Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Hakuna namna, Watumishi wa umma hasa wa Zile taasisi zilizochoka ambazo wanategemea mishahara tu na posho kidogo tena mpaka pale wakurugenzi au watendaji wao wakuu watakapokuwa na furaha kama Ualimu, Halmashauri,GPSA, LITA, RITA,BAKITA,TMA, Ofisi za wakuu wa wilaya, TTRI,Temesa,Mamlaka za Mabonde, MAHAKAMA, na nyingine mtaziongezea WENYEWE watumishi wake wanaenda kupata shida sana na HAPA na-imