Mpaji Mungu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2023
- 13,544
- 43,537
Kariakoo mambo ni mengi sana!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hopeless kbsaKunitaja katika Mada za Kipuuzi na za Wapuuzi ni Kunidhalilisha tu Mkuu sawa? Sipendi na Sijapenda.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] utafanyaje think tank la mkoa wenu
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Hahahhaha et bonge la kofi la kichwani[emoji1787][emoji1787],any way ungenishtua[emoji116][emoji116][emoji116]
Karibu kwa Lewis MVincent upate huduma zifuatazo kila siku:
[emoji419]Nakununulia,nakufungia na kukusafirishia bidhaa kutoka kariakoo kwenda mitaa yote ndani ya Dar es salaam na mikoa yote Tanzania.Huduma hii unaipata kwa tsh 10000/= tu.
[emoji419]Nakutafutia bidhaa pamoja na bei zake za jumla na reja reja ndani ya soko la kariakoo.Huduma hii unaipata kwa tsh 2000/= tu.
[emoji419]Nakutafutia basi au lori zuri pamoja na gharama zao kwaajili ya kusafirisha bidhaa zako kutoka kariakoo kwenda mikoa yote Tanzania kwa uharaka na usalama zaidi.Huduma hii unaipata kwa tsh 5000/= tu.
AGIZA BIDHAA KAMA:
-Simu aina zote
-vifaa vya simu aina zote mfano: chaji,covers,protectors.
-Vifaa vyote vya kieletronic kama TV,SABUFA,SPEAKER,FRIJI,HEATER nk
-Vyombo vya ndani aina zote
-Nguo za kiume za watu wazima aina zote
-Nguo za kike za watu wazima aina zote
-Nguo za watoto aina zote
-Nguo za ndani aina zote mfano chupi,sidiria,boksa nk
-Urembo aina zote kama heleni,bangiri,kacha,saa nk
-Vipodozi na mawigi
-Vifaa vya stationary aina zote.
-Vifaa vya ushonaji aina zote kama cherehani,vitambaa,vitenge,sindano,nyuzi nk
-Material ya furniture aina zote.
-Vijora
-Mitumba aina zote
-CD na Movies kwa wale ote wenye library
-Hardware na Vifaa aina zote vya ujenzi.
-Spea za pikipiki na bajaji
-Baiskeli aina zote
-Betri na matairi aina zote
-Mashine za bekari
-Vifaa na material ya keki aina zote.
-Mapazia na mashuka aina zote.
-Mabegi,pochi na mikoba aina zote
-Viatu aina zote
-Na bidhaa zinginezo ambazo sijataja hapa.
MAWASILIANO: 0745645035 (PIGA/SMS/WHATSAPP).
KARIBU SANA KWA HUDUMA BORA NA ZA UHAKIKA KILA SIKU MASAA 24.
UAMINIFU NI MTAJI,OKOA MUDA NA GHARAMA ZA NAULI KWA KUNIAGIZA MIMI BIDHAA AINA ZOTE KUTOKA KARIAKOO KWENDA MITAA YOTE NDANI YA DAR ES SALAAM NA MIKOA YOTE TANZANIA KILA SIKU.
Nguvu zipo...Mkuu kama uko vizuri lete hizo nguvu niunganishe na zangu ninazozifahamu tumshughulikie,amenidhalilisha sana yule mjinga
Unakuwa mtumwa wakiumbe nawe ni walewale tu washirikini….watu wengi wenye tamaa za dunia hii wameamua kuwa watumwa wa shetani. pamoja na kuonekana kuwa na mali nyingi, ili wana shida balaa! Binafsi nimeamua kuwa mtumwa wa Yesu. hata kama tutapitia magumu neema yake inatufunika na tunakuwa na amani moyoni. tunasonga mbele na mwishoni tunaurithi uzima wa milele.
YESU NI MWOKOZI
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.
Wiki iliyoisha nilikuwa na mtoko wa kuelekea mahali fulani,nikasema siwezi kwenda huko bila kutupia mitupio ya Ki-Jentromeni,nikaona isiwe tabu nielekee Kariakoo ambako ningepata mavazi mazuri kwa bei nzuri iliyoendana na bajeti yangu.
