Ni kwa sababu wakati KIA na DIA zinajengwa hatujui mikoa mingapi ilifunga mikanda ili viwanja hivyo vijengwe.
Ikumbukwe kuwa maendeleo hayavutii miundombinu mizuri,bali miundo mbinu mizuri inavutia maendeleo
Mbuga ya wanyama ya burigi chato ni ya muda mrefu,haipati watalii sababu ya miundo mbinu mibovu,
sasa kwa kuwa upele umepata mkunaji,miaka ijayo utashuhudia maendeleo kwa macho yako,kama sio wewe basi uzao wetu
utayashuhudia. Kuna watoto wengi wamesomea tour guide lakini macho yetu yanaangalia mbuga chache za tangu enzi za mkoloni ili kuwaajiri.
Kuongezeka kwa mbuga za burigi chato ni fursa kwa wasomi wa utalii,pia maeneo mapya ya uwekezaji kwa kujenga hotels
sehemu ambazo unapata viwanja kwa bei rahisi na hivi vyote ni vichocheo vya kukua kwa uchumi.
Angalia DSM ilivyokuwa imeghubikwa na kero ya foleni za magari,linganisha na sasa hivi baada ya ikulu kuhamia dodoma
Kwa jicho la karibu utadhani serikali imekosea kuhamia dodoma,lkn kwa jicho la kuona mbali ni kwamba
unapotawanya miundo mbinu na maendeleo yanafuata huko huko,na hivyo utajikuta mazoea ya kurundikana sehemu moja
na kuwa kero mnatowanyika mnapata maendeleo bila kero.