Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
- Thread starter
- #81
Wamarekani waendapo vitani wana msemo maarufu sana, 'Dead or alive, we will always be back home'.Siwezi sikitika mtu kuzikwa na manispaa, siwezi sikitika mtu kukosa watu wa kumzika. Nasikitika mtu akifa tu, akishakufa mumzike kwa helicopter au toroli bado amekufa.
Mumzike kwenye jeneza au kwenye mkeka, amekufa. Na mazishi mazuri hayampi nafasi ya kwenda mbinguni wala kumuepusha na moto.
Kwangu mimi nikiona mtu anasikitika na kulilia maiti kuzikwa na manispaa huwa namuona weak, na taifa halijengwi na watu wa mioyo dhaifu kama huyo. Mkiwa vitani comrade akafa si lazima mbebe mwili kurudisha nyumbani kama logistics haziruhusu. Yani tuhangaike kubeba majeruhi kutoka frontline kisha tuhangaike kubeba miili ya waliokufa? Kama hakuna ceasefire ya kuchukua deceased mnachukua dogtags na vitambulisho ila miili mnazika ukouko frontline.
Nikienda sehemu kutafuta, sina ndugu wala jamaa nikatangulia ghafla bila yeyote kujua ni sahihi sana nizikwe na manispaa. Hakuna haja ya kutia huruma kwenye hilo
Na wafafanya kila namna, mwanajeshi aliyefia katika uwanja wa vita anarudishwa nyumbani. Shushushu aliyeuwawa wakati wa kutimiza majukumu yake, hata ipite miaka mingapi, watapeleleza wajue ni wapi mwili wa mpambanaji wao ulizikwa.
Watafukua hata kama ni mabaki, kisha kuipeleka nyumbani kuzikwa kiheshima.
Sawa, ameshafariki na hana faida tena, lakini maisha yake yalikuwa na maana hapo kabla.
Taifa halijengwi na watu wenye roho mbaya. Halijengwi na watu wasio na hofu. Taifa linajengwa na watu waliostaarabika.
Uwe na asubuhi njema.