Pesa haipaswi kukaa mfukoni mwa mtu asiyejielewa. Labda ipitie tu kwake na kwenda kwa anayejielewa.
Si kwamba watumishi wote ni mifuko, bali asilimia kubwa ni mifuko, hawajielewi. Na hawa mifuko ndiyo wanaowaponza wenzao.
Kiongozi anapowaangalia hawa mifukoni anapata picha ya kundi zima. Inapelekea kiongozi kuamua lolote juu ya watumishi wa umma bila woga.
- Watumishi wa idara mbalimbali walilipwa Tsh. 20000 ili wakafanye maandamano ya amani kumsifia mtu aliyerudisha kikokotoo cha zamani. Ijulikane kuwa si kikokotoo kipya wala cha zamani kinachoweza kumpa mtumishi wa umma maisha bora.
Waliweza kusahau maumivu yao ya kutoongezewa mishahara na kutokupanda madaraja kwa miaka karibu 4 wakaingia road kwa shinikizo la wanasiasa wachache kwa malipo ya fedha ambayo nikimpa mwanangu wa la kwanza Jumamosi asubuhi mapema siku anayoshinda nyumbani mpaka saa 12 mfukoni anabakiwa na buku tu (Not real).
- Mpaka leo sijapata habari ya mtumishi aliyekwenda ofisi za TUCTA au CW, TALGWU, TUGHE, TUICO kutaka ajiondoe uanachama kwakuwa anakatwa pesa ambayo hajui fedha yake inafanya nini.
Kila leo mtu anajinasibu nchi ina fedha za kutosha ila ukimgusia kuhusu maslahi ya watumishi wanaambiwa wasubiri miradi ikamilike ndipo watafikiriwa na hupiga makofi wakishangilia.
Kama watumishi wenyewe ndiyo hawa, ni bora wasubiri miradi mikubwa ikamilike ndipo walete kelele zao.