Kununua magori au kudhamini michezo kwa mamilioni, wengi ni kusafisha matendo yao machafu.

Zygot

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2016
Posts
2,319
Reaction score
3,128
Ukiangalia hisoria ya wanasiasa na wasio wanasiasa, Wanajiingiza ktk kufurahisha umma kupitia michezo, ili kuwasahaulisha juu ya matendo yao machafu. Historia inao watu wengi wa aina hii na wengine huenda wamejulikana kuliko wengine.

Pablo Escobar, muuza cocain mashuhuri wa dunia, alijihusisha sana na jamii. Akajenga nyumba zilizoitwaBarrio Pablo Escobar, akajenga shule na makanisha ya kikatoliki ambayo ndo pendwa kwa nchi za amerika ya kusini. Aligawa hata pesa kwa maskini na akajulikana kwa jina la ’The Boss’. Yote ilikuwa ni kusafisha jina lake ili atetewe na jamii kwamba ni mwema.

Katika siasa pia wapo akina Winnie Mandela na Timu yake ya Mandela United Football Club ambayo aliitumia vizuri kufanikisha malengo ya kisiasa, lakini baadaye alihusishwa na mauaji ya kijana mdogo, Stompie Seipei.

Daniel Ortega wa Nicaragua pia aligawa pesa na chakula kwa umma na kuita Zero hunger.
Nayib Bukele wa El Salvador alianzisha Casa Para Todos; nyumba kwa maskini.
Al Capone wa US alikuwa kiongozi wa makundi ya kiharifu pia, alianzisha hata supu za bure kwa aliowaitwa wenye njaa, na kugawa pesa kwa wenye uchumi mbaya.

Sasa tuangalie nchi yetu hii. Tumefikia hatua rais ananunua magori ya mpira wa miguu, Pembeni unaona shule haina madawati. Ukiangalia wadhamini wa ligi pia ni wafanyabiashara wanaoitwa ni 'wakubwa’. Unadhani wanapenda sana michezo kiasi cha kupoteza pesa zote hizo? Je kuna faida gani ktk maisha ya biashsrs zao? Inaweza iwe kusahaulisha madhaifu yao ktk jamii. Yaani kila wakati kuwe na kundi linalowatetea.
 
Magori ni nini?
Anyway, wazungu kuna muda huwa wanatucheka sana, imagine mtu kaja umkopeshe milioni1.

Baada ya muda katika pitapita zako, unapita sehemu unakuta kuna ndondo cup na uliyemkopesha anajinadi atatoa laki1 kwa kila goli unajisikiaje!
 
r & l ni shida ktk kiswahili. Lakini kuna kitu inaitwa cognitive processing of words, inaturuhusu kusoma na kuelewa bila kuangalia usahihi wa herufi.

Aoccdrnig to a rscheearch at Cmabrigde Uinervtisy, it deosn’t mttaer in waht oredr the ltteers in a wrod are...
 
Ukiangalia hisoria ya wanasiasa na wasio wanasiasa, Wanajiingiza ktk kufurahisha umma kupitia michezo, ili kuwasahaulisha juu ya matendo yao machafu. Historia inao watu wengi wa aina hii na wengine huenda wamejulikana kuliko wengine.

Pablo Escobar, muuza cocain mashuhuri wa dunia, alijihusisha sana na jamii. Akajenga nyumba zilizoitwaBarrio Pablo Escobar, akajenga shule na makanisha ya kikatoliki ambayo ndo pendwa kwa nchi za amerika ya kusini. Aligawa hata pesa kwa maskini na akajulikana kwa jina la ’The Boss’. Yote ilikuwa ni kusafisha jina lake ili atetewe na jamii kwamba ni mwema.

Katika siasa pia wapo akina Winnie Mandela na Timu yake ya Mandela United Football Club ambayo aliitumia vizuri kufanikisha malengo ya kisiasa, lakini baadaye alihusishwa na mauaji ya kijana mdogo, Stompie Seipei.

Daniel Ortega wa Nicaragua pia aligawa pesa na chakula kwa umma na kuita Zero hunger.
Nayib Bukele wa El Salvador alianzisha Casa Para Todos; nyumba kwa maskini.
Al Capone wa US alikuwa kiongozi wa makundi ya kiharifu pia, alianzisha hata supu za bure kwa aliowaitwa wenye njaa, na kugawa pesa kwa wenye uchumi mbaya.

Sasa tuangalie nchi yetu hii. Tumefikia hatua rais ananunua magori ya mpira wa miguu, Pembeni unaona shule haina madawati. Ukiangalia wadhamini wa ligi pia ni wafanyabiashara wanaoitwa ni 'wakubwa’. Unadhani wanapenda sana michezo kiasi cha kupoteza pesa zote hizo? Je kuna faida gani ktk maisha ya biashsrs zao? Inaweza iwe kusahaulisha madhaifu yao ktk jamii. Yaani kila wakati kuwe na kundi linalowatetea.
Hii ni shida inayoongezeka sana ktk nchi. Imefikia hatua inaonekana kama hata kiongozi wa kitaifa hajui umuhimu wa matatizo ya wananchi wake. Kama anaamua kununua magoli, kweli bajeti ya Taifa anatoa mchango wa kuliendeleza taifa?
 
Back
Top Bottom