DOKEZO Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM

DOKEZO Kunguni wanatutesa Wanafunzi tunaolala kwenye mabweni ya UDOM

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kijana kunguni tu unakuja kulalamika JF [emoji1745]sisi ndio waanzilishi(intake ya kwanza ya Masters)hapo UDOM,tulikuwa tunakaa Ng'ong'ona kule Block S 2008/2009 na tunasomea Social,kipindi barabara ya kutoka kule ni vumbi na makorongo kama yote,Daladala ikienda Mjini inabidi muisuburi mpaka irudi tena au mtembee kwa miguu mpaka Social kuhudhuria PINDI,sasa kijana mayaimayai unalalamika Kunguni JF duuh,si ni suala la kuchangishana tu wana-chumba na kununua dawa!!vijana wa siku hizi lainilaini sana
Like niliokupatia ni kwasababu ya historia hio lakini sio hitimisho ulilofanya kuhusu vijana.
 
Tatizo la wachangiaji huwa wanatoa majibu ya kejeli au kubeza mara uchafu

🔷 Kunguni ni janga la wadudu ambao huibuka kwa kipindi Fulani kutokana na mabadiliko mbalimbali ya tabia nchi kama ilivyo wadudu wengine kama senene, NDEGE waharibifu kama kwelea kwelea nk

🔷 Kuna baadhi ya watu hawajawahi kukutana na majanga haya kutokana na eneo wanapotoka labda hawajawahi kuvamiwa na tatizo hili na mengine.

🔷 Ni kwamba mdudu huyu akishavamia sehemu hajali Cha usafi uchafu na dawa mpaka uipatie Sana. Tena kwa Taarifa nanastawi zaidi kwa mtu msafi ndio anajitokeza hadharani kwa mbwembwe

🔷 Huko ufaransa Sasa hivi wapo maabara kumchunguza zaidi mdudu huyu chanzo chake ni kitu gani kimesababisha kuibuka mpaka kuwashinda nguvu na wanajitahidi Sana kuepuka maneno ya kibaguzi na ya kipuuzi kuwa wageni ndio wameleta wadudu hao kama hapa watu wanavyosema uchafu unachangia. Kwa bongo Kuna baadhi ya eneo ambalo halijawahi kabisa kukumbwa na mdudu huyu na yawezekana baadhi hawajamwona hata kwa macho zaidi ya kuiona picha yake na kusoma tabia yake ndio wanatoa maneno ya jumla kuwa ni uchafu.

🔷Kuna baadhi ya viumbe hutumiwa kwenye ulimwengu wa roho. Kwamba Kuna watu wanaweza kuvitumia baadhi ya viumbe kwenda kuleta majanga kwa binaadamu kama nyuki, fisi, kunguru, bundi ,funza nk. Na viumbe hao wanaweza kuwa wenye roho tuu kama majini yanavyosumbua baadhi ya sule kwa wanafunzi kuchanganyikiwa au viumbe wenye mwili. Yote hayo yanaweza kufanyika, hivyo sio Kila janga hutokea kiasili mengine hutengenezwa ndio maana unaweza kukuta nyumba Fulani inavamiwa na janga Fulani pamoja na jitihada za usafi , dawa nk lakini wapi.

🔷 Kunguni ni sawa na janga la panya likija huwezi kulishugulikia peke yako, linahitaji jitihada ya jamii nzima ikiwemo serikali kwenye tafsiri za dawa kwani unaweza kusema unawaua kwa mafuta ya taa , maji ya moto, maji ya chumvi au maji ya sabuni ya unga kumbe imeibuka specie mpya hambayo haisikii chochote kuhusu hayo mazoea ya kupambana nayo. NO RESEARCH NO RIGHT OF SPEECH
 
Acha kudeka,

Chukua heater, chemsha maji mengi ya moto, osha hivyo vitanda kwa maji moto kila kona,

Chukua godoro lako, kung'uta vizuri kabisa, toa folonya ulifue, fua mashuka yako then pasi kwa moto mkali,
You are good to go,

Short cut, nunua dawa za kuua wadudu, pulizieni humo ndani, hazizidi buku 5, kwa watu wanne ni 1250 each,

Tuache kulalamikia vitu vidogo tunavyoweza solve wenyewe, sisi sio toddlers bana
Hakuna kunguni atakufa hapo.
Dawa ya kunguni chukua mafuta ya taa changanya na sabuni ya unga weka kwenye spray gun,nyunyizia ...hutaona kunguni hata mmoja...
 
