Uchaguzi 2020 Kuomba kura kwa ukabila CCM hii imezidi. Msukuma awaambia wana Geita kwa kisukuma mnamwachaje mtoto wenu mnachagua asiye wa kwenu

Uchaguzi 2020 Kuomba kura kwa ukabila CCM hii imezidi. Msukuma awaambia wana Geita kwa kisukuma mnamwachaje mtoto wenu mnachagua asiye wa kwenu

Inasikitisha na kuhuzunisha kura za Magufuli zinaombwa kwa ukabila na eneo analotoka.

Leo yuko Geita cha ajabu kikabila kinatumika kuomba kura tena kwa vijembe kwa kusema inakuwaje mnataka kumchagua asiye wa nyumbani kwenu usukumani na kasema kwa kuwa tunafahamiana kwenye mikutano yao wakija ole msukuma ahudhurie baada ya Uchaguzi wataonana.

Huu ukabila tume ya Uchaguzi haioni kuwa ni kuligawa taifa?
wiki iliyopita katoa rushwa ya ajira elfu 13 za walimu, jana katoa rushwa ya ujenzi wa barabara wakati akifanya kampeni. NEC kimya!

hapa itafutwe intervention kutoka UN hakuna namna.
 
Na sisi hatuwezi kumuacha Wenje ni mtoto wetu japo yupo upinzani.
 
Inasikitisha na kuhuzunisha kura za Magufuli zinaombwa kwa ukabila na eneo analotoka.

Leo yuko Geita cha ajabu kikabila kinatumika kuomba kura tena kwa vijembe kwa kusema inakuwaje mnataka kumchagua asiye wa nyumbani kwenu usukumani na kasema kwa kuwa tunafahamiana kwenye mikutano yao wakija ole msukuma ahudhurie baada ya Uchaguzi wataonana.

Huu ukabila tume ya Uchaguzi haioni kuwa ni kuligawa taifa?
Kama na wewe ni mgombea na wewe omba kura kwa lugha yako hakuna shida.
 
Hivi Mwadila ndio Habari za asubuhi ? Acha nichukue mafunzo maana huko mbeleni kinaweza kuwa ni mtaji
 
Inasikitisha na kuhuzunisha kura za Magufuli zinaombwa kwa ukabila na eneo analotoka...
SHERIA GANI YA NCHI INAZUIA MTU KUSEMA LUGHA YAKE ? AU MNAKURUPUKA KWA KUKOSA CHA KUANDIKA ? JOSEPH KASHEKU MSUKUMA BAADA YA KUONA KUNDI KUBWA LILILOPO MBELE YAKE HALIELEWI VIZURI KISWAHILI AMETUMIA LUGHA YA KWAO KUWAFIKISHIA UJUMBE NA UJUMBE UMEFIKA KOSA LIKO WAPI?
 
Ngoja tuende kwa staili hii,tusio wasukuma wote tuungane kumchagua mtu wetu maana Mgombea wa wasukuma tunamsikia na kumuona anavyojinadi. Tundu ccm wanakuongezea pointi tembea na biti hii
 
Siwezi kukulaumu Kwa sababu pia wajinga nao ni binadamu, nao ni wa mhimu, Kwa kuwa watu wooote duniani wangekuwa welevu, Neno Ujinga lisingekuwepo, lakini lipo Kwa kuwa wajinga kweli Wapo, Wewe ni mmoja wa hao wajinga wasioelewa hata maana ya kile mtu ameuliza,

Yaani hata hapo hjaelewa?
Ongeza lishe labda unaweza kuondokana na upumbuvu wa udumavu wa uelewa, nimekupuuza rasimi sasa!
Kampuuze mama yako aliyekuzaa na mtindio wa ubongo!
 
Tulieni Dawa Iwaingie Kwani Ubaya upo wapi nyie Mbona mnaongea Kingerezaaa
mtumbwi ukianguka hauangalii ni nani alikuwa dereva..., wote waliomo wanaloa maji....,

Hivi unadhani naongelea kabila lililotumika kuongea kilichoongelewa au ninaongelea kilichoongelewa..., huenda hapa fikra zetu zikawa kwenye wavelength tofauti...., kwahio mwisho wa siku ni vigumu kuelewana
 
Ila nani alitumbia Ukabila ni mbaya?
Kabila sio baya ila Ukiongezea U kwenye kabila ndio shida, na si kabila tu chochote kinachotenga wao na sisi kwa kuweka umimi au usisi kwenye jamii ndio mwanzo wa chuki na utengano
 
Kwa hiyo hii nayo umeona hoja ya kuibua na kuianzishia uzi? Mtu kuuliza kuwa itakuwa ajabu kutochagua mtoto wa nyumbani ni kosa?
Kwa akili yako hii unaona kawaida
Ila impact yake itakuwa kubwa na madhara makubwa
 
Unategemea mawazo gani kutoka kwa mtu wa darasa la 7?
 
Musoma alikemea ukabila kumbe hata hakumbuki jana tu ameongea kitu gani. Jamani na sisi huku hakuna kumpa kura kwa sababu siyo ndugu yetu. Bora wale wengine wasio na uelekeo wa ukabila tutawapa.
 
Ni kawaida, kule nimewahi kuishi, kuna wazee kule hawajiu Kiswahili hata cha kuombea maji tu. Acha tu mkuu waombwe Kura Kwa lugha Yao ileile!! Na nadhani hakuna ubaya Ila tu mtizamo tu ulionao wewe
Kuwa "mnamwachaje mtoto wenu na kuchagua wageni" ni sawa maneno haya ya kibaguzi kwenye kampeni?

Vv
 
Wanaombea wenyewe mikutanoni kumejaa watoto tupu
IMG_20200909_135653.jpg
IMG_20200907_224431.png
 
Back
Top Bottom