Kuona Maiti ikizikwa na Manispaa kumenitafakarisha sana maisha yetu hapa duniani

Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.
Mwananyamala hospital hata kama hukupenda kuweka wazi jina la hospital husika... Je nimepatia?

Kwa bahati mbaya Serikali haina muda wa kufanya utambuzi wa DNA ili walau waondolewe kwenye kundi la waliopotea wasitafutwe zaidi na ndugu zao.
 
Chai
 
Upande wangu mwezi June mwaka huu nilihudhuria mazishi ya ndugu mmoja aliyefariki huko DSM akaletwa kuzikwa huko kwao nilipokuwepo kama mgeni tu. Yule ndugu aliniuma kwakweli maana alizikwa na Serikali ya mtaa imagine.

Ndugu walikuwepo na wachungaji + mashehe ila hawakuhusika katika kumzika kwa sababu ya Kwanza toka akiwa kijana hakua akishiriki ibada ya kanisa wala msikiti japo alikuwa anafahamika kama mkristo.

Iliniuma aiseee yaani hata ile sala au dua ya mwisho hakusaliwa, yaani kama tumefukia mbwa aliyegongwa na gari.
Unataka wamuombee ili afufuke?
 
Mkuu binadam akifa ni sawa tu na maiti ya ngombe bmbuzi ama chochote huo umebaki mwili ila kitu cha thaman ni ile nafsi iliyoacha mwili so sioni shida kabisa hata wangeletwa fisi wakala ili kuepusha kujaza nafasi za kuzika na gharama pia, kuna mataifa mengine mtu akifa anaenda kuwekwa sehem kama jalala kuna ndege wanaitwa vurture hatari na nusu ndani ya robo saa tu utakuta mifupa imebakia
 
Mwananyamala hospital hata kama hukupenda kuweka wazi jina la hospital husika... Je nimepatia?

Kwa bahati mbaya serikali haina muda wa kufanya utambuzi wa DNA ili walau waondolewe kwenye kundi la waliopotea wasitafutwe zaidi na ndugu zao
Haya ndio tukiambiwa tunaishi in a shithole country tuelewe, hata wahanga wa vita wanazikwa kwa heshima na utambulisho wao hasa wa DNA, ndio maana utasikia hizi mass graves zinapogundulika huwa zinafukuliwa na utambuzi unafanyika kwa DNA au dental formula, haya ni matokeo ya uzuzu na watawala wanaendeleza hii kitu ili familia zao zitawale nchi hii kwa muda mrefu
 
Wasalaam!.

Kuna ndugu wa Mfanyakazi mwenzangu alipatwa na maradhi, akalizimika kulazwa ili kuendelea kupata matibabu zaidi katika moja ya Hospital za Rufaa hapa nchini.

Nilikuwa na ratiba ya kwenda kumuona baada ya ibada. Hivyo nilipotoka kanisani nilienda sokoni kununua baadhi ya vitu vya kumpelekea. Wakati nipo katika manunuzi, nikajisemea moyoni acha ninunue na vya ziada ili niwapelekee wakina mama wenye watoto wachanga. Napenda sana kutembelea wodi ya watoto. Nikavibeba na kuondoka kuelekea hospitali.

Kwa kuwa nilishawasiliana na mfanyakazi mwenzangu na kunitaarifu yupo, sikutilia maanani nitafikia wodi ipi nikishafika. Hivyo niliendesha bila wasiwasi wowote.

Mungu ni mwema nilifika salama. Lakini wakati naingia, niliona kitu cha kunistaajabisha na kunisononesha sana. Niliumia sana kiukweli.

Mlango niliongilia ni maarufu kama Mlango wa Mochwary. Na kwa hakika geti lipo karibu kabisa na chumba hicho cha kuhifadhia wapendwa wetu waliotutangulia. Geti la mochwari pia lilikuwa wazi. Kwa sababu gari lisingetoshea kuingia mazima. Hivyo ilinipa nafasi ya kuona barabara kile kilochokuwa kinafanyika.

Miili ya watu takribani mitano ilitolewa na kutupwa ndani ya gari (double cabin) hilo la manispaa. Waliwekwa kwa kupandanishwa. Kwa kweli niliumia sana.

Wakati nastaajabu kinachoendelea, watu hao wanatupiwa kwenye gari hilo kama takataka za muozo. Hawapangwi, wanarusha tu pwaa!.

Nilijisikia vibaya sana. Bahati mbaya nikapigiwa honi ikanilibidi nisogeze gari mbele. Nikasimama na kumruhusu mwenzangu apite.

Nikamuita mlinzi mmoja wa hapo hospitali. Kumuuliza, ndiyo akajibu ni miili ya watu iliyokosa ndugu na jamaa wa kuzika. Hivyo Manispaa inachukua jukumu la kwenda kuwafukia. Maana kule si kuzika.

