Mercedes wametengeneza M139 2L I4 engine yenye displacement ya 2000cc, hii engine inatoa 416bhp na inapatikana kwenye Mercedes AMG A45S, inaipa uwezo wa kutoka 0-100kph ndani ya sekunde 3.9 na speed ya juu 270kph.
Ukilinganisha na ngongingo Toyota 3UR FE yenye 5700CC na nguvu farasi 381bhp inayoitoa Land cruiser 200 Series kutoka 0-100kph ndani ya sekunde 6.6 na speed ya juu 220kph.
Ukweli ni kwamba CC au ujazo wa engine si kila kitu, nimeamua kulinganisha Toyota Land Cruiser VX-R na Merc AMG A45s kwa sababu ya utofauti wa ukubwa wa miili na engine zilizopo kwenye hizi gari.
Hapa tunakuja kwenye suala la uhusiano uwezo wa engine Horsepower dhidi ya uzito wa gari husika, Toyota Land Cruiser 3UR FE inatoa 381bhp kubeba 3350kg ina maana 3350kg÷381bhp=7.9 ina maana kila horsepower inabeba kilo 7.9.
Upande wa AMG A45S, M139 inatoa 416bhp kubeba uzito wa 1,642kg÷416bhp=3.95 ina maana kila horsepower inabeba kilo 3.9.
Hiyo ndiyo Ratio kati ya nguvu ya engine dhidi ya uzito inaobeba, leo hii ukimchukua Hussain Bolt ukamtwika begi lenye kilo 50 alafu ukamshindanisha na binti wa miaka kumi na mbili kwenye mbio za mita mia moja, Bolt atapoteza shindano hilo. Power to Weight Ratio. Hii imepelekea watengenezaji wengi wa magari kutumia composites kama Carbo Fiber, PVC plastics, ili kupunguza uzito wa baadhi ya panels na ata rim/wheels. Uzito wa gari ni kitu muhimu sana na huchangia mengi sana kwenye uwezo na mwenendo wa gari kwa ujumla.
Tofauti na uwezo au ukubwa engine watu wengi wanasahau umuhimu wa Gearbox/Transmission zipo aina nyingi za Gearbox, na kila moja imetengenezwa tofauti kulingana na mahitaji yanayodhaniwa, ZF 8 speed imekua ikizitesa sana Aisins kwenye drag races.
Pia kama unawaza kuhusu uwezo wa engine pekee kukupa kasi na performance ya gari, usisahau kuhusu Aerodynamics, sijui kwa kiswahili inaitwaje lakini kiufupi ni uhusiano kati ya muundo au umbo la gari na ukinzani wa nguvu ya upepo, hapa ndipo gari kama Toyota Land Cruisers zinapofeli, landcruisers na SUV nyingi ni shape za box na zipo juu hivyo kwenye kasi zinakumbana na nguvu kubwa ya upepo kwa maana miwili ua hizi gari haipo na muundo wa kupenya kwenye mawimbi ya upepo.