Kununua hisa Tanzania ni kucheza kamari

Kununua hisa Tanzania ni kucheza kamari

Bora hata wewe CRDB wanasikika, nilinunuaga precision air, tangu nilivyonunua miaka mitano iliyopita sijawahi hata kuwasikia wanaongelea habari za hisa, ila kiukweli hali ni mbaya
Duh pole sana mkuu. Umenikumbusha mambo ya precision air...hatari sana, hapo ndo ujue nchi yetu bado changa sana.
 
Mkuu wake wa kitengo alikuwa pale BOT akiongoza kurugenzi ya 'Risk management', sasa sijui kwa nini hamshauri!
Tatizo naamini anaona anajua kila kitu.anafanya anachokiona kinafaa kwa mda na ku win cheap rating ya mda huo na kusahau long term impact and damages! nchi yetu yenyewe imegeuka risk kwa investors wa ndani na nje.
 
Sio Tanzania tu duniani kote kununua hisa ni kucheza kamari.

Kama unataka uwe na uhakika wa asilimia kubwa kaweke kwenye Treasury bills ambazo zinakupa interest ya uhakika , japokuwa hutapata nyingi kama kwenye hisa ambapo mambo yakienda vizuri unapata gawio na capital gain.
Hisa sio kamari kama misingi ya biashara na uwekezaji inazingatiwa. Kikubwa hapa ni matamko yenye kuathiri biashara za watu tofauti na kwingineko ambako biashara zinaathiriwa na sababu za kibiashara na si siasa.

Utanunua hisa za kampuni ya simu ikiwa kuna kampuni moja pinzani inapigiwa upatu na mamlaka kukamata soko?

Utanunua hisa za kampuni ya cement ikiwa kuna kampuni mojawapo pinzani inawekewa mazingira pendelezi ya kuwezesha uzalishaji kwa unafuu zaidi ya kampuni nyingine?

Utanunua hisa za benki ya kilimo na maendeleo vijijini ikiwa tayari mamlaka zinapendekeza amana ziwekwe kwenye benki nyingine pinzani?

Shida hapa sio BUSINESS TREND, shida ni POLITICAL FLAMES
 
Duh pole sana mkuu. Umenikumbusha mambo ya precision air...hatari sana, hapo ndo ujue nchi yetu bado changa sana.
Yap kweli namimi hao jamaa wa Precision niliwasahau.toka wakose mtaji zaidi na kupata hasara wamewatia umaskini wanahisa wao
 
Bora hata wewe CRDB wanasikika, nilinunuaga precision air, tangu nilivyonunua miaka mitano iliyopita sijawahi hata kuwasikia wanaongelea habari za hisa, ila kiukweli hali ni mbaya
mkuu uwekezaji kwa nchi yetu unaathiriwa na serikali inayokuwa madarakani.Serikali haina mtizamo wa kuwasaidia wanahisa na wenye kampuni.wao ni kupata chao na kukaa pembeni.hata stimulus package ili kampuni iendelee kusimama hawatoi.hawa Precision nakumbuka waliomba hela serikalini takribani 50bn mpaka kesho hawajapewa.
 
Binafsi kwa sasa siwezi nunua hisa hata watangaze nyumba kwa nyumba.

Ni kitu kipo wazi, Drop iliyoonekana DSE pekee inatosha kuonesha picha ya miezi inayokuja
unabusara na upo smart. watu wanaingia kichwakichwa kunyolewa
 
Kushuka kwa Mauzo kwny Soko la Hisa kwa zaid ya 30Billion kwa Mwezi Mmoja tu Nchi zingine Waziri wa Fedha na wa Viwanda na Biashara 'wangesharudisha Mpira kwa Kipa' lakin kwa Bongo hata Media hazijaona kuwa ni habari ya kuwekwa kwny front page ya Magazeti Yao!

Hata huu Uzi kwa kuwa unazungumzia hisa hautopata wachangiaji wa kutosha! [emoji12]
kweli nchi zinazojari wananchi angekubali kujiuzuru kuwa amekosa mkakati wa kunusuru uwekezaji wa wananchi.wao kwa akili zao ndogo wanadhani wanaumiza wale big investors wenye big shares kumbe wahanga pia ni sisi tunaochagizwa kumiliki uchumi wa nchi kupitia hisa.
 
Hisa sio kamari kama misingi ya biashara na uwekezaji inazingatiwa. Kikubwa hapa ni matamko yenye kuathiri biashara za watu tofauti na kwingineko ambako biashara zinaathiriwa na sababu za kibiashara na si siasa.

Utanunua hisa za kampuni ya simu ikiwa kuna kampuni moja pinzani inapigiwa upatu na mamlaka kukamata soko?

Utanunua hisa za kampuni ya cement ikiwa kuna kampuni mojawapo pinzani inawekewa mazingira pendelezi ya kuwezesha uzalishaji kwa unafuu zaidi ya kampuni nyingine?

Utanunua hisa za benki ya kilimo na maendeleo vijijini ikiwa tayari mamlaka zinapendekeza amana ziwekwe kwenye benki nyingine pinzani?

Shida hapa sio BUSINESS TREND, shida ni POLITICAL FLAMES
exactly. shida ipo ikulu
 
Hashauriki yule, yeye ni kila kitu, pale mjengo kuna washauri wa kila sekta lakini anajifanyia anayoyajua yeye tu
kibaya amekusanya wasomi waliobobea wamezunguka serikali yake nzima lakini anayaamini mawazo yake wasomi kawaweka pale kupunguza ukosoaji mitaani.
 
Yaani nilinunua hisa CRDB mwaka juzi kwa bei ya TZS 380 kwa hisa, juzi nimeangalia ili niongeze hisa kidogo nizimie. Yaani ngoma imeshuka by 50% inauzwa TZS 180 kwa hisa. Nimechoka kabisa kabisa!! Sasa inabidi niwekeze kwingine...sijui Dangote anauza hisa.
Hiyo CRDB Jamaa hataki hata kuisikia anaona anamkomoa C.E.O kumbe anangamiza wananchi wanaomiliki hisa kule.Haachi huduma na nguvu ya soko iamue ubora wa benki.
 
Kushuka kwa Mauzo kwny Soko la Hisa kwa zaid ya 30Billion kwa Mwezi Mmoja tu Nchi zingine Waziri wa Fedha na wa Viwanda na Biashara 'wangesharudisha Mpira kwa Kipa' lakin kwa Bongo hata Media hazijaona kuwa ni habari ya kuwekwa kwny front page ya Magazeti Yao!

Hata huu Uzi kwa kuwa unazungumzia hisa hautopata wachangiaji wa kutosha! [emoji12]
Niwatetee watanzania walio Wengi mkuu haya tunayoyapigia kelele ndo yanachangia kushuka kwa soko hisa .mtu anaweza asilalamike direct kuhusu DSE lakini anacholalamika kina impact kwenye kuporomoka kwa soko la hisa.
 
Kwenye uzi kama huu hauwezi kumuona Lizaboni.
Nilikuwa najadiliana na mdau mmoja wa soko la hisa, alionesha wasiwasi wake kuwa hizo hisa zilizo katika Initial Public Offer (IPO) kwa sasa, ziko "over-priced". Wanunuzi wanaweza kuwa wananunua brand, lakini huko mbele hakutabiriki. Nadhani ni kampuni ya kwanza katika DSE iliyomwaga shares nyingi kiasi hicho!
 
Back
Top Bottom