Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

Hatari sana, na inawezekana walipofika mazikoni walitoa jeneza wakaweka pembeni halafu wakawachukua marehemu na kuwatupia wote kwenye shimo hilo moja ili watosheleze maana ukiwazika na majeneza wasingetosha shimo moja. Yale majeneza wanayauza kwa watengezaji hata wakipata elfu 20 kwa kila jeneza wao huridhika tu....cha muhimu wewe ulifanya upande wako Mungu akubariki na akukumbuke siku ya umwisho wako
Umeniwahi nilitaka kusema hivyo hivyo ilipaswa aambatane nao mpaka huko wanapowafukia
 
Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.
Ulipotoa Mwenyez Mungu atarejesha...humanity!
 
Mkuu unachobishania wala hukifahamu. Huenda ukatili uliojijengea unakamata na ufahamu wako wa kushindwa kuelewa kinachozungumziwa.

Kilichonisikitisha ni namna ndugu zetu wanavyositiriwa wakati wa kupelekwa mazikoni. Wanatupwa kama boksi. Hawaulazi hata kistaarabu.

Hakuna hata sanda ya kuwasitiri. Wanatupwa kwenye shimo moja. Kwako ni sahihi?
Sijui kama kuna sheria ya nchi ya ya kidini inayosema maiti izikwe na sanda, kwenye jeneza na shimo moja kila maiti.

Wahindi huzika kwa kuchoma moto ambavyo kwako wewe sio sahihi, kuna wazungu huchoma moto mwili na kuzika mabaki sehemu tofauti, wengine huchoma na majivu kuyapeperusha hewani na wengine majini. Sasa sijui imani yako inasemaje ambavyo hao wengine hawajulikani wana imani gani.

Kwangu mimi haina mantiki, nikifa nikazikwa kwenye sanduku la dhahabu au mkeka sitajua
 
Pole.
Lakini haijalishi umezikwaje kama mtu akifa ameshakufa. Hizo taratibu ni kwaajili yetu sisi tuliobaki...kujifariji tu lakini haina maana yoyote kwa marehemu.
Ahsante ma'am!
Ni kweli hazina maana kwa marehemu lakini kwa sisi ndugu tuliofiwa ndio zinatufariji kwamba angalau ndugu yetu yupo salama kutokana na kile tunachoamini/imani yetu.
Inauma sana nduguyo akizikwa kama mzoga!
Sisi ni binaadamu thamani yetu haiishii tunapokufa
 
Mkiwa vitani comrade akafa si lazima mbebe mwili kurudisha nyumbani kama logistics haziruhusu. Yani tuhangaike kubeba majeruhi kutoka frontline kisha tuhangaike kubeba miili ya waliokufa?
Kuna mataifa huwa hawaachi maiti zao tena wana vikosi maalumu vya kufanya hayo yaani kuhakikisha wanarudishwa wafu wao mf.Israel, hata USA..

Kama hakuna ceasefire ya kuchukua deceased mnachukua dogtags na vitambulisho ila miili mnazika ukouko frontline.
Tumeshuhudia hili huko Ukraine kwa mamia ya Warusi waliozikwa huko...

Upo sahihi lakini, waliokufa hawana fungu kwa walio hai.
 
No I don't believe in it sir. Why??
Then why do u say "living in africa is ur punishment,a hell from your past life (meaning that u were living befor n now u r living again to pay for ur previous life?.")
 
Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.
Pole sana na hongera sana.
Ila hili neno la mwisho kila topc linaniudhi mimi hata sielewi kwa nini!
Eti TUNACHOKIJUA.
 
Then why do u say "living in africa is ur punishment,a hell from your past life (meaning that u were living befor n now u r living again to pay for ur previous life?.")
I don't believe in incarnation but I do in Afterlife.
Well my pitch is pinpointed to the logic that if there's is hell and heaven when we die then Africa is our hell.
 
Acha kuamini umizimu.
Mtu akifa amekufa. Umzike usimzike hakuna kinachoongezeka wala Kupungua. Yaani workdone is equal to Zero.
Kwa kifupi hakuna ulichofanya.
Hiyo pesa uliyonunulia majeneza ungeenda kuwasaidia wagonjwa kama ilivyodesturi yako.

Lakini kusaidia miili ya wafu tena usiyoijua ni kutokuwa na Uelewa wa mambo kuhusu ulimwengu WA rohoni
 
Imani yako juu ya mambo hayo ya rohoni tunatofautiana katika mapokeo.

Ni wewe kuamini unachokiamini nami niamini kile ninachokiamini. Siku mama yako akifariki, simjui ila nikimkuta katika hali ya aibu, nitamsitiri.

Sifanyi kwa ajili ya maiti au mtu yeyote. Nafanya kwa ajili ya nafsi yangu mwenyewe. Amani ya moyo wangu.
 
Acha kuamini umizimu.
Mtu akifa amekufa. Umzike usimzike hakuna kinachoongezeka wala Kupungua. Yaani workdone is equal to Zero.
Kwa kifupi hakuna ulichofanya.
Hiyo pesa uliyonunulia majeneza ungeenda kuwasaidia wagonjwa kama ilivyodesturi yako.

Lakini kusaidia miili ya wafu tena usiyoijua ni kutokuwa na Uelewa wa mambo kuhusu ulimwengu WA rohoni
Una bwabwaja tu mkiamka mswaki kwanza
 
Sio kwa maana ya kuwa rude ama vip ila nachoamini mm ni bora kuwasaidia walio hai cos hakuna ibada wala baraka kwa kuwatendea mema waliotangulia,Najua hawakufanya kwa uwazi ila we uliona baada ya kupata view flan..

Mwisho;Ndugu tuwe responsible na miili ya marehemu wetu
 
Back
Top Bottom