Kuomba ufafanuzi kuhusu hii habari iliyopostiwa East Africa tv

Kuomba ufafanuzi kuhusu hii habari iliyopostiwa East Africa tv

Gotze Giyani

Senior Member
Joined
Feb 28, 2022
Posts
143
Reaction score
213
#HABARI Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.Deus Sangu ametangaza kuanza kutumika kwa Muundo mpya wa Utumishi wa Maendeleo ya kada za Uuguzi na Ukunga ifikapo mwezi Julai mwaka huu.

Sangu ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Aprili 10, 2025 Mkoani Iringa wakati akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kisayansi na Mkutano Mkuu wa 54 wa Chama Cha Wauguzi Tanzania unaofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia leo kukiwa na jumla ya Washiriki 1500.

Amesema kutokana na changamoto za muundo huo, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais. UTUMISHI na Utawala Bora , Baraza la Uuguzi na Ukunga na Vyama vya Kitaaluma ilipitia muundo huo na kurekebisha changamoto zilizokuwepo na hivi sasa upo tayari kwa hatua za utekelezaji.

Katika hatua nyingine Mhe.Sangu ameziagiza Mamlaka za ajira nchini ifikapo Mei 31, 2025 zihakikishe zinawasilisha orodha ya Watumishi wanaostahili kupandishwa vyeo wakiwemo wauguzi na wakunga huku akisisitiza kuwa bajeti ya kiasi cha Sh. Bil.207 zimeshatengwa kwa ajili ya upandishaji vyeo

Wakati huo huo, Mhe.Sangu amezitaka Mamlaka za Ajira nchini kuhakikisha orodha ya Watumishi wakiwemo Wauguzi wanaodai malimbikizo yao yawasilishwe ifikapo Mei 31, 2025 yakiwa yamehakikiwa ili yawasilishwe Hazina kwa ajili ya taratibu za malipo

Akizungumzia suala la uhaba wa Watumishi wa Kada hiyo ya Wauguzi, Mhe.Sangu amesema Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha Uongozi amewekeza vya kutosha kwenye sekta ya afya ikiwemo vifaa tiba na miundombinu ya afya.

Awali, Rais wa Chama cha Wauguzi, Bw. Alexander Baluhya amesema uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye sekta ya afya lakini umekuwa hauendani na huduma zinazotolewa kutokana na uhaba wa Wauguzi na hivyo kupelekea wananchi kupata huduma zisizoridhisha.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe.Peter Serukamba amewataka Wauguzi hao kufanya kazi kwa weledi huku akiwasisitiza umuhimu wa kujiendeleza ili kujitafutia maarifa mapya kutokana na mabadiliko makubwa ya teknolojia yanayotokea duniani kote.

#EastAfricaTV
 
Mama mitano tenaaaa😄😄😄😄 ..
Hatimaye ajira mpya zimetokaa Ili mama apitee bilaa choyoooo.....
 
Back
Top Bottom