Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

We jichanganye uone kama utazikwa na ndugu
Sijamaanisha ishu kuzikwa na ndugu.
Hoja yangu ni utambuzi wa ndugu wa marehemu ili wafikiwe na taarifa ya status ya ndugu yao kuwa ni no more.
Hili ndio la muhimu. Kwangu unazikwaje si la muhimu.
 
Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.
We unaandika hadithi au unaandika nini? Mbona km mambo ya kusadikika tu. Manispaa gani hiyo? Mi hata sijakuelewa.
 
Mimi nikifa hata wanitupe porini niliwe na fisi sijali. Hata nizikwe kwenye jeneza la bilioni moja na mbwembwe za kila aina sijali. I am dead. Sihisi cho chote. Sipo!

Zingine zote hizi ni mbwembwe tu za binadamu za kupotezeana muda na resources...

Sasa hata misiba imekuwa ni sehemu ya kuonyeshea jeuri ya pesa. Mijeneza ya bei mbaya, sare, maua na aina ya viongozi wa dini na kisiasa watakaohudhuria...Huwa nawaonea wivu sana Waislamu. Unakata moto saa tatu asubuhi ukizubaa by saa nane mchana tayari ushazikwa...hakuna cha mbwembwe wala nini!

Haya dunia nzima ilikusanyika Afrika Kusini kumzika Mandela. Mbwembwe zote zile zilimsaidia nini Mandela?

Rubbish!
Hey! Who do you think cares about your physical body? Issue hapa ni roho au the soul ndiyo ina kila kitu. Mwili wetu ni boksi tu iliyotengenezwa kwa different proportions and composition of earth
Jenga imani
 
Upande wangu mwezi June mwaka huu nilihudhuria mazishi ya ndugu mmoja aliyefariki huko DSM akaletwa kuzikwa huko kwao nilipokuwepo kama mgeni tu. Yule ndugu aliniuma kwakweli maana alizikwa na Serikali ya mtaa imagine.

Ndugu walikuwepo na wachungaji + mashehe ila hawakuhusika katika kumzika kwa sababu ya Kwanza toka akiwa kijana hakua akishiriki ibada ya kanisa wala msikiti japo alikuwa anafahamika kama mkristo.

Iliniuma aiseee yaani hata ile sala au dua ya mwisho hakusaliwa, yaani kama tumefukia mbwa aliyegongwa na gari.
Dua/sala ya mwisho inamsaidia nn marehemu?
 
Gerezani?

Sidhani. Kwa kadri nijuavyo, Gerezani wakati unaingizwa unaandika wosia. Si ya mali zako bali mwili wako. Kwamba endapo ukafariki mwili wako wakabidhiwe nani na wapi.

Maana yake, wanakuwa na taarifa zako zinakuwepo.

Hawa ni ndugu waliopata ajali ama kuuwawa. Na kwa bahati mbaya asiwepo anayemfahamu. Utazikwa kama mzoga.

Umetoka umeenda sehemu ya mbali. Kwa bahati mbaya mauti yakakukutia katikati ya harakati. Utazikwa na manispaa kama mbwa.

Inaumiza sana.
Kuna utofauti gan kati ya aliyezikwa na manispaa kama mbwa na ww uliyezikwa kwa heshima na ibada kama mangufuli alivozikwa?? Yaan huyu marehem anapata nn hasa akizikwa kwa ibada/heshima
 
Kama kweli wamefanya hivyo, nawaombea Msamaha kwa Mungu. Yeye ndiye anayejua zaidi.

Aamin na ahsante kwa dua yako Mkuu..
Unawaombea msamaha kwa kosa gan? Kwan huyo alozikwa kwa jeneza haozi?
 
IMG_0815.jpg

mkuu,Mungu akuongezee palipopungua kwa sadaka hii,kuna vichaa wengi sana nchini ila mortuary kuna mazombie.
 
Ndo maana ndugu zetu waislamu wanapenda sana sala ya kuomba mwisho mwema, Mwenyezi Mungu atujaalie mwisho mwema.[emoji120]

No mwisho mwema wanaoomba waislam sio kifo cha staha au cha starehe,ni kifo chenye nafasi ya kuomba msamaha kwa mola wako.
 
Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.

Mungu akubariki sana,hadi machozi yamenitoka
 
Hiyo ni kama mtu anaeishi mwenyewe huku akiogopa kwamba siku akifa ndani mwenyewe watu hawatajua..atajikuta ameoza tuu.hahaha ukifa mwenyewe ukaoza na ukifa mwenyewe ndugu wakijua pia wataenda kukuzika na utaoza tuu.
 
Siwezi sikitika mtu kuzikwa na manispaa, siwezi sikitika mtu kukosa watu wa kumzika. Nasikitika mtu akifa tu, akishakufa mumzike kwa helicopter au toroli bado amekufa.

Mumzike kwenye jeneza au kwenye mkeka, amekufa. Na mazishi mazuri hayampi nafasi ya kwenda mbinguni wala kumuepusha na moto.

Kwangu mimi nikiona mtu anasikitika na kulilia maiti kuzikwa na manispaa huwa namuona weak, na taifa halijengwi na watu wa mioyo dhaifu kama huyo. Mkiwa vitani comrade akafa si lazima mbebe mwili kurudisha nyumbani kama logistics haziruhusu. Yani tuhangaike kubeba majeruhi kutoka frontline kisha tuhangaike kubeba miili ya waliokufa? Kama hakuna ceasefire ya kuchukua deceased mnachukua dogtags na vitambulisho ila miili mnazika ukouko frontline.

Nikienda sehemu kutafuta, sina ndugu wala jamaa nikatangulia ghafla bila yeyote kujua ni sahihi sana nizikwe na manispaa. Hakuna haja ya kutia huruma kwenye hilo
Kabisa
 
Nimekumbuka back to 2017 dingi mzazi alinambia ata ukifa uzikwe na manispaa maan nilienda mkoa wa mbali nikawa uko kwa muda hakuna anaenijuwa, na nilimtolea shit, ila saiv tuko fresh kabisa
 
Upande wangu mwezi June mwaka huu nilihudhuria mazishi ya ndugu mmoja aliyefariki huko DSM akaletwa kuzikwa huko kwao nilipokuwepo kama mgeni tu. Yule ndugu aliniuma kwakweli maana alizikwa na Serikali ya mtaa imagine.

Ndugu walikuwepo na wachungaji + mashehe ila hawakuhusika katika kumzika kwa sababu ya Kwanza toka akiwa kijana hakua akishiriki ibada ya kanisa wala msikiti japo alikuwa anafahamika kama mkristo.

Iliniuma aiseee yaani hata ile sala au dua ya mwisho hakusaliwa, yaani kama tumefukia mbwa aliyegongwa na gari.
Maiti haki yake ni kuondoshwa. Azikwe au achomwe moto kama Wahindi yote ni sawa. Siamini katika kusalia maiti.
 
Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.
mwenyezi mungu atakupia kwa wema ulioutenda,inaumiza sana
 
Back
Top Bottom