barabara ya korogwe same mwanga moshi inapita ktk jimbo la mwanga ambalo msuya alikuwa mbunge. sasa hebu tueleze huo upendeleo uko wapi wakati tayari barabara inapita jimboni kwake? mimi ninavyoelewa upendeleo ni kiongozi kupeleka huduma fulani eneo lake na kuwanyima wananchi wa maeneo mengine huduma hiyo. kwa mfano kiongozi toka wilaya A alazimishe huduma ipelekwe ktk eneo lake wakati serikali ilikuwa imepanga huduma hiyo iende eneo B.
tukirudi kwa cleopa msuya kuna wakati watu walikuwa wanadai kwamba amechukua ramani ya ujenzi wa jiji la dodoma na kwenda kujenga kwao mwanga. sasa kuna watu wa ccm walitembelea jimbo la mwanga na kukuta hali tofauti na maneno ya mitaani yaliyokuwa yakisemwa kuhusu wapare, wana mwanga, na cleopa msuya. mambo mengi kuhusu msuya siyo ya kweli, bali yametokana na vita ya uongozi ndani ya ccm na serikalini.
mwisho, naomba uache kuchonganisha jamii wa wapare na watanzania wenzao. maendeleo ya upareni yametokana na juhudi za wananchi wenyewe kutokana na utamaduni wa kujitolea kazi wa MSARAGAMBO. kupitia msaragambo wapare wameweza kujenga mashule, kuchimba mifereji ya kilimo cha umwagiliaji, kuchimba barabara za milimani, n.k