Kwa hiyo kwa akili yako unaamini matajiri huwa wanazitoa tu hizo laki 5 wakiombwa za harusi ? Hakuna tajiri wa hivyo labda huko kwenu Sitimbi.kua maskini ni kitu mbaya sana,
yaani kuchangia laki2 au laki5 mtu anaejiskia uchungu utadhani nini sijui,
huna mchango sema wazi huna, sio kuahidi kinafiki na kushauri mambo ambayo ni ni wazi ni mbinu ya kukwepa kuchangia harusi 🐒
Masikini ndio wachangiaji wakubwa wa hizo sherehe.Sababu za Masikini kuwa wachangiaji (1)Kutarajia na wenyewe kuchangiwa hapo baadae (2)Kutarajia kuhudhuria sherehe ya harusi ili akanywe ,akale misosi na akajionyeshe. Masikini anachangia harusi sio kwa sababu anapenda maendeleo ya bwana/bibi harusi bali ili ajionyeshe na akale, akanywe kwenye hiyo sherehe na ndio maana bwana/bibi harusi utanuniwa miaka yote kama umechangiwa na hujaweka sherehe hata kama aliekuchangia yuko mbali.
Sababu zipo nyingi ila jua tu mambo ya sherehe ni mambo yako binafsi na ndugu zako na unakuwa unayapanga kufanya ukiwa na afya njema kabisa, hivyo tafuta hela zako ndio uweke sherehe na sio kuunga watu whatsap group bila ridhaa na kuanza kusumbuana kwa meseji.