Sasa nilipofika Kariakoo ikabidi nizunguke kwenye maduka kadhaa nikajichukulia mavazi yangu,kuna duka moja niliingia ndani nikamkuta mwanamke mmoja mweupe ambaye kimuonekano wa uso alikuwa mweupe na mzuri,sasa kuna shati moja zuri nilikuwa nimelipointi lilikuwa limening'inizwa kwa juu,hivyo baada ya kumuuliza bei nikamwambia anitolee ili niangalie kama lingenitosha nilichukue,aliponyanyuka kwenye kiti nikagundua ni aina ya mwanamke ambaye alikuwa amevimba juu na chini kapigwa pasi,OK!,akalitoa lile shati na nikalichukua nikalifungua vifungo ili nilivae.
Sasa wakati nimelivaa lile shati huku nikiendelea kufunga vifungo,nilikuwa najaribu wakati huo kupepesa macho uenda ningeona lingine zuri nimwambie anishushie,aiseeee kufumba na kufumbua nikaona kuna dogo mmoja anatoka mle dukani anakuja pale mbele ya lile duka anatiririka kamasi si mchezo huku akiwa ananifanyia ishara ya kwamba anahisi njaa,kiukweli nilihamaki sana na nikashituka,nilipozidi kumuangalia yule maza ni kama alishituka akaniambia
Maza " kuna nini ?"
Mimi " Huyo dogo humuoni?"
Baada ya kumwambia hivyo yule mwanamke alichomoka pale dukani kuoingia kwenye chemba ya mlango wa duka ilipokuwa stoo,sasa pale kwenye ule mlango wa kuingilia huko stoo kulikuwa kumetundikwa mashati na ilikuwa vigumu sana kuona kuna mlango hadi alipofunguq yule dogo wakati anatoka,yule mwanamke akazama ndani na hakumaliza muda akawa ametoka,alipotoka nikaona anachukua maji yaliyokuwa kwenye chupa anajipaka mkononi na mengine nadhani alikunywa,Aiseee ndipo sasa nadhani akamuona yule dogo,akamchukua akamrudisha mle dukani kisha akafunga ule mlango wa stoo kwa mbele uliojazwa mashati mengi,baada ya kutoka huko kuna wateja wengine walifika pale,sasa yule maza akaanza kuniwashia moto.
Maza " Rudisha shati langu na uondoke hapa nisije kukuitia mwizi"
Mimi " Mama kuna nini?"
Niendelea " Mbona tumekubaliana ni elfu 15!,shida ni nini?"
Maza "Nimekwambia ondoka au wewe mwizi nini!"
Aiseee kama mjuavyo,kulikuwa na wateja wengine pamoja na wale madogo wanapangaga tu ndala na tusendo kwenye tule tu meza wakawa wamesikia wakajaa mle dukani.
Madogo " Mama Mungi nini shida?"
Yule Maza " Huyu kaka namwambia aondoke dukani kwangu lakini hasikii"
Aisee wale madogo walianza kunizonga zonga huku wakidhani mimi ni mwizi,ajabu ni kwamba yule maza hakutaka kabisa nijielezee wala kuwaelezea wale watu ni kitu gani kilijiri.
Jamaa Mmoja " Kama amekataa kukuuzia wewe angalia ustaarabu wako maduka yako mengi"
Aliendelea "Au kibaka nini mwanetu"
Kuna jamaa akanishushia bonge la kofi kichwani lakini bahati nzuri kuna watu ambao walikuja nikiwa bado pale dukani wakanitetea wakasema "Jamaa kama ameshindwana bei na bi mkubwa Hampaswi kumpiga muacheni akatafute maduka mengine"
Pamoja na hayo lakini nilikuwa nikijitetea,kilichosaidia ilikuwa muonekano wangu!.Aiseee yule mama kumbe nilipomuona yule dogo ndiyo niliharibu kabisa na nadhani ni Mungu tu lakini vinginevyo nilikuwa napigika vibaya sana hadi kuchomwa moto.
Yule mwanamke nimeshampeleleza na anaishi Mbezi Tangi bovu,sasa nitakachomfanya hatokuja kusahau na lazima atakuja kunipigia magoti.Na yeye ndiye atakayenipa mtaji wa Bajaji,subiri uone
Nimeteseka sana na hii siri lakini leo nimeona niwaeleze wakurungwa ya duniani huko.
Hapo Kariakoo kunanuka ushirikina.
