Siwezi sikitika mtu kuzikwa na manispaa, siwezi sikitika mtu kukosa watu wa kumzika. Nasikitika mtu akifa tu, akishakufa mumzike kwa helicopter au toroli bado amekufa.
Mumzike kwenye jeneza au kwenye mkeka, amekufa. Na mazishi mazuri hayampi nafasi ya kwenda mbinguni wala kumuepusha na moto.
Kwangu mimi nikiona mtu anasikitika na kulilia maiti kuzikwa na manispaa huwa namuona weak, na taifa halijengwi na watu wa mioyo dhaifu kama huyo. Mkiwa vitani comrade akafa si lazima mbebe mwili kurudisha nyumbani kama logistics haziruhusu. Yani tuhangaike kubeba majeruhi kutoka frontline kisha tuhangaike kubeba miili ya waliokufa? Kama hakuna ceasefire ya kuchukua deceased mnachukua dogtags na vitambulisho ila miili mnazika ukouko frontline.
Nikienda sehemu kutafuta, sina ndugu wala jamaa nikatangulia ghafla bila yeyote kujua ni sahihi sana nizikwe na manispaa. Hakuna haja ya kutia huruma kwenye hilo