Kuomba mchango wa harusi ni matusi makubwa

Kuomba mchango wa harusi ni matusi makubwa

Jumapili au Jumamosi funga ndoa kanisani rudi nyumbani na mwenzi wako muishi kwa amani na furaha. Nendeni ofisi ya DC fungeni ndoa mrudi nyumbani muishi kwa amani.
Au fungeni ndoa nyumbani kwa binti murudi nyumbani mukaishi kwa amani.
Kama unataka kufanya sherehe ruksa, fanya kwa uwezo wako. Mchangishane wana familia, hiyo ndio heshima na busara. Marafiki mutualike tu, kwakuwa tunajua mnaanza maisha hatutakuja mikono mitupu. Pesa mtapata ambazo mtafungulia biashara au kuanza ujenzi. Vyombo mtapata pia.
Hii ya kukabana michango mwisho wa siku ikipatikana millioni 20 yote wanakula ma MC, wapambaji, catering, wapiga picha nyie mnabakiwa na laki 6 .
Hakuna zawadi ya maana rafiki au workmate alitetoa mchango atakuletea.
Sherehe utaiandaa kulingana na kiasi cha fedha. Wengine wameanza maisha ya ndoa kwa mkosi wa madeni .
Hiyo ndoa itajaa madeni, madeni, madeni mpaka ivunjike.
Baeelezee!!
 
michango ya harusi ina create significant amount of jobs?, hizo kazi zitaendelea kuwepo, hizo forced contributions si njia smart ya ku create jobs
mmh nisije nikawa nafanya conversation na midoli ya Elon Musk (AI is real)😀 , yaani kuna watu ndyo maisha yao, how can you creat jobs from unsuspecting contributors
 
Back
Top Bottom