[emoji23]Hahahaha mi nikiona thread zako nafurahi tu
Sasa kama uko ulipigwa likibao na ukufanya kitu utamuweza master GENTAMYCINE si atakuvunja mbavu
Case ya wanga hiyo kawaida.
Think tank gn? Kilaza wa kutupa huyu juhaThink tank la mkoa mzima musoma ,Mara [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mara umuite mshamba mara umuite dogo Janja..😅😅😅Kipya sio nyuzi yako hii inaweza ikawa chai kama chai zingine naona umeota kiburi skuhizi dogo ila huna jipya kwenye biashara ya mtu akikufukuza huna haja ya kubisha mara mbili upo town ila mshamba stuka dogo janja
Yaani mkuu ukimueleza mtu hawezi elewa mpaka ajionee mwenyeweumenikumbusha mbali sana ndugu yangu,....nikiwa mlowo kipindi hicho ipo bado ndani ya mkoa wa mbeya, tuliingia dukani mimi na binamu zangu wawili....muuzaji alikuwa mzee wa makamo mwanaume, amekaa kwenye kiti cha plastic...wote tukamsalimia mzee then tukaomba atupatie counter books 📚 tisa...mzee akiwa anahangaika na ngazi kupanda kutuchukulia mzigo wetu kwenye shelvu za juu, ghafla nikamwona mmama mmoja amekaa kwenye kiti kinginge cha mbao kilichopo kwenye moja ya kona ya duka kwa utulivu wa hali juu mno ndani ya mavazi ya rangi ya damu ya mzee mchanganyiko na nyeusi,..nikadhani hatukumuona hapo kabla sababu ya haraka zetu,...nikamsalimia yule mama shikamoo mama,.hakujibu..ajabu ni kuwa wale binamu zangu wawili wakaniuliza unamsalimia nani, ndipo na yule mzee kusikia hivyo akageuka na kukuta hamna mteja yeyote zaidi yetu,. nayeye tena akaniuliza, hiyo mama shikamoo unampatia nani, muda huo ameshachukua zile counter books 📚 anazihesabu,..nikajibu kirahisi tu,...si yule mama pale kwenye kona,...mzee alihamaki isivyo kawaida..binamu zangu wakaanza kucheka na kusema umechanganyikiwa mbona hamna mtu yeyote pale kwenye kona, nilishituka lakini ajabu bado nilikuwa nikiendelea kumuona ,alitupatia mzigo wetu chap tukampa pesa na kusepa, tukiwa tunaondoka mzee aliniita , we kijana mrefu njoo hapa, akauliza wewe n mwenyeji wa hapa nikajibu hapana,....kwenu wapi?... nikamtajia...akaniambia tu,..naomba usije tena dukani hapa, sikutaka mambo mengi kwani tayari nami niliingiwa na hofu na hata hivyo nilikuwa chaliii sana kwa kipindi hicho...niliondoka chap..siku kama tatu mbeleni hakufungua duka ,kwani mjombA alikuwa akienda kumcheki kuhoji nn kilitokea mpaka akafikia maamuzi hayo...mjomba na huyo muuzaji walikuwa wakifahamiana kiasi, na hivyo baada mjomba kusimuliwa mkasa huu alitaka kujua zaidi.....haya mambo ni bahati mbaya sana huwezi kuthibitisha kirahisi mbele ya umma,..but it's just (KUA UYAONE)
Pole muraNsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!.
Wiki iliyoisha nilikuwa na mtoko wa kuelekea mahali fulani,nikasema siwezi kwenda huko bila kutupia mitupio ya Ki-Jentromeni,nikaona isiwe tabu nielekee Kariakoo ambako ningepata mavazi mazuri kwa bei nzuri iliyoendana na bajeti yangu.
Sasa nilipofika Kariakoo ikabidi nizunguke kwenye maduka kadhaa nikajichukulia mavazi yangu,kuna duka moja niliingia ndani nikamkuta mwanamke mmoja mweupe ambaye kimuonekano wa uso alikuwa mweupe na mzuri,sasa kuna shati moja zuri nilikuwa nimelipointi lilikuwa limening'inizwa kwa juu,hivyo baada ya kumuuliza bei nikamwambia anitolee ili niangalie kama lingenitosha nilichukue,aliponyanyuka kwenye kiti nikagundua ni aina ya mwanamke ambaye alikuwa amevimba juu na chini kapigwa pasi,OK!,akalitoa lile shati na nikalichukua nikalifungua vifungo ili nilivae.
