Kunuka miguu: Chanzo na tiba

Kunuka miguu: Chanzo na tiba

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,296
Reaction score
12,972
Tatizo la kunuka miguu husababishwa na pale jasho linaposhindwa ku- evaporate na bacteria kuanza kupata mlo humo kwenye jasho la miguuni ambalo huwa katika mfumo wa organic acids na hii hutoa harufu kali sana (pungent smell).

Mara nyingi huwapata wale ambao wana miili yenye kutoa jasho jingi.

Watu wa aina hii wanapovaa viatu vinavyofunika sehemu kubwa ya miguu huku wamevaa soksi, halafu wakakaa navyo kwa muda mrefu, basi wakivua ni balaa.

Tatizo hili ni sugu sana ka wanaume, utakuta mwanaume amekutembelea ile kutoa viatu akifika nyumbani kwako au chumbani kwako tayari hapakaliki.

JINSI YA KUONDOKA NA TATIZO LA KUNUKA MIGUU

Safisha nyayo za miguu, katikati ya vidole kwa maji kwa kutumia antibacterial soap kila mara.

Tumia soksi safi na tofauti kila siku.

Pia usivae viatu pair moja kila siku.

Uwe makini na aina za viatu na aina ya miguu uliyonayo.

Hakikisha unavaa viatu safi.

Vaa ndala (thongs) unapoenda kuoga siyo unaenda kuoga umevaa viatu na ukishaoga unavaa viatu na kuingiza miguu imelowa kwenye viatu.

Pia, kuna deodorant ambazo zinasaidia zaidi kama vile Admire Deodorant Spray ambayo ndani yake ina Butane, Propane na Alcohol ambazo husaidia kukausha jasho na kuondoa harufu mbaya ya miguu na kuwa mtanashati wa uhakika na usiwe usumbufu kwa marafiki na watu wengine.

Pia unaweza kutumia corn starch powder kwenye miguu yako.

Ukiona tatizo ni kubwa Nenda kupata ushauri kwa daktari ujue kwa nini miguu inanuka.
 
Hili kweli ni tatizo kwa wengi. Hv linatibika?
 
Jf mimi ninasumbuliwa na tatizo la kutokwa na harufu mbaya kwenye miguu.najitahidi kuosha miguu na kuvaa viatu ambavyo sivyakufunika ila bado inaendele, kama kuna mwenye kujua dawa naomba msaada Wako/wenu.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Jamani makaka,

Unamkuta mkaka handsome, subiri muingie mahali muambiwe kuvua viatu, kwanza anajikanyaga kumbe socks zimetoboka, haya utamuonea huruma, sasa huo uvundo unaotoka miguuni, unaweza kumkana kuwa humfahamu. Kama umemkaribisha nyumbani kwako, ndioy inabidi ufungue madirisha ukidai ni joto, hata kama inabidi utupie kisweater na kibaridi hiki cha June. Wakinakaka ni nini hiki?
 
Kulikuwa na ukaguzi wa soksi mkuu??!!Anyway inakera sana kiukweli
 
Pole sana wengine...hili tatizo sometimes unakuta ni ugonjwa..
Kama ni ugonjwa si utibiwe? Unakuta amealikwa ubwabwa wa shughuli huku kwetu Kwamtogole lakini mwanaume anafikiria jinsi ya kuvua viatu.
 
Back
Top Bottom