Kuongezeka kwa Tumbili na Ngedere hapa Dar hasa Mbezi beach mpaka Ununio

Kuongezeka kwa Tumbili na Ngedere hapa Dar hasa Mbezi beach mpaka Ununio

Hawa ngedere wangeonekana Mbagala, ingekuwa stori nyingine..!!!
Ngedere na tumbili sehemu yao wanapenda kuishi Mbezi Beach sio Mbagala

Binafsi nimeshtuka sana kusikia Mbezi beach wanaishi watu mimi nilikuwa najua ni maeneo ya kuishi tumbili na ngedere

Serikali iwahamishe wakazi wa Mbezi beach iwapeleke Mbagala kutatua hiyo kero
 
Hayo ni mapori yao mmewavamia tu.

Pale Tangi Bovu miaka ya 1980s kati ya 1983 mpaka 1986 palikuwa mashamba na mapori tu.

Bibi yangu alikuwa na shamba pale kwenye Tangi Bovu barabarani, kulikuwa na Tangi limeharibika lina kutu, siku hizi watu wanapaita Tangi Bovu hata hilo Tangi Bovu hawajaliona.
Du, asante sana kwa kipande hiki cha historia. Kumbe ni kwa sababu kulikuwa na tangi bovu!
 
Ni kwamba tumbili na ngedere ndio wameongezeka au watu ndio wameongezeka hivyo kumaliza sehemu zao waliokuwa wanajipatia basic needs hivyo wanavinjari kutafuta wao mkate wa kila siku...
Mbezi beach binadamu hawana uzazi wanazaa kama kanga yai moja tofauti na maeneo kama Mbagala

Waweza zurura Mbezi beach yote ukakutana na watoto wawili.

Ngedere na tumbili wamewazidi uzazi wakazi wa Mbezi beach
 
Kwa upendo nilionao kwa binadamu wenzangu wakaao Mbezi beach niko tayari kuunga juhudi za serikali kutatua huo mgogoro kati ya binadamu na tumbili na ngedere kwa kutoa lori langu la Fuso kuwahamisha wakazi wa Mbezi beach bure kuwahamishia Mbagala ambako hakuna hiyo kero ili ngedere na tumbili waishi kwa amani na utulivu Mbezi beach na wakazi wa Mbezi beach waishi kwa amani na utulivu Mbagala
 
Hili nalo la kuanzishia uzi?? kweli wanaume wa Dar mnasikitisha. Watu tunaishi na nyani wakubwa aka magumbe miaka na miaka. Pale UDSM tumbili wamefugwa kwenye yale mapori zaidi ya miaka 50 sasa na pana wanachuo lukuki na hatujawahi kusikia magonjwa nk nk zaidi ya wale nyani kupenda mademu na kuiba vyepe...

ACHENI KUDEKA!!! ASEEEEH! (Kwa Kinyakyusa)
 
Mamlaka zinazohusika hasa Maliasili. AFYA . Kuna ongezeko kubwa la tumbili na ngedere maeneo ya Mbezibeach Nssf flats kwenye bonde la mto ndumbwi.

Maeneo ya Bahari beach Kondo mpaka Tegeta masaiti. Boko mpaka mbweni ngedere na tumbili wamezaliana sana na kuleta tishio la magonjwa na usalama wa binadamu hasa wanawake.

Wahusika wachukue hatua za haraka
Waache tu, kama 'chawa wa mama' wameongezeka, iweje wao wasiongezeke?
 
Mamlaka zinazohusika hasa Maliasili. AFYA . Kuna ongezeko kubwa la tumbili na ngedere maeneo ya Mbezibeach Nssf flats kwenye bonde la mto ndumbwi.

Maeneo ya Bahari beach Kondo mpaka Tegeta masaiti. Boko mpaka mbweni ngedere na tumbili wamezaliana sana na kuleta tishio la magonjwa na usalama wa binadamu hasa wanawake.

Wahusika wachukue hatua za haraka
Hao ngedere na nyani ni raia huru.
Hao wanyama wana muwakilishi wao, Tumbili, YUUPO!( In Makongoro voice)
 
Mamlaka zinazohusika hasa Maliasili. AFYA . Kuna ongezeko kubwa la tumbili na ngedere maeneo ya Mbezibeach Nssf flats kwenye bonde la mto ndumbwi.

Maeneo ya Bahari beach Kondo mpaka Tegeta masaiti. Boko mpaka mbweni ngedere na tumbili wamezaliana sana na kuleta tishio la magonjwa na usalama wa binadamu hasa wanawake.

Wahusika wachukue hatua za haraka
Maeneo yao hayo,nyi mmetoka kwenu kilimanjaro,mbeya mmewafuata, wapo kimara pori la jeshi mpaka mitaa ya UD
 
Mbezi beach binadamu hawana uzazi wanazaa kama kanga yai moja tofauti na maeneo kama Mbagala

Waweza zurura Mbezi beach yote ukakutana na watoto wawili.

Ngedere na tumbili wamewazidi uzazi wakazi wa Mbezi beach
Kabla kote huko yalikuwa ni makazi yao sasa unavyowafukuza kwa kujenga huko na kule wanatafuta sehemu ambayo angalau ni kimya...

In short kwa Macho wa species wengine Binadamu ni Kirusi kibaya sana yaani ni zaidi ya Ukimwi, wanasema bora binadamu angekuwa hayupo mambo yangekuwa bora zaidi..


View: https://youtu.be/fPQ7SpdVDpE?si=xYpOp_6lfL7JPI3I
 
Back
Top Bottom