Kuota naokota hela, hii ndoto ina maana gani?

Kuota naokota hela, hii ndoto ina maana gani?

Kwanza kujirudia mara mbili ni kwamba iyo ndoto inatoka kwa Mungu na anakwambia/anakuhakikishia kwamba hakika itakuwa.

Maji: Inamaanisha watu au nchi
Pesa; inamaanisha Heshima, utawala au utatuzi
Kwenye benchi: Penye watu
Kanisani: Amani au Utulivu

Kwahiyo: Siku zijazo utapata uongozi au heri fulani ya maisha, utaipata katikati ya ya watu bila kuitolea jasho either kwa kupendelewa au kuirithi, hii heri itakuwa kwenye eneo lisilochangamana na wengine, bahati mbaya uzinzi utakuponza maana utaitapanya iyo heri kwa njia ya sirini(kitanda). Mwombe Mungu akujalie kutubu ukianguka uweze kuinuka tena maana itakuwa bado kuna azina yako uliacha kule kisimani japo haitokuwa kubwa Kama ile ya kwanza.
Kwa tafsiri hii kuna kitu nimeelewa, ahsante.
 
Ukame zaidi ya nilionao 😁😁 ukame utapita na roho yangu sasa
Njozi za kuokota sio nzuri...
Pili ukaokota na kanisani...je huwa unavusha au kula fungu la kumi?

Kwani umeokota kanisani pia.

Kama ndio basi umepewa ujumbe wa kurekebisha mambo
 
Nilijifunza kutokupuuzia ndoto nnazoota huwa najitahidi kufatilia na kuulizia maana yake, kwani nimekua naota mambo halafu yanatokea kweli yanatokea vile vile nnavoona kwenye ndoto, hadi najihisi unabii unaninyemelea.

Wiki kama mbili hivi zilizopita niliota nimepita njiani kuna kisima kimejaa maji, ndani ya kisima kuna vibunda vya noti za elf kumi kumi vinaelea juu ya maji basi nikaziokota nyingiii niakaacha kama viwili tu, nikaingia ndani nikawa nazisambaza kitandani ili zikauke.

Usiku wa leo nimeota nimeenda kanisani kwenye bench nilipokaa nikakuta kuna hela nyingi elf kumi kumi, nikafanya kilichonipeleka kisha nikabeba zile hela sijui nimeiba au nimeokota ila niliondoka nazo.

Wataalamu wa haya mambo, hizi ndoto za hela maana yake ni nini???
Mshana Jr BIN NUN na wengine mnaojua.
Hii ndoto inaashiria utapata danga jipya
 
Majibu umepata ...huyo jamaa amekujibu vuema na majibu yake ni sawa na niliyokupa.

Nimekuuliza swali kuhusu zaka uka mute.

Ungejibu ningeendelea
Kwakweli fungu la kumi sijawahi kutoa, endelea mtumishi nasubiria
 
Back
Top Bottom