Dogo mmoja dereva wangu wa Bajaj akataka kwenda kuoa kwa hawa watu,hakutaka mbwembwe sijui za magari na nini yeye akachukua kijiweni kwake vijana wenzake kumpa kampan ya kumbebea ndugu zake kwenda ukweni kujitambulisha,Bajaj zilikuwa kama sita hivi.
Kufika gate lilipo na ilipo nyumba ya wakwe (ndani ya fence) ni zaidi ya 100 mt sasa ule muongozano wa vile vibajaj mule ndani wale wahaya wakaona ajabu nikasikia mmoja wao(baadae kwenye mazungumzo nilikuja kugundua ni mjomba mtu) akisema kwa lafudhi yao “iih bhojo,hutu tudude twa walemavu tumefuata nini humu ndani,we mujuni ka-press alarm switch pale watu wajiandae kwa mapambano,raabda tumevamiwa”,mwengine akadaki “ina maana ndugu yetu anaolewa na mulemavu”mi nilivyosikia tu ile lafudhi na yale maneno nikamwambia oya dogo hapa mke hamna.