo room toka kwengine watawaleta wapya, na mduara utaanza upya
Kunguni ni mdudu hatari sana, ana uwezo wa kutembea hadi kilometer mbili usiku kufuata damu. Akishapata damu anataga awe jike au dume wote wanataga Akishapata damu, ni vigumu mno kuwaangamiza, tafuteni watu wa pest control watawaelekeza namna ya kuwaangamiza
 
Kuna shehe ubwawa alisema kunguni ni pigo la allah[emoji28].
Acha ujinga.....nilitamani hata nifahamu kiwango chako cha elimu maana reasoning yako ipo chini sana, bad enough unaweza kuwa ni mume/mke wa mtu
 
Sina haja ya kutaja jina langu wala kuandika maelezo mengi, lakini kwa ufupi mimi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Kwakweli suala la kunguni UDOM limekuwa linasumbuwa na lina kera kwa muda mrefu.

Ajabu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sasa wadudu hao wamekuwa wengi sana yaani nahisi hata Ufaransa tunaposikia wamefunga vyuo hawajafikia huku, ni kero sana.

Kunguni hao wanapatikana kwenye mabweni tunapolala, mfano kwenye college ya Education ndio balaa.

Siku za nyuma uongozi wa chuo ulikuwa na kawaida ya kupuliza dawa kwenye mabweni, lakini ndani ya miaka hii miwili hali imekuwa tofauti.

Tulipofunga Chuo Juni na Julai 2023 tulitegemea tukirudi tutakuta wamepuliza dawa lakini hali imekuwa tofauti, matokeo yake watu tumeanza kulazimika kutandika na kulala chini kwani vitandani hakulaliki.

Changamoto hii sio kwenye college yetu pekee bali karibia zote Wanafunzi tumekuwa tukilalamika kunguni.
Poleni sana, kuna dawa nyepesi sana ya kinyumbani. Maji ya moto.
 
Nunua Dawa Inaitwa Lava Nyunyiza Ndani Siku Mbili Utawamaliza Wote Chap Chap
Leo Tunazima Mwenge Manyara
 
Kunguni ni mdudu hatari sana, ana uwezo wa kutembea hadi kilometer mbili usiku kufuata damu. Akishapata damu anataga awe jike au dume wote wanataga Akishapata damu, ni vigumu mno kuwaangamiza, tafuteni watu wa pest control watawaelekeza namna ya kuwaangamiza
Naomba niwajulishe kuwa fumigation inatumika kwenye maghala ya chakula. Kudili na wadudu ni pest control na siyo ku fumigate.
 
Acha kudeka,

Chukua heater, chemsha maji mengi ya moto, osha hivyo vitanda kwa maji moto kila kona,

Chukua godoro lako, kung'uta vizuri kabisa, toa folonya ulifue, fua mashuka yako then pasi kwa moto mkali,
You are good to go,

Short cut, nunua dawa za kuua wadudu, pulizieni humo ndani, hazizidi buku 5, kwa watu wanne ni 1250 each,

Tuache kulalamikia vitu vidogo tunavyoweza solve wenyewe, sisi sio toddlers bana
Nakazia,nilichogundua watoto wa seminari or wale wanaodekezwa majumbani hawana ubunifu kabisa they wait someone to do on their behalf.no creativity.
Mleta mada kuna wanaosoma education with chemistry wailize dawa za kunguni otherwise waambie wakatengeneze maabara kule ilichuo kisiingie gharama
 
Bila fumigation hawaishi., hao wanao shauri mchemshe maji ni ushauri mbovu, mkitibu room moja bado haisaidii, maana wanatembeleana mabwenini lazima wasambae tu.

Sasa mlivyo wabeba kuwasambaza nyumbani kwenu likizo loh. Polen sana.
 
Acha ujinga.....nilitamani hata nifahamu kiwango chako cha elimu maana reasoning yako ipo chini sana, bad enough unaweza kuwa ni mume/mke wa mtu

Tatizo umeanza kutumia smartphone jana,nenda accont ya hilda mtandao wa x,utakutana na hiyo post ya shehe ubwabwa akisema mlipuko wa kunguni ufaransa ni pigo la ala kwa wafaransa[emoji28],dini ni upuuzi kama upuuzi mwingine,hope pigo la ala limehamia udom. [emoji706]
 
Acha kudeka,

Chukua heater, chemsha maji mengi ya moto, osha hivyo vitanda kwa maji moto kila kona,

Chukua godoro lako, kung'uta vizuri kabisa, toa folonya ulifue, fua mashuka yako then pasi kwa moto mkali,
You are good to go,

Short cut, nunua dawa za kuua wadudu, pulizieni humo ndani, hazizidi buku 5, kwa watu wanne ni 1250 each,

Tuache kulalamikia vitu vidogo tunavyoweza solve wenyewe, sisi sio toddlers bana
Dawa yoyote watakayonunua wachanganye na mafuta ya taa. Watakufa mpaka mbegu zao
 
Hivi mlipokuwa likizo walikuwa wanaishije hao kunguni? Isije kuwa mmetoka nao huko vijijini kwenu. Kwani kunguni anaishi muda gani bila kunywa damu?

Edit: eti jamaa wanaweza ishi hadi siku 400 bila kunyonya damu!!! Natengua kauli.
Wana ishi miezi mpaka sita bila kula chochote
 
Hiyo ni dalili ya kwamba mnashindwa kutatua changamoto zenu , punguza kudeka hapo inaonyesha wazi hamjitambui swala la kunguni ni uchafu sas mnashindwa vipi kufanya usafi wa kina hata kuchangishana kias Cha pesa zipigwe dawa ? Ok sawa basi tumien maji moto kusafisha Kila kitu hrf zianikwe Juan,,achen kulalamika watoto wa kishua ,nyie ndio hata makwenu mlikuwa hamfungi mabomba mkikuta maji Yana mwagika kwakuwa baba/ mama atalipia bili! Badilikeni ifike muda mnayosoma mjue kuyatumia kwenye maisha ya kawaida ili muwe mnajisimamia! ( acha kumaindi babu nakuchana makavu ) Sijapinga hoja
 
Back
Top Bottom