Kuolewa ni Heshima kwa Mwanamke

Kuolewa ni Heshima kwa Mwanamke

Sad generation....

Kuoa hakubadili chochote kwa mwanaume zaidi ya kuongeza majukumu... Hakuna furaha yoyote huko... Kama umeshindwa kuipata furaha kabla hujaoa na utegemee ukioa ndio utaipata nikupe POLE..

Kwa ground vitu huwa ni tofauti sana...

Maoni tu,,, don't take it personal.
Nakazia!
 
KUOLEWA ni heshima kwa mwanamke


Heshima hiyo inaenda mbali zaidi hadi kuwagusa wazazi wa binti ambaye ataolewa. Wazazi wanatembea kifua mbele pindi binti yao anapoolewa, tena wanafurahia zaidi binti huyo anapoolewa akiwa angali bado hajazaa.

Wanamshukuru Mungu kwa binti yao kujitunza. Wanamshukuru binti kwa kuwapa heshima katika familia yao na ndiyo maana siku ya sherehe ya kuagwa (send off) wazazi wanafurahi sana kuagana na binti yao kwa heshima.

Hali hiyo huwa inaleta shauku kubwa kwa warembo wengi kutamani kuingia kwenye ndoa. Wengi wanaguswa na rekodi za wanawake wenzao ambao wamejitunza na hatimaye kuwaletea heshima wazazi wao.

Kinyume chake, wengi wamejikuta wakijilaumu kwa kushindwa kuleta heshima katika familia zao. Binti umri unaenda, anatamani kuingia kwenye ndoa lakini hapati wa kumuoa. Au mwingine inatokea, anatamani kuolewa lakini anaishia kupigwa mimba na kuachwa.

Badala ya kuleta heshima, analeta aibu katika familia yake kutokana na mila na desturi zetu kumtaka binti azae pale tu atakapokuwa ameolewa. Azae pale atakapokuwa kwa mumewe na si vinginevyo. Inapotokea bahati mbaya basi ni mara moja na si kuzaa na kuzaa watoto kibao.

Pamoja na kuwa ndoa ni mpango wa Mungu lakini hivi umeshawahi kujiuliza wanaolewa wanakuwa na sifa gani? Kwa nini wanaume wanavutiwa nao? Wanakuwa na kitu gani cha ziada ambacho wanawake wengine hawana? Leo nitakuambia!
Jamani, sifa ya kwanza ambayo mwanamke anapaswa kuwa nayo ni ile hulka ya kuwa mke. Wanaume wengi huwa wanapenda kuishi na mwanamke ambaye ana ile sifa ya kuwa mke. Ninaposema sifa ya kuwa mke naamisha mwanamke ambaye atakuwa tayari kumlea mume na hata watoto.

Mwanamke ambaye atakuwa msaada kwa mwanaume wake pindi atakapokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo za maisha pamoja na maradhi. Mwanamke ambaye atajua thamani ya mume, ambaye atajua nini maana ya heshima kwa mumewe.

Mwanamke ambaye atamudu misukosuko ya maisha ikiwemo kufilisika, kuachishwa kazi na mengine magumu yanayofanana na hayo. Mwanamke ataka-yevaa sifa ya kuwa mke kwa maana ya kumhudumia mumewe pindi atakaporudi amechoka kutoka kazini.

Wanaoolewa ni wale pia ambao wanajua kushuka pindi wanapoona kumetokea kutoelewana. Wanawake wale ambao wanajua kumtoa uchovu wa maisha mwanaume. Mwanamke ambaye hasababishi makelele ya mara kwa mara kwenye ngoma za masikio ya mwanaume.

Mwanamke ambaye hana gubu. Mwanamke atakayeelewa kwamba muunganiko wa ndoa una pande mbili hivyo kuwajali ndugu wa pande zote mbili, ndugu zake na ndugu wa upande wa mumewe. Mwanamke ambaye atakuwa na muonekano wa mke kwa maana ya mavazi na hata mazungumzo.

Wanaoolewa jamani wanakuwa na sifa ya uvumilivu. Wanakuwa na hofu ya Mungu. Mwanamke mwenye hofu ya Mungu, anamuomba yeye ampatie mwanaume mcha Mungu na kweli inatokea. Kuna siri kubwa sana katika kumuomba Mungu ambayo wengi wetu hatuijui lakini ni vyema kumtanguliza yeye katika kila jambo.

