Kununua ndege bila business plan ni kufuja fedha za maskini

Kununua ndege bila business plan ni kufuja fedha za maskini

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Biashara ya ndege ni moja ya biashara ngumu zaidi duniani. Hii ni biashara yenye mahesabu makali. Ni biashara ya kimataifa.

Kufanikisha biashara ya ndege tunahitaji timu yenye weledi mkubwa sana kibiashara. Wazungu Afrika Kusini wamepata changamoto kubwa na hasara pia, Wanaigeria, Wamisri na Wakenya wanasusua kwenye biashara ya ndege, hasara imetawala. Hata British Airways, Air France na American Airlines wanapata changamoto kuendesha biashara ya ndege kwa hasara sasa kwa miaka mingi.

Ndege sio kwa ajili ya kupaki viwanjani, wataalamu wanasema ili upate faida kutokana na biashara ya ndege, ndege inatakiwa itumie muda mwingi wa maisha yake (>75%) ikiwa angani.

Tangu ndege zetu kubwa zinunuliwe, nyingi zimepaki viwanjani, muda mwingi zikiwa ardhini kuliko angani, hii ni hatari na hasara kubwa! Je, tuna business plani au tunanunua ndege kwa ajili ya mapambo?
 
Back
Top Bottom