Kuongezeka kwa ubaguzi wa kiuchumi, kieneo na ukabila nchini Tanzania

Sielewi una maana gani.
1. "Hakuna ubaguzi wowote uliofanywa na serikali ya awamu ya 5"? Ubaguzi au upendeleo wa kieneo kidogo katika kanda nzima? Sijaona kama Mara, Simiyu,Shinyanga na hata Kagera wanatofauti yoyote na mikoa mingine isiyokuwa ya kanda ya ziwa. Hata Geita yenyewe sioni kuwa imefaidika sana; ila Chato ni tofauti.

Katika nafasi za ajira serikalini, sijui; lakini je katika nafasi za uongozi katika taasisi na ngazi za juu serikalini kama mawizara, kuna upendeleo huko?

2. "Wao wanalilia 'dominance""? Wao, akina nani? Dominance ya kitu gani?
Hakuna upendeleo popote nchi hii. Nafasi za ajira serikalini siku husimamiwa na sekretariati ya ajira isipokuwa kwa BoT. Hata taasisi za elimu ya juu hutangaza wenyewe na kufanya interview wenyewe kwa nafasi za taaluma lkn lazima PSRS iwe na wawakilishi hatua zote. Hakuna siasa huko.
 
Kwa nafasi za uteuzi sioni upendeleo popote. Miongozo inaelekeza teuzi kuakisi utaifa. Sioni palipovunjwa hiyo miongozo katika teuzi kuu. Teuzi kuu ni za Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za Umma na Mabalozi.
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo, ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania.

Haya ni mambo ambayo Tanzania hatukuyazoea wala kushuhudia toka enzi za kupata uhuru.

Mwalimu alijishusha mno na hata hakupendelea kwao kwa jinsi tunavyoshuhudia sasa, mimi Butiama nimefika.

Ubaguzi wa aina yoyote una mwisho si mzuri kwa mustakabali wa Taifa.

Chama kimelala.
Bunge ndio kabisa.
Lakini wahenga wanasema tutavuna tunachopanda.
Huu ni wakati wetu raia kutoka Burundi kuifaidi hii nchi.
 
Tunaishi nyakati unazizijua vema.

Na mada umeilewa vema ila una unafiki wa ku act kuwa a wounded guy.

Kisaikolojia umasikini wako unaamua kujihalalishia ubaguzi wako.

Refer kwa Mwalimu, nakupeleka SUNGURATEX Butiama, ingwaje kule wanalima pamba.

Hata barabara kwenda Butiama zilijengwa baada ya yeye kufariki.

Buhemba pale kuna dhahabu, lakini Mwalimu hakuweka umimi mbele.

Tunayoyaona yanashangaza.
Magu atawashangaza , atawashangaza mpaka umauti.
 
Mazao mengine yote yaathiriwe na ujamaa lakn kahawa haikuathirika? Kwanini?
Sababu pekee ambayo ingeweza kunishawishi mkoa wa Kilimanjaro kuwa mbele kuliko mikoa mingine ni tabia yao ya kurudi nyumbani, kujenga nyumbani, yaani kutolowea huko anakoenda kutafuta maisha. Tabia ambayo makabila mengine ya kaskazini mwa Tanzania tumeiga/tunaiga.
Huwezi kusema wachagga ni wasomi kuliko wahaya au wakerewe au wanyakyusa. Au ukasema wachagga wana hela saana kuliko wakinga. Tofauti ni hiyo tu ya kupenda kwao. Makabila yote yakipenda kwao, vijiji vya Tanzania kote vitapendeza.
mazao mengi yaliathiriwa kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya ushirika. lakini huwezi kusema kwamba athari hizo zilikuwa za kiwango sawa kila mahali. na pia ni lazima uangalie wananchi / wakulima wa zao husika walikuwa na alternative zipi za kuuza mazao yao baada ya vyama vya ushirika kuvunjwa na kuundwa kwa mamlaka za mazao.

nakubaliana na wewe 100% kwamba utamaduni wa kurudi nyumbani umewasaidia watu wa kaskazini kuliko maeneo mengine. pia muamko wa kufuatilia na kuchangia miradi ya maendeleo haswa kwa wasomi wa kaskazini naamini una mchango mkubwa ktk maendeleo ya ukanda huo. lingine ni mwamko wa wapiga kura wa ukanda wa kaskazini ambako siyo rahisi kukuta mbunge anashinda kwa kishindo, au anaongoza kwa vipindi vingi. hali ya wapiga kura kuwa na mwamko inawafanya wabunge wawe makini na wasibweteke wakati wote.
 
Umeongeza sifa ambazo sio za kweli. Majimbo 2 ya Same hawarudii? Mwanga hawarudii? Magembe amekuwa mbunge Mwanga mara ngapi? Mbowe amekuwa mbunge Hai mara ngapi? Au The late Ndesamburo je? Kina Mramba kabla ya kustaafu? Hata kina Komu, Mbatia, Jafari wangeendelea kuwa wabunge ila ninkwa sababunya nature ya uchaguzi wa 2020.
Majimbo magumu nchi hii yanajulikana; Nyamagana, Tarime, Arusha mjini, Mbeya mjini.
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo, ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania.

Haya ni mambo ambayo Tanzania hatukuyazoea wala kushuhudia toka enzi za kupata uhuru.

Mwalimu alijishusha mno na hata hakupendelea kwao kwa jinsi tunavyoshuhudia sasa, mimi Butiama nimefika.

Ubaguzi wa aina yoyote una mwisho si mzuri kwa mustakabali wa Taifa.

Chama kimelala.
Bunge ndio kabisa.
Lakini wahenga wanasema tutavuna tunachopanda.
Ninauliza tu muda ule wa Tigray walijazana TRA kisa wamesoma ivi uliliona hilo suala ama ni kwa vile walikuwa wamesoma wao tu.
Acheni wachunga nao wale keki bana mbona kama unaumia. Enzi hizo maendeleo mpaka umeme wafungwa mgombani. Na watakutawala subiria na katiba inabadilishwa ni mwendo wa kimu7 kama vipi hama nchi bana.
Na tunahamisha mlima na mbuga zote Kwenda chato.

Sema akili yako imekaa kuangalia ukabila ndo mana unayaona haya kitu kidogo . you're already addicted with tribalism
 
Umeongeza sifa ambazo sio za kweli. Majimbo 2 ya Same hawarudii? Mwanga hawarudii? Magembe amekuwa mbunge Mwanga mara ngapi? Mbowe amekuwa mbunge Hai mara ngapi? Au The late Ndesamburo je? Kina Mramba kabla ya kustaafu? Hata kina Komu, Mbatia, Jafari wangeendelea kuwa wabunge ila ninkwa sababunya nature ya uchaguzi wa 2020.
Majimbo magumu nchi hii yanajulikana; Nyamagana, Tarime, Arusha mjini, Mbeya mjini.
nimesema wabunge huwa hawashindi kwa kishindo. pia hawadumu muda mrefu ktk nafasi zao. kwa kumbukumbu zangu Mbowe aliwahi kugombea na kushindwa. Mramba aliwahi kushindwa kule Rombo. Jimbo la Mbatia limebadilisha wabunge mara kadhaa. Same Mashariki walimtosa Daniel Yona ktk kura za maoni bila kujali kuwa ni waziri.

Hata hivyo nakubaliana na wewe kwamba majimbo ya Nyamagana/Mwanza mjini, Tarime, Arusha mjini, na Mbeya mjini, yana ushindani mkali kuliko majimbo ya mkoa wa Kilimanjaro.
 
Tusiposema sasa mawe yatasema.

Sasa hivi nchi inapitia ubaguzi wa wazi kieneo, ukabila na upendeleo wa wazi kwa sehemu fulani fulani nchini Tanzania.

Haya ni mambo ambayo Tanzania hatukuyazoea wala kushuhudia toka enzi za kupata uhuru.

Mwalimu alijishusha mno na hata hakupendelea kwao kwa jinsi tunavyoshuhudia sasa, mimi Butiama nimefika.

Ubaguzi wa aina yoyote una mwisho si mzuri kwa mustakabali wa Taifa.

Chama kimelala.
Bunge ndio kabisa.
Lakini wahenga wanasema tutavuna tunachopanda.
Ubaguzi ulikuwepo na upo ila tu watu huwa wanaamua kukaa kimya . Mfano mmoja mdogo tu, pale Moshi huwezi kupata frem ya biashara inayomilikiwa na Mchaga kama wewe si Mchaga. Je huo si ubaguzi wa kikabila? Bahati mbaya sana hao wabaguzi wa siku zote ndo wanaopiga kelele leo kwamba wanabaguliwa baada ya nchi kuwa mikononi mwa Mzalendo namba moja aliyeamua kusambaza keki ya nchi ktk maeneo mengi ya nchi
 
Hakuna ubaguzi wowote uliofanywa na serikali ya awamu ya 5. Wao wanalilia dominance.
Unaposema "Hakuna ubaguzi wowote uliofanywa na serikali ya awamu ya 5" nawe unajiingiza kwenye mambo hayo hayo ya "wao wanalilia dominance".

Huwezi kuwa mkweli kwa kujifanya huoni upendeleo na uonevu unaofanyika. Unapopendelea sehemu moja, unatafuta 'dominance' ya sehemu hiyo.
 
Kwa nafasi za uteuzi sioni upendeleo popote. Miongozo inaelekeza teuzi kuakisi utaifa. Sioni palipovunjwa hiyo miongozo katika teuzi kuu. Teuzi kuu ni za Baraza la Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa taasisi za Umma na Mabalozi.
Wewe unaona hivyo kwa sababu zako.
Sikiliza na wengine wanaona na kusema nini.
 
Lakini kwa nini mapato ya kutoka mikoa yote yanapopatikana yapelekwe kanda ya ziwa? Je Unadhani hapo tunagawana vyema kweli keki ya nchi ? Issue syo wami wala mtwara wala dsm walau kila litokanalo na eneo husika lingetumika kuboresha sehem husika ndo mana umaskin hauishi tunajenga mavitu ya kufurahisha lakin ukiangalia kwa kiasi kikubwa hayasaidii,Najua kama una mdogo wako hajaajiriwa wewe hujaongezwa mshahara alafu unafurahia upanuzi wa uwanja mkubwa chatle ilihal kuna uwanja wa mwanza

Tatizo hata kama ww ni mzazi usioneshe kumpendelea sana Mwanao mmoja kuliko wengine utaharibu.
Ni kwa sababu wakati KIA na DIA zinajengwa hatujui mikoa mingapi ilifunga mikanda ili viwanja hivyo vijengwe.
Ikumbukwe kuwa maendeleo hayavutii miundombinu mizuri,bali miundo mbinu mizuri inavutia maendeleo
 
Mbuga ya wanyama ya burigi chato ni ya muda mrefu,haipati watalii sababu ya miundo mbinu mibovu,
sasa kwa kuwa upele umepata mkunaji,miaka ijayo utashuhudia maendeleo kwa macho yako,kama sio wewe basi uzao wetu
utayashuhudia. Kuna watoto wengi wamesomea tour guide lakini macho yetu yanaangalia mbuga chache za tangu enzi za mkoloni ili kuwaajiri.
Kuongezeka kwa mbuga za burigi chato ni fursa kwa wasomi wa utalii,pia maeneo mapya ya uwekezaji kwa kujenga hotels
sehemu ambazo unapata viwanja kwa bei rahisi na hivi vyote ni vichocheo vya kukua kwa uchumi.

Angalia DSM ilivyokuwa imeghubikwa na kero ya foleni za magari,linganisha na sasa hivi baada ya ikulu kuhamia dodoma
Kwa jicho la karibu utadhani serikali imekosea kuhamia dodoma,lkn kwa jicho la kuona mbali ni kwamba
unapotawanya miundo mbinu na maendeleo yanafuata huko huko,na hivyo utajikuta mazoea ya kurundikana sehemu moja
na kuwa kero mnatowanyika mnapata maendeleo bila kero.
 
sioni ubaguzi hapa zaidi ya wivu
ni haki kila mtanzania apate mgao wa keki ya taifa sa we kama ulkula kipande chako usiwaonee wivu wanaokula sasaivi
 
Ubaguzi ulikuwepo na upo ila tu watu huwa wanaamua kukaa kimya . Mfano mmoja mdogo tu, pale Moshi huwezi kupata frem ya biashara inayomilikiwa na Mchaga kama wewe si Mchaga. Je huo si ubaguzi wa kikabila? Bahati mbaya sana hao wabaguzi wa siku zote ndo wanaopiga kelele leo kwamba wanabaguliwa baada ya nchi kuwa mikononi mwa Mzalendo namba moja aliyeamua kusambaza keki ya nchi ktk maeneo mengi ya nchi
Majamaa ni wabaguzi sana. Lakini kimsingi wanajibagua. Haiwezekani katikati ya watu wengi, wao wanajibagua kwamba ni bora kuliko wengine, eti mchagga anunue bidhaa za mchagga tu, asiende duka linalomikikiwa na kabila lingine au kabila lingine lisipate ajira hata kama amempita mchagga kwenye interview.
Hivi makabila mengine yangeamua kutonunua bidhaa na huduma hizo hela wanzosema wanazo wangepata wapi?
Au hata sasa wakiamua kununua kwenye maduka yao watafanya biashara kweli? Mtaweza kuungishana ninyi kwa ninyi tu bila kutegemea makabila mnayoyaita washamba, wajinga na maskini?
 
Halafu eti yanataka yatoe Rais wa nchi. Nani akubali kwa mijitu mibaguzi kama hii.
 
Ubaguzi ulikuwepo na upo ila tu watu huwa wanaamua kukaa kimya . Mfano mmoja mdogo tu, pale Moshi huwezi kupata frem ya biashara inayomilikiwa na Mchaga kama wewe si Mchaga. Je huo si ubaguzi wa kikabila? Bahati mbaya sana hao wabaguzi wa siku zote ndo wanaopiga kelele leo kwamba wanabaguliwa baada ya nchi kuwa mikononi mwa Mzalendo namba moja aliyeamua kusambaza keki ya nchi ktk maeneo mengi ya nchi
huu ni UONGO mwingine unaotumika kuhalalisha CHUKI. kwa Tanzania ninayoijua mimi hakuna kabila wameoleana na makabila mengine kushinda ndugu zetu Wachagga. Pia hapo Moshi mjini wameshachagua MEYA na MBUNGE ambaye siyo Mchagga. sasa utahukumu vipi jamii nzima kuwa ina ubaguzi? Yaani mtu akunyime fremu ya duka lakini awe radhi kukuoza binti yake, au kijana wake aoe binti yako?
 
Hatuongelei makabila tunaongelea uongozi na attitude ya viongozi na mustakabali wa nchi yetu huko baadaye!!
 
Back
Top Bottom