Habarini Wadau,
Ninaomba kuuliza lakini pia kupatiwa msaada katika jambo hili.
Mwaka Jana mwezi wa 5, watumishi wengi wenye sifa walipandishwa madaraja. Lakini cha kushangaza katika mabadiliko ya mishahara ni kama kuna UBAGUZI kwa watumishi.
Kwa Mkoa wa Kilimanjaro kuna ambao wamebadilishiwa mishahara na wengine wenye barua kabisa za kupanda daraja mishahara yao haijabadilika.
Mimi nina miaka 7 tangu kuajiriwa,huu ni wa 8. Nilipoajiriwa baada ya miaka miwili nikapata ruhusa rasmi ya kwenda masomoni, nikarudi kazini tangu 2017 na kufanya kazi kwa miaka miwili na huu wa 2020 ni wa tatu.
Nimepata barua ya kupandishwa daraja mwaka Jana lakini leo Afisa Utumishi wilaya ananiambia kuwa sina sifa ya kubadilishiwa mshahara hata kama barua imekuja.
SABABU: Afisa Utumishi anasema kuwa kuna Mwongozo umekuja ambao hautambui ule muda wa mtumishi kuwa masomoni kuwa upo ndani ya Utumishi hata kama alienda kwa barua rasmi bila kutoroka.
SWALI: NI KWELI HUO MWONGOZO UPO? JE NI RASMI ?
Au upo kwa Mkoa wa Kilimanjaro tu?
Naombeni Msaada wenu.
Sent using
Jamii Forums mobile app