Kuombwa talaka gerezani

Kuombwa talaka gerezani

Ni wakat Sasa magereza yetu kuweka utaratibu wa kukutana kimwili walau Mara moja kwa mwezi na mke au mume

Hata Kama angeacha mali uraiani lazima wangemgegedea tu miaka nane n mingi Sana
Humans rights watch walikuwa wanadili ni hii kitu kuona kama kuna uwezekano wa kuliruhusu hili huko magerezani
 
Aisee walikuwa na mtihani mzito, mwenyezimungu awafanyie wepesi
 
Lakini kwa mtazamo mwingine. Huyu ni Sheikh maana yake ana Watu wengi nyuma yake. Kwa nini kama vile walivyokuwa wanakuja kusikiliza kesi yangu Mahakamani au kuniona mahabusu walishindwa angalau kuchanga chochote kila Mwezi kusitiri familia za Masheikh.

Huu ni unafiki wa hali ya juu sana. Yaani Watu walalamike, walaumu, waandike ubaya wa Serikali kuhusu hili lakini wasikumbuke kuwa Masheikh wameacha familia nyuma.
 
Hv hii thread mbona kila nikiingia humu naikuta ipo juu na wachangiaji haina na mods mpo tu.
 
Mi nikikaa miaka mitatu tatu tu jela na sion raman nampa mke taraka
 
Maisha ya mapenzi na ndoa yana changamoto sana. Ila matatizo ndio kipimo cha uvumilivu. Hiki kisa cha masheikh hawa, kimenikumbusha kisa cha Ayoub kuugua hadi kubaki ulimi tu na mkewe alisimama naye.

==============
Unguja.

Masheikh wa Uamsho, wameendelea kufunguka kuhusu machungu waliyopitia, huku baadhi wakieleza namna wake zao walivyowaomba talaka wakiwa gerezani

Taarifa kutoka miongoni mwao zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa masheikh wanne kati ya 36 waliombwa talaka, huku mmoja aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina akisema baada ya kutoka amebaini aliyekuwa mkewe ameolewa na ana mtoto mmoja.

Masheikh hao waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka 14 walioachiliwa huru kuanzia Juni 15 mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kuwafutia mashtaka yaliyokuwa yakiwaka

Sheikh huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alisema: “Ilikuwa mwaka jana mke mkubwa alinifuata gerezani, nia ni kuniambia maisha magumu afanyaje? Nilikuwa mpole na kumjibu sina la kusema kwa sababu sijui hatima yangu huku gerezani.”

“Aliniomba ushauri aende wapi nikamwambia sina la kusema pia, basi akaniambia nimpe talaka na nilimpa kwa sababu aliniambia maisha magumu na hajui mimi nitatoka lini gerezani. Juzi nimerudi nikaambiwa ameshaolewa na ana mtoto mmoja.”

Alisema huyo alikuwa mkewe mkubwa ambaye alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja, lakini kwa sasa amebaki na mke mmoja ambaye ni mdogo mwenye watoto wawili, huku akitumia nafasi hiyo kumshukuru mke huyo kwa uvumilivu

“ Namsihi aendelee kunivumilia maana ndio kwanza nimerudi kutoka gerezani. Miaka minane haikuwa mepesi kwa sababu nimerudi nyumba baadhi ya mali zangu nilizokuwa nazitumia kibiashara zote zimeharibika,” alisema.

Mbali na hilo, alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa ushirikiano wao uliosaidia kesi yao kuharakishwa kusikilizwa na hatimaye kuachiliwa huru.

Jana aliyekuwa kiongozi wa Uamsho, Sheikh Mselem Ali Mselem aliswali katika msikiti wa Swahaba Mtoni Kidatu, Mjini Unguja huku waumini waliojitokeza katika ibada hiyo wakionyesha furaha yao kwa sheikh huyo.

Source: Mwananchi
Kwani walioa wakiwa gerezani? Kwanini wenzetu hawawezi kuaminiana na kuvumiliana hasa wakati wa kuhitajiana na kusaidiana? Ni mazoea ya watu wa aina hii kuacha wake zao wakipata kash kash. Je wanahofia wanachowafanyia wenzao yanapowakuta yaliyowakuta?
 
Hii nchi ilipelekwa kubaya sana
Asante kwa mama SSH kurekebisha makosa ya watangulizi wake JK na JPM (RIP)
Mbona naye anatuambia mbowe gaidi?
Au kwa sababu kalipiza upande wa pili?
 
Back
Top Bottom