Acha kudeka,

Chukua heater, chemsha maji mengi ya moto, osha hivyo vitanda kwa maji moto kila kona,

Chukua godoro lako, kung'uta vizuri kabisa, toa folonya ulifue, fua mashuka yako then pasi kwa moto mkali,
You are good to go,

Short cut, nunua dawa za kuua wadudu, pulizieni humo ndani, hazizidi buku 5, kwa watu wanne ni 1250 each,

Tuache kulalamikia vitu vidogo tunavyoweza solve wenyewe, sisi sio toddlers bana
Hilo unalosema ni rahisi kufanya nyumbani kwako,kwa maeneo ya public kama chuoni n.k ili utokomeze kunguni inatakiwa eneo lote lifanyiwe fumigation,ukifanya wewe peke yako basi uamue hakuna mtu kukalia kitanda chako na wewe usikae kwenye vitanda vya wenzio,vinginevyo utapiga dawa mwaka mzima na kunguni hawataisha...
 
Mambo mengine ni kuchoshana tu. Hao kunguni mmewaleta wenyewe kutoka majumbani kwenu, halafu mnakuja kuusumbua uongozi wa chuo kuwatokomeza!!

Yaani watu wanapambania elimu yenu, wanapambania usalama wenu hapo chuo! Bado mbawabebesha tena mzigo wa kupambana dhidi ya kunguni, mliokuja nao kutoka majumbani kwenu!!

Kama vipi jichangisheni ili mpate dawa ya kuwaua. Inauzwa shilingi elfu 6 tu.
Hapana.Institution ina responsibility ya kuhakikisha wakazi kwenye nyumba zake wanaishi confortably How,ndio wajipange sasa na vikanuni,elimu nk
 
Sina haja ya kutaja jina langu wala kuandika maelezo mengi, lakini kwa ufupi mimi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwakweli suala la kunguni UDOM limekuwa linasumbuwa na lina kera kwa muda mrefu.

Ajabu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sasa wadudu hao wamekuwa wengi sana yaani nahisi hata Ufaransa tunaposikia wamefunga vyuo hawajafikia huku, ni kero sana.

Kunguni hao wanapatikana kwenye mabweni tunapolala, mfano kwenye college ya Education ndio balaa.

Siku za nyuma uongozi wa chuo ulikuwa na kawaida ya kupuliza dawa kwenye mabweni, lakini ndani ya miaka hii miwili hali imekuwa tofauti.

Tulipofunga Chuo Juni na Julai 2023 tulitegemea tukirudi tutakuta wamepuliza dawa lakini hali imekuwa tofauti, matokeo yake watu tumeanza kulazimika kutandika na kulala chini kwani vitandani hakulaliki.

Changamoto hii sio kwenye college yetu pekee bali karibia zote Wanafunzi tumekuwa tukilalamika kunguni.

Majibu ya UDOM yako hapa: Uongozi wa UDOM wajibu madai ya kuwepo kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi
VC anajua hilo?
Mkuu wa Chuo DR TAX anajua?
 
Kwa vile hao wanafunzi wanalipa ada hivyo basi uongozi was chuo wenyewe inabidi uwajibike for it but, it seems ndo yaleyale as if zile shule za kata kata ikishajengwa ndo imeisha iyo no maintenance nor wat 😂
Wizara ya elimu kiujumla inajifanya kuelemewa na mambo mengi lakini sio kwel coz kila mtu kwwnye uongozi huenda ikawa anajjua lakin he /she don't care for it yote hiii sababu tu mambo ya serikari yanajisahau
 
😂😂
Sina haja ya kutaja jina langu wala kuandika maelezo mengi, lakini kwa ufupi mimi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwakweli suala la kunguni UDOM limekuwa linasumbuwa na lina kera kwa muda mrefu.

Ajabu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sasa wadudu hao wamekuwa wengi sana yaani nahisi hata Ufaransa tunaposikia wamefunga vyuo hawajafikia huku, ni kero sana.

Kunguni hao wanapatikana kwenye mabweni tunapolala, mfano kwenye college ya Education ndio balaa.

Siku za nyuma uongozi wa chuo ulikuwa na kawaida ya kupuliza dawa kwenye mabweni, lakini ndani ya miaka hii miwili hali imekuwa tofauti.

Tulipofunga Chuo Juni na Julai 2023 tulitegemea tukirudi tutakuta wamepuliza dawa lakini hali imekuwa tofauti, matokeo yake watu tumeanza kulazimika kutandika na kulala chini kwani vitandani hakulaliki.

Changamoto hii sio kwenye college yetu pekee bali karibia zote Wanafunzi tumekuwa tukilalamika kunguni.

Majibu ya UDOM yako hapa: Uongozi wa UDOM wajibu madai ya kuwepo kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi
Kama wazungu wanateseka na kunguni sisi ni nani😂😂
 
Kunguni wa bongo ni himilivu. Kuna siku wameniparamia pale block G kunguni kama hamsini hivi wale wadogo wadogo halafu nikakuta wao wafugaji wameshawazoea wala hawaguswi.
Maafisa ufugaji kunguni🤣🤣🤣
 
𝐀𝐧𝐲 𝐰𝐚𝐲 𝐜𝐡𝐮𝐤𝐮𝐚 𝐦𝐚𝐟𝐮𝐭𝐚 𝐲𝐚 𝐭𝐚𝐚 𝐥𝐢𝐭𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐧𝐠𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐜𝐡𝐮𝐦𝐯𝐢 𝐯𝐢𝐣𝐢𝐤𝐨 𝐯𝐢𝐰𝐢𝐥𝐢 𝐰𝐞𝐤𝐚 𝐧𝐚 𝐨𝐦𝐨 𝐤𝐢𝐠𝐚𝐧𝐣𝐚 𝐜𝐡𝐚𝐤𝐨 𝐤𝐨𝐫𝐨𝐠𝐚 𝐯𝐢𝐳𝐮𝐫𝐢 𝐭𝐡𝐞𝐧 𝐦 𝐭𝐨𝐛𝐨𝐚 𝐦𝐟𝐮𝐧𝐢𝐤𝐨 𝐰𝐚 𝐜𝐡𝐮𝐩𝐚 𝐲𝐚 𝐩𝐥𝐚𝐬𝐭𝐢𝐤𝐢 𝐧𝐲𝐮𝐧𝐲𝐮𝐳𝐢𝐚 𝐯𝐢𝐱𝐮𝐮𝐫𝐢 𝐡𝐚𝐥𝐚 𝐧𝐢𝐭𝐚𝐟𝐮𝐭𝐞 𝐏𝐌 𝐭𝐮𝐨𝐧𝐠𝐞𝐞 𝐯𝐢𝐱𝐮𝐫𝐢.
 
Sina haja ya kutaja jina langu wala kuandika maelezo mengi, lakini kwa ufupi mimi ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Kwakweli suala la kunguni UDOM limekuwa linasumbuwa na lina kera kwa muda mrefu.

Ajabu ni kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa sasa wadudu hao wamekuwa wengi sana yaani nahisi hata Ufaransa tunaposikia wamefunga vyuo hawajafikia huku, ni kero sana.

Kunguni hao wanapatikana kwenye mabweni tunapolala, mfano kwenye college ya Education ndio balaa.

Siku za nyuma uongozi wa chuo ulikuwa na kawaida ya kupuliza dawa kwenye mabweni, lakini ndani ya miaka hii miwili hali imekuwa tofauti.

Tulipofunga Chuo Juni na Julai 2023 tulitegemea tukirudi tutakuta wamepuliza dawa lakini hali imekuwa tofauti, matokeo yake watu tumeanza kulazimika kutandika na kulala chini kwani vitandani hakulaliki.

Changamoto hii sio kwenye college yetu pekee bali karibia zote Wanafunzi tumekuwa tukilalamika kunguni.

Majibu ya UDOM yako hapa: Uongozi wa UDOM wajibu madai ya kuwepo kunguni kwenye mabweni ya Wanafunzi
Kuna kale kajamaa feki kanajiita Sheikh Kishiki au Kisiki, majuzi alikuwa anakashifu shule za Wafaransa kuwa na kunguni na kuwa Mungu ndiyo aliwatumia hao kunguni, sisi je hapa Dom ni Mungu ndiye aliyefanya hivi kwetu na kwanini?
 
Back
Top Bottom