Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Binadamu ni wanyama.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Niko na wewe katika hili. Mimi nina wosia kabisa. Nitakakofia nizikwe huko huko kwa namna yo yote ile isiyoleta hasara na kupoteza muda kwa waliobaki. Na sitaki mbwembwe za aina yo yote maana nyingi ni unafiki wa binadamu tu.Siwezi sikitika mtu kuzikwa na manispaa, siwezi sikitika mtu kukosa watu wa kumzika. Nasikitika mtu akifa tu, akishakufa mumzike kwa helicopter au toroli bado amekufa.
Mumzike kwenye jeneza au kwenye mkeka, amekufa. Na mazishi mazuri hayampi nafasi ya kwenda mbinguni wala kumuepusha na moto.
Kwangu mimi nikiona mtu anasikitika na kulilia maiti kuzikwa na manispaa huwa namuona weak, na taifa halijengwi na watu wa mioyo dhaifu kama huyo. Mkiwa vitani comrade akafa si lazima mbebe mwili kurudisha nyumbani kama logistics haziruhusu. Yani tuhangaike kubeba majeruhi kutoka frontline kisha tuhangaike kubeba miili ya waliokufa? Kama hakuna ceasefire ya kuchukua deceased mnachukua dogtags na vitambulisho ila miili mnazika ukouko frontline.
Nikienda sehemu kutafuta, sina ndugu wala jamaa nikatangulia ghafla bila yeyote kujua ni sahihi sana nizikwe na manispaa. Hakuna haja ya kutia huruma kwenye hilo
Watumiaji wa app ya zamani tunalazimishwa tumia app mpya ambayo inatutaka kubonyeza next kusoma storyNaomba kufahamishwa hii source 1 na source 2 ni aina gani ya mtindo mpya mjini hapa
Mkuu sikufanya ili kupata baraka. Nilifanya ili nafsi yangu ipate amani. Si kwa nia nyingine yeyote.nachoamini mm ni bora kuwasaidia walio hai cos hakuna ibada wala baraka kwa kuwatendea mema waliotangulia,Najua hawakufanya kwa uwazi ila we uliona baada ya kupata view flan..
Naam. Hili haswa ndilo linalopaswa kuwa. Lakini kama taarifa hawana, serikali iwasitiri katika namna ya faragha. Si kwa namna ile. Waheshimiwe walau kidogo.Mwisho;Ndugu tuwe responsible na miili ya marehemu wetu
Watu hawajui kuwa mtu akishakufa yake yameishia hapo.Sala haina maana yoyote kwa mtu aliyekufa. Zile ibada lengo lake ni kuwakumbusha walio hai kuenenda katika njia inayopaswa.
Naomba kufahamishwa hii source 1 na source 2 ni aina gani ya mtindo mpya mjini hapa
Ili DNA iwe sahihi yahitajika ndugu wa Marehemu pia ili waeze fanya cross match.Mwananyamala hospital hata kama hukupenda kuweka wazi jina la hospital husika... Je nimepatia?
Kwa bahati mbaya Serikali haina muda wa kufanya utambuzi wa DNA ili walau waondolewe kwenye kundi la waliopotea wasitafutwe zaidi na ndugu zao.
Kwenye kununua Sanda na JenezaChai
Kwa waliokufa Natural DeathWengine wanachukuliwa kama dead body kwa ajili ya study za mambo ya afya ( cadaver)
Imani yako juu ya mambo hayo ya rohoni tunatofautiana katika mapokeo.
Ni wewe kuamini unachokiamini nami niamini kile ninachokiamini. Siku mama yako akifariki, simjui ila nikimkuta katika hali ya aibu, nitamsitiri.
Sifanyi kwa ajili ya maiti au mtu yeyote. Nafanya kwa ajili ya nafsi yangu mwenyewe. Amani ya moyo wangu.
Tatizo la Tanzania ni huduma mbovu.Kuna siku nilikuwa Mwananyamala Hospital hao jamaa na Manispaa wakaja kushukua maiti..aisee ilikuwa imebarikika inavyoonyesha kwa sababu ya harufu ila kilichonoshangaza ni jinsi alivyowekwa kwenye gari..yaani alitupwa tu kama box vile.
All in all mtu akifa amekufa..azikwe vizuri asizikwe vizuri hilo halina maana sana.
We jichanganye uone kama utazikwa na nduguInakuaje mtu kukosa ndugu serikali ijiangalie kwa hilo. Ni mauzembe tu. Science ilisha advance ila sisi bado tupo nyuma. Lililokubwa hapa ni ndugu za maiti wawe na taarifa kwamba jamaa yao kashaondoka ulimwenguni ili wasibaki njia panda.
Pole sana, ukute hayo majeneza yarirudishwa sokoniWasalaam!.
Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.
Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.
Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.
Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.
Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.
Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.
Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.
Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.
Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.
Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.
Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.
Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.
Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.
Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.
Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..
Mungu atusaidie.
DNA hadi Mahakama iruhusu, pia DNA inaweza tumika vibaya kwa kupunguza aina fulani ya watu.Serikali imechelewa kidogo.
Inapaswa kuwa na database ya DNA ya wananchi wake wote. Kuanzia wanaozaliwa mpaka utu uzimani.
Hii itasaidia sana katika utambuzi na usalama wa raia wake. Hata pia katika swala zima la usalama.
Sasa maiti si maiti tuuWatu hao wa mochwar nadhan mioyo ishakuwa chuma.
Hata kama wanazikwa na manispaa Serikali hawawezi shindwa kuwazika vizuri.
Huyo jamaa ana matatizo ya akili hautawezana nae... Kuna kipindi alisema Marekani ndio walioumba hii dunia eti 😅😅Nimezungumzia swala lolote la kuwabakisha Mortuary?
Ambacho sikuona ni sawa ni namna maziko yao yanavyofanyika Mkuu. Wala si swala la kuwatoa humo ili wengine wapate nafasi.
Mtu asitupwe kama boksi wakati wa kupakizwa. Walau asitiriwe na Sanda. Wanapozikwa pachimbwe vizuri. Hayo si mauaji ya halaiki kwamba wazikwe kwa pamoja.
Duh!. Hayo ya poor thinking capacity yametokea wapi tena?
Izo ibada za wafu ni mapokeo tu na sio maagizo ya kwny maandiko,Mkuu sikufanya ili kupata baraka. Nilifanya ili nafsi yangu ipate amani. Si kwa nia nyingine yeyote.
Kuzika waliotutangulia ni ibada. Kwa waislamu ni faradhi.
Kwetu sisi Wakristo ni matendo ya huruma.
Naam. Hili haswa ndilo linalopaswa kuwa. Lakini kama taarifa hawana, serikali iwasitiri katika namna ya faragha. Si kwa namna ile. Waheshimiwe walau kidogo.