Kuhusu majumba, siku hizi yanajengwa kote nchini. Mikoa kama Kagera, Mbeya, Songwe, Manyara, Arusha, Morogoro, Shinyanga, Geita, Mwanza, majumba yanajengwa kote, mijini na kijijini. Swala la kijisifia nyumba bora ingekuwa miaka ya 90.
wachaga wana bahati mbili. bahati ya kwanza ni kahawa. bahati ya pili ni mpaka wa tanzania na kenya. kahawa ni zao ambalo limekuwa na bei nzuri kwa muda mrefu na linastawi zaidi ktk ardhi ya wachaga. kenya ndio jirani wa tanzania mwenye hali nzuri ya kiuchumi kuliko majirani zetu wote. siri ya " mafanikio " ya wachaga ni hiyo nimewapa. sasa mwenye CHUKI zake aendelee tu lakini ukweli ndio huo.
eneo lolote lile lisipokuwa na zao la biashara lenye bei nzuri hata serikali ikiwekeza haliwezi kuinuka. mfano mzuri ni mkoa wa dodoma ambao siku zote una changamoto pamoja na serikali kuwekeza. mikoa ya mbeya na iringa ni mifano ya mikoa ambayo ina mazao ya mpunga na mbao ambayo yana bei nzuri. na ndio maana tumeshuhudia jamii ya wakinga wakiibuka kama wafanyabiashara wakubwa.
wapemba pia wameibuka kutokana na zao la karafuu kustawi ktk ardhi yao. biashara ya karafuu imewawezesha wapemba kuja mjini wakiwa tayari na mtaji wa kuanzisha biashara, tofauti na jamii nyingine ambazo huhamia mjini bila mtaji wa biashara au elimu na maarifa ya kupata ajira nzuri.