Ukiwa na sifa hizo, hata kama hautakuwa na muonekano wa kimisi au kuwa na shepu bomba kama wanavyosema vijana wa kisasa, utaolewa tu na hizo ndizo sifa za mwanamke anayetaka kuolewa!
Sasa hivi wanataka kuheshimiwa kila mahala, na wao wanataka kuonekana ni wabeba majukumu, waolewe na nani?

Wamekua na viburi chungu mzima achana nao, muheshimu mama yako tu ambaye nae ana shida zake Kwa BABA
 
Sasa hivi wanataka kuheshimiwa kila mahala, na wao wanataka kuonekana ni wabeba majukumu, waolewe na nani? Wamekua na viburi chungu mzima achana nao, muheshimu mama yako tu ambaye nae ana shida zake Kwa BABA
G 'taxi, mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanaume, mwanaume ni mwanaume tuh, cha msingi muwe mnawapenda wake zenu wenyewe watawaheshimu.
 
Huo ndio uhalisia, japo katika jamii siku hizi, wanaepuka mapunguwani kadhaa kuonesha ndoa sio kitu cha maana, lakini hapo hapo anataka huyo anaezini nae awe wa kwake pekee yake, kama ndoa haina maana tufanye kama kuku na wanyama wengineo, tuone kama watoto watakuwa na baba.

Sisi wanaume tuna mchango katika hili pia, siku hizi wanaume weengi hatujitambui ama kutimiza wajibu wetu ndani ya ndoa, wanawake hawapati haki zao vema.
Mkuu lakini mnaweza kuwa kwenye ndoa na bado asiwe wa kwako peke yako unaliongeleaje hili?. Kwamba anakuwa wa kwako kwa jina tu "mke wangu" ila nyuma ya pazia mna share na mtu
 
Kawaida tu tusikuze Mambo,Sasa umeolewa na mwanaume mwasherati anatongoza kila kitu hata mbuzi, irresponsible,mleviii mbwa,kila siku maugomvi,utasema ndoa Ni heshima?Tumeshuhudia mauaji mangapi ya hao wanandoa kuuana? Sema hivi,kibahatika kupata anayeeleweka sawa ukilamba garasa huwezi kuwa proud na hiyo ndoa.
 
Hebu waache wachuchu waendelee kuwa 'singo' wakiolewa wote kutakuwa na uhaba mkubwa sana wa micheps [emoji3526]
 
Mkuu lakini mnaweza kuwa kwenye ndoa na bado asiwe wa kwako peke yako unaliongeleaje hili?. Kwamba anakuwa wa kwako kwa jina tu "mke wangu" ila nyuma ya pazia mna share na mtu
Hilo lipo, inategemeana na mwanamke uliyechukja ukichukua jini litakunyonya damu tu.
 
Kawaida tu tusikuze Mambo,Sasa umeolewa na mwanaume mwasherati anatongoza kila kitu hata mbuzi, irresponsible,mleviii mbwa,kila siku maugomvi,utasema ndoa Ni heshima?Tumeshuhudia mauaji mangapi ya hao wanandoa kuuana?
Sema hivi,kibahatika kupata anayeeleweka sawa ukilamba garasa huwezi kuwa proud na hiyo ndoa.
Kwa nini ukubali kuolewa na garasa?
 
Heshima kubwa sana! Ila kwa sasa Heshima inapungua kwa sababu mambo ya ndani yote yanafanyika nje ya Ndoa,Siri iliyobaki ndani ya Ndoa ni Migogoro tu.
 
Kama Kuolewa ni Heshima kwa Mwanamke, Je mwanaume kuoa ni nini?
Ni hasara make utatoboka kila siku...hasa mke km hana kismart ndo ivo tena...utakuwa maskini milele km mke wa Lowasa huyu hafai alitema jamaa uwaziri mkuu ivi ivi!!..ila alimlilia mumewe saaana. Kwa mkosi ule.....mke wa ukweli ni Mama kikwete yaani fulll kismart!! Mmewe Hawajawahi pigika .wale...jk nyota iliwaka mazimaaaa!! Mpaka sasa......si unaona na vibinti vyake vimeolewa vyoote! Af hawana mapigano.
 
Back
Top Bottom