Kuongezeka kwa Tumbili na Ngedere hapa Dar hasa Mbezi beach mpaka Ununio

Wapandikize wahadzabe week ni nyingi sana mkuu, hutaona hata mmoja.
 
ni kweli ni makazi yao, kote huko yalikuaga mapoli makubwa tu, sisi binadamu ndio tumewavamia
 
Aliye vamia hayo maeneo ni nani kati ya tumbili na mwanadamu
 
Hao ngedere bila shaka wanatokea Pande Game reserve hapo mitaa ya kati hapo karibia na bunju.

Haya mambo ya kuendekeza hifadhi wasije wakaleta simba hapo.
 

Hiyo haina sababu ya kuwaita maliasili. Turudishe tena wamakonde waliokuwa wanalinda mapori ya Dar. Kama mtawaona tena
 
Ukikaa kizembe hao wanakupelekea moto
 
Kwanini umesema hasa wanawake,kwani hao ngedere wa kiume huwa wanajamiiana na wanawake?
 
Mbezi beach binadamu hawana uzazi wanazaa kama kanga yai moja tofauti na maeneo kama Mbagala

Waweza zurura Mbezi beach yote ukakutana na watoto wawili.

Ngedere na tumbili wamewazidi uzazi wakazi wa Mbezi beach
We jamaa 🀣🀣🀣
 
Mbona kama unatoka nje ya uzi mambo ya bibi yako kuwa na shamba na tank bovu lenye kutu yanaingiaje hapa
 
Umenikumbusha mwishoni wa mwa 80's tulienda picnic bagamoyo "msalabani beach" yani ukitoka tu mbezi beach ni barabara ya vumbi hadi bagamoyo.

Bado na hiyo lami ilikuwa ni mashimo ya kutosha.
 
Ni jambo la kumshukuru mheshimiwa rais daktari profesa Samia Suluhu Hassan kwa ongezeko la chawa , nyani, na tumbili. Ni ishara ya maono ma neema
 
Hao ngedere bila shaka wanatokea Pande Game reserve hapo mitaa ya kati hapo karibia na bunju.

Haya mambo ya kuendekeza hifadhi wasije wakaleta simba hapo.
Mji wa dar umevamiwa tu na binadamu lkn ulikuwa kkoo na posta nje ya hapo ni mapori

Ukipita morogoro road karibu na mbezi stand kuu ya mabasi kwa sasa kuna kituo kinaitwa temboni.

Miaka hiyo ndani kidogo ya kituo hicho kulikuwa na bwawa kubwa sana lkn juu yake lilijaa magugu maji na watu na watu kufanya uvuvi walikuwa wanakata hayo ndio wanafikia maji ( wakati huo wazaramo, wamatumbi na wandengereko wamejaa maeneo hayo) sasa tembo na wanyama wengine walikuwa wakivuka bila tahadhari ila tembo kulingana na uzito wake walikuwa wakizama sana na ndio sababu ya jina hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…