Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Wasalaam!.
Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.
Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.
Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.
Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.
Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.
Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.
Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.
Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.
Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.
Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.
Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.
Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.
Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.
Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.
Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..
Mungu atusaidie.