CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,296
- 12,972
Tatizo la kunuka miguu husababishwa na pale jasho linaposhindwa ku- evaporate na bacteria kuanza kupata mlo humo kwenye jasho la miguuni ambalo huwa katika mfumo wa organic acids na hii hutoa harufu kali sana (pungent smell).
Mara nyingi huwapata wale ambao wana miili yenye kutoa jasho jingi.
Watu wa aina hii wanapovaa viatu vinavyofunika sehemu kubwa ya miguu huku wamevaa soksi, halafu wakakaa navyo kwa muda mrefu, basi wakivua ni balaa.
Tatizo hili ni sugu sana ka wanaume, utakuta mwanaume amekutembelea ile kutoa viatu akifika nyumbani kwako au chumbani kwako tayari hapakaliki.
JINSI YA KUONDOKA NA TATIZO LA KUNUKA MIGUU
Safisha nyayo za miguu, katikati ya vidole kwa maji kwa kutumia antibacterial soap kila mara.
Tumia soksi safi na tofauti kila siku.
Pia usivae viatu pair moja kila siku.
Uwe makini na aina za viatu na aina ya miguu uliyonayo.
Hakikisha unavaa viatu safi.
Vaa ndala (thongs) unapoenda kuoga siyo unaenda kuoga umevaa viatu na ukishaoga unavaa viatu na kuingiza miguu imelowa kwenye viatu.
Pia, kuna deodorant ambazo zinasaidia zaidi kama vile Admire Deodorant Spray ambayo ndani yake ina Butane, Propane na Alcohol ambazo husaidia kukausha jasho na kuondoa harufu mbaya ya miguu na kuwa mtanashati wa uhakika na usiwe usumbufu kwa marafiki na watu wengine.
Pia unaweza kutumia corn starch powder kwenye miguu yako.
Ukiona tatizo ni kubwa Nenda kupata ushauri kwa daktari ujue kwa nini miguu inanuka.