kilimanjaro siyo eneo pekee ambalo wamisionari walifika na kuwekeza. kwa hiyo huwezi kusema kwamba kilimanjaro peke yao ndio waliopewa elimu na mkoloni. na popote pale ambapo wamisionari walifika wananchi wa eneo husika walichangia nguvu kazi ktk miradi kama ya elimu, afya, na maji. siyo kweli kwamba wamisionari walikuwa wanafika mahali na kumwaga mapesa na kufungua miradi ya kijamii. wananchi wa maeneo husika walijitolea kujenga makanisa, mashule, etcNi kweli watu wa kaskazini wameanza kupata elimu toka enzi za mkoloni kupitia makanisa. Wamiossionary waliyakimbia maeneo ya uswahili na yaliyokuwa na waislamu wengi. Tunachokiona leo ni multipliers' effect tu.
Toka enzi za mkoloni yalitengwa maeneo ya uzalishaji na yale ya kutoa vibarua. Yapo maeneo walizuiwa kulima mazao ya biashara kabisaa. Ukiacha PLANTATIONS mashamba ya mazao ya biashara ndiyo yaliyokuza uchumi wa wananchi enzi za mkoloni.
Kwa hiyo tukizungumzia ubaguzi upo na ulianzishwa makusudi na wakoloni kisera kabisa. Serikali zetu baada ya uhuru zilipawsa kuchukua hatua za makusudi kuondoa ubaguzi wa kila aina
QUOTA SYSTEM baada ya uhuru. tulipopata uhuru serikali ilibaini kwamba hakuna uwiano mzuri wa wanafunzi wanaojiunga na shule za sekondari. kulikuwa na mikoa ambayo ufaulu wa wanafunzi ulikuwa uko chini, na kulikuwa na mikoa ambayo ufaulu wa wanafunzi ulikuwa juu. hali hiyo ilitokana na sababu za KIHISTORIA siyo kwamba wanafunzi ktk mikoa husika walikuwa hawana uwezo.
kwa kutambua uwepo wa tatizo hilo serikali ikaanzisha mfumo wa QUOTA SYSTEM ili kuweka usawa ktk nafasi za ufaulu kujiunga na masomo ya sekondari. kwa hiyo maeneo ambayo yalikuwa yanafaulisha sana yaliwekewa pass mark kubwa ya mwanafunzi kufikia ili aende sekondari. maeneo ambayo wanafunzi walikuwa wana-struggle waliwekewa pass mark ya chini kidogo ili watoto wapate nafasi.
Mtindo wa quota system uliwezesha watoto wengi toka maeneo ya "pembezoni" kupata nafasi kujiunga na sekondari. lakini quota system pia ilileta changamoto kwa mkoa kama Kilimanjaro na kusababisha wazazi kuanza kuhamisha watoto wao kwenda mikoa mingine kwa ajili ya mitihani ya darasa la saba. Pia quota system ilileta muamko wa kujenga shule za private za sekondari ktk mkoa wa kilimanjaro kwani wazazi waliona watoto wao wanakosa nafasi kwenda shule za sekondari za serikali.
tunapolaumu serikali inabidi tuwe na kiasi. pia tunaposhutumu wenyeji wa kilimanjaro basi walau tuwe na ushahidi wa shutuma tunazotoa.