Sasa wakati nimelivaa lile shati huku nikiendelea kufunga vifungo,nilikuwa najaribu wakati huo kupepesa macho uenda ningeona lingine zuri nimwambie anishushie,aiseeee kufumba na kufumbua nikaona kuna dogo mmoja anatoka mle dukani anakuja pale mbele ya lile duka anatiririka kamasi si mchezo huku akiwa ananifanyia ishara ya kwamba anahisi njaa,kiukweli nilihamaki sana na nikashituka,nilipozidi kumuangalia yule maza ni kama alishituka akaniambia
Maza " kuna nini ?"
Mimi " Huyo dogo humuoni?"
Baada ya kumwambia hivyo yule mwanamke alichomoka pale dukani kuoingia kwenye chemba ya mlango wa duka ilipokuwa stoo,sasa pale kwenye ule mlango wa kuingilia huko stoo kulikuwa kumetundikwa mashati na ilikuwa vigumu sana kuona kuna mlango hadi alipofunguq yule dogo wakati anatoka,yule mwanamke akazama ndani na hakumaliza muda akawa ametoka,alipotoka nikaona anachukua maji yaliyokuwa kwenye chupa anajipaka mkononi na mengine nadhani alikunywa,Aiseee ndipo sasa nadhani akamuona yule dogo,akamchukua akamrudisha mle dukani kisha akafunga ule mlango wa stoo kwa mbele uliojazwa mashati mengi,baada ya kutoka huko kuna wateja wengine walifika pale,sasa yule maza akaanza kuniwashia moto.
Maza " Rudisha shati langu na uondoke hapa nisije kukuitia mwizi"
Mimi " Mama kuna nini?"
Niendelea " Mbona tumekubaliana ni elfu 15!,shida ni nini?"
Maza "Nimekwambia ondoka au wewe mwizi nini!"
Aiseee kama mjuavyo,kulikuwa na wateja wengine pamoja na wale madogo wanapangaga tu ndala na tusendo kwenye tule tu meza wakawa wamesikia wakajaa mle dukani.
Madogo " Mama Mungi nini shida?"
Yule Maza " Huyu kaka namwambia aondoke dukani kwangu lakini hasikii"
Aisee wale madogo walianza kunizonga zonga huku wakidhani mimi ni mwizi,ajabu ni kwamba yule maza hakutaka kabisa nijielezee wala kuwaelezea wale watu ni kitu gani kilijiri.
Jamaa Mmoja " Kama amekataa kukuuzia wewe angalia ustaarabu wako maduka yako mengi"
Aliendelea "Au kibaka nini mwanetu"
Kuna jamaa akanishushia bonge la kofi kichwani lakini bahati nzuri kuna watu ambao walikuja nikiwa bado pale dukani wakanitetea wakasema "Jamaa kama ameshindwana bei na bi mkubwa Hampaswi kumpiga muacheni akatafute maduka mengine"
Pamoja na hayo lakini nilikuwa nikijitetea,kilichosaidia ilikuwa muonekano wangu!.Aiseee yule mama kumbe nilipomuona yule dogo ndiyo niliharibu kabisa na nadhani ni Mungu tu lakini vinginevyo nilikuwa napigika vibaya sana hadi kuchomwa moto.
Yule mwanamke nimeshampeleleza na anaishi Mbezi Tangi bovu,sasa nitakachomfanya hatokuja kusahau na lazima atakuja kunipigia magoti.Na yeye ndiye atakayenipa mtaji wa Bajaji,subiri uone
Nimeteseka sana na hii siri lakini leo nimeona niwaeleze wakurungwa ya duniani huko.
Hapo Kariakoo kunanuka ushirikina.
Peleka chuki Yako hukoMama Mungi Ni mchaga piwa.halafu Kuna watu wanasema wachagga sio washirikina.
Kumbuka mazezeta mengi yanapatikana Uru kuliko sehemu nyingine yoyote Tanzania.
Vimaskin bhana vina mawazo mgando Kila tajiri ni mshirikina,mtazd kubaki maskini hivyohivyoWa Uru wenyewe.
Ukikutana nao Dar watakuambia kwao Ni Old Moshi.