Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

Kunuka kikwapa: Fahamu chanzo, tiba na namna ya kuepuka tatizo

Jasho la mtu halinuki, kinachosababisha harufu ni byproduct inayotokana na maisha ya bacteria. Njia ya kwanza ya kupambana na kikwapa ni usafi. Anyoe makwapa kila mara, aoshe na sabuni walau mara tatu kutwa. Ndimu na white vinegar, kama acid inasababisha pH kuwa ndogo na hivyo kusababisha bakteria kufa. Kama ulivyoambiwa sugua na ndimu ama vinegar b4 kuoga na ukishaoga futa kwapa vema na kisha tumia deodorant. Kwa kweli harufu ya kikwapa inakera,mkipambana nayo itaisha tu! kila la kheri

Ushauri huu nimeupenda si wa kilozi ni "kisayansi zaidi" Big up King'asti. Mbinu hii ikidunda, Chinchilla kaa chini ufikiri. Kama umeweza mwaka na nusu basi hicho kikwapa hakina nguvu kwako, go on with your relation. Halafu ujue ni vile pia anakupenda, wewe umekurupuka kuja kutangaza humu, unadhani na yeye hana mapungufu yako? au kwa vile hajasema? Usitafute kisingizio, utaumia mbeleni ukaja juta.
 
He he he, mie nachagua option ya kukaa ndani bila nguo na kujipepea, afu nimepanga rum 1 na wapo mabachala 4.

Nshapata kisingizio cha kuwategea

Msisahau pia maji katika mwili ni kitu muhimu sana, lita tatu hadi nne kwa siku, punguza spicy foods, caffeine na alcohol, au chochote kinachodehydrate mwili wako. A dehydrated body smells bad especialy kikwapa kinachoacha vitu vyeupevyeupe kwapani, au vinavyoacha alama ya njano kwenye shati jeupe.

Kunywa maji kadri uwezavyo, kiyoyozi nyumbani kama unaweza kinasaidia, tembea sehemu za vivuli au kaa ndani bila nguo na ujipepee.

Whatever it takes not to dehydrate urself.
 
He he he, mie nachagua option ya kukaa ndani bila nguo na kujipepea, afu nimepanga rum 1 na wapo mabachala 4.

Nshapata kisingizio cha kuwategea
Dah!! We uko freaky sana, unawataka wote kwa mpigo?
 
ANTI-PERSPIRANTS SI NZURI KWA AFYA YA BINADAMU NA ZINASABABISHA MADHARA MAKUBWA KAMA BREAST CANCER COZ ZINAZUIA JASHO KUTOKA. PIA ZINA Alluminium AMBAYO SI NZURI KWA AFYA YA BINADAMU

Well...kama ni madhara basi hakuna kitu ambacho hakina madhara. Hata maji yana madhara vile vile lakini mbona bado tunakunywa?

Supposedly hata cell phones zina madhara lakni mbona hatuachi kuzitumia? Au hujasikia madai kuwa zinasababisha saratani ya ubongo?

Anyway, kama anti perspirants zina madhara au la hakuna conclusive proof kuonyesha hilo. Na kwa jinsi Marekani ilivyoendelea kisayansi na teknolojia, kama kweli kungekuwa na conclusive proof kuwa zinaleta au zinasababisha saratani za matiti basi nina uhakika wa asilimia 100 FDA (Food and Drug Administration) ingekuwa isha act zamani sana.

Ni mara ngapi FDA wana issue recalls za product flani flani kwa sababu zina madhara na kadhalika? Lakini nenda US uone jinsi anti perspirant deodorants zilivyojaa madukani. Si kwenye pharmacies, si kwenye grocery stores, si kwenye beauty shops, si kwenye gas and service stations, anti perspirant deodorants are everywhere. Kama kuna agency ingine duniani ambayo inaaizidi FDA na CDC (Centers for Disease Control and Prevention) hebu zitaje hapa tuzilinganishe.

Vivyo hivyo Ulaya. Nenda Boots kama uko UK uone ma anti perspirant deodorants yalivyojaa. Kwa hiyo, hizo habari za kusema kwamba eti zina madhara na ni mbaya hazina ushahidi wa kutosha kulithibitisha hivyo. Ndiyo yale yale ya cell phones na kompyuta.

Tunaambiwa hata kompyuta ni mbaya. Zina madhara. Sijui zina mionzi gani inayoharibu macho na seli mwilini na blah blah nyiiiingi. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba hakuna conclusive proof. Mwisho wa siku nadhani baadhi ya haya madai huwa ni propaganda tu za ma environmentalists.
 
Namaanisha atayewahi ndo huyo huyo
ila kompetita wakiwa wengi dau hupanda zaidi
Nina uhakika kuna moja ndiye unaemtegea, wakinadada siku zote wanaju nani watampa darasani, mtani, kazini, roommates wanajua yupi ni sexy na ndiowanawategea. Ila yako kali,inaonekana pesa ndiyo itayotembeza mkia.

I kinda liked it.
 
Da kuna magonjwa yakustajabisha! kuna demu nlikua nampata, yeye 2kiwa chuo ukipishana nae ata km hujamwona,unajua ni namba imepita! yaani bora m2 ajambe frequently kuliko kwapa! sasa ukute uko 6 ukapat ako kaarufu mashine inafyata!
 
Ushauri huu nimeupenda si wa kilozi ni "kisayansi zaidi" Big up King'asti. Mbinu hii ikidunda, Chinchilla kaa chini ufikiri. Kama umeweza mwaka na nusu basi hicho kikwapa hakina nguvu kwako, go on with your relation. Halafu ujue ni vile pia anakupenda, wewe umekurupuka kuja kutangaza humu, unadhani na yeye hana mapungufu yako? au kwa vile hajasema? Usitafute kisingizio, utaumia mbeleni ukaja juta.

Nimie, mie natafuta dawa wala sijaja kumuanika mpenzi wangu humu!

mie ndiyo najua matatizo nayopata
 
Siyo tu atumie deodorant. Anachotakiwa kutumia ni 48 hr clinical strength ANTI-PERSPIRANT deodorant. Kuna tofauti baina ya deodorant na ANTI-PERSPIRANT deodorant.

Mtu kmwenye tatizo kubwa la kikwapa deodorant pekee haitasadia kuondoa tatizo. Inapaswa atumie deodorant zinazokata utokwaji wa jasho kwenye kwapa na hizo ndiyo ANTI-PERSPIRANT deodorants.

Baadhi ya watu huwa hawajui hilo. Wakiona tu container lina neno deodorant basi anakimbilia kununua. Sasa deodorants zisizo anti perspirant ingredients huwa haziko effective kwa watu wenye vikwapa vinavyotema na ndiyo maana utakuta watu wanalalamika kuwa wamejaribu kutumia deodorant lakini wapi.

Ni muhimu sana kusoma ni deodorant ya aina gani mtu unanunua. I always recommend ANTI-PERSPIRANT deodorants.

Mkubwa Ngabu, Nashukuru sana kwa ushauri wako taufanyia kazi!
 
Niliwahi kusikia lakini sijui kama ni kweli eti dawa ya kienyeji ya kikwapa hata kiwe kikalo vipi inachukua sufuria uliyopikia ugali kisha unailoweka na maji halafu asubuhi unaoga yale maji yaani kama unajikanda sehemu za kikwapa kabla ya kuoga kwa muda wa siku mbili tatu halafu nasikia kinapotea!

Nilisikia watu wanajadili dawa hii baada ya jamaa yangu mmoja kuwa na kikwapa na kushauriwa tumwambie afanye hivyo mambo yatakuwa mazuri!!!!

Hii dawa tulishawahi kufanya lakini hamna kitu
 
Great Thinkers.
Mimi na mpenzi wangu leo tuna mwaka na nusu toka tuwe kwenye mahusiano. Lakini napata shida sana kupambana na harufu ya kikwapa chake.

Tumejaribu kutumia kila aina ya vipodozi bado wakati mwingine nakuwa kama nazidisha harufu, mtanisaidiaje ili kikwapa kisiwepo!

Umenusa kwapa lako? Mara nyingine mtu unafikiria harufu inatoka kwingine kumbe? Inakuwa ile story ya "nyani haoni kundule".
 
Wakuu, hizo ndimu, malimao, vitunguu, kupaka kwenye makwapa havina madhara kweli?
 
Back
Top Bottom