Kumdadisi kiundani, akanieleza wanaenda kutupwa katika shimo moja lililokwishachimbwa na Caterpillar. Maumivu yake sijapata kuyaona. Nilisismkwa na kukosa raha. Kwa hakika niliumia sana.

Sikuweza tena kukaa ndani ya gari. Nikashuka na kuwafata wahusika. Wanadai ni mali ya manispaa. Wanajaza nafasi, wanapaswa wakaliwe na mbwa. Kwa maana ya kuwa hawafukiwi sana. Ni kidogo tu. Mbwa na paka wanapita kujipatia vitoweo.

Kiukweli nilisononeka kusipo kawaida. Hawana sanda, wamefunikwa tu na shuka la MSD. Nilipoanza kujifikiria maisha yangu ya ulimwenguni, machozi ya Utu uzima yalinitoka.

Nikawaomba walau hata niwanunulie jeneza wawekwe huko wakalazwe. Walikataa kabisa. Lakini baada ya kuwasihi, walikubali. Mungu ni mwema. Nje kidogo ya geti kuna wafanyabiashara wa majeneza. Nikanunua ya kuingizwa ndani. Nikanunua na Sanda, wakaviringishwa na kuwekwa yake. Wakapakiwa na kwenda kupumzishwa. Niliwalipa vijana kwa kazi ya ziada.

Sikuwa na raha siku nzima na hata sasa. Nina mawazo mengi mno. Lile tukio linaogofya na kuumiza sana.

Tuishi maisha ya kumpendeza Mungu. Wapendwa wetu kwa namna yeyote wapumzishwe kwa heshima..

Mungu atusaidie.
Hongera kwa kuwa na Moyo mkuu wa ubinadamu.

Hapo hapo unaweza anzia kwa kuanzisha trust fund ya kusaidia hiyo kazi kwa watu waliofariki na Kukosa ndugu, nadhani kuna wadau wengine wenye moyo wa huruma na utu watachangia Pesa na hiyo taarsisi itasimama.
 
Upande wangu mwezi June mwaka huu nilihudhuria mazishi ya ndugu mmoja aliyefariki huko DSM akaletwa kuzikwa huko kwao nilipokuwepo kama mgeni tu. Yule ndugu aliniuma kwakweli maana alizikwa na Serikali ya mtaa imagine.

Ndugu walikuwepo na wachungaji + mashehe ila hawakuhusika katika kumzika kwa sababu ya Kwanza toka akiwa kijana hakua akishiriki ibada ya kanisa wala msikiti japo alikuwa anafahamika kama mkristo.

Iliniuma aiseee yaani hata ile sala au dua ya mwisho hakusaliwa, yaani kama tumefukia mbwa aliyegongwa na gari.
Potelea mbali hukumu Ni kwa Mungu hao wanayofanya maigizo ili wazikwe kwa sala achana nao.
 
Siwezi sikitika mtu kuzikwa na manispaa, siwezi sikitika mtu kukosa watu wa kumzika. Nasikitika mtu akifa tu, akishakufa mumzike kwa helicopter au toroli bado amekufa.
Mumzike kwenye jeneza au kwenye mkeka, amekufa. Na mazishi mazuri hayampi nafasi ya kwenda mbinguni wala kumuepusha na moto.

Kwangu mimi nikiona mtu anasikitika na kulilia maiti kuzikwa na manispaa huwa namuona weak, na taifa halijengwi na watu wa mioyo dhaifu kama huyo. Mkiwa vitani comrade akafa si lazima mbebe mwili kurudisha nyumbani kama logistics haziruhusu. Yani tuhangaike kubeba majeruhi kutoka frontline kisha tuhangaike kubeba miili ya waliokufa? Kama hakuna ceasefire ya kuchukua deceased mnachukua dogtags na vitambulisho ila miili mnazika ukouko frontline.

Nikienda sehemu kutafuta, sina ndugu wala jamaa nikatangulia ghafla bila yeyote kujua ni sahihi sana nizikwe na manispaa. Hakuna haja ya kutia huruma kwenye hilo
Uko sahihi Ila kwenye mazingira Kama aliyisimulia mtoa mada hakuona Kama Ni sahihi.

Taifa halijengwi na wenye roho za kikatili pekee,chukulia mfano mediators wasingekuwepo ambao Ni sawa na mtoa mada ndio kusema maisha yangekuwa Kama ya wanyama mbabe ndio ata survive na hats huko vitani kupata hiyo ceasefire au kukomesha Vita inakuwa ngumu na unachukua mda mrefu huku watu wakiendelea kuteketea..

Kama watu wenu mnaodai kuwapigania wakiteketea wote Taifa hapo linatoka wapi? Vita huwa Ni njia ya mwisho lakini ikiwa haileti matokea kwa haraka lazima mrudi mezani kwa msingi wa ubinadamu.
 
Back
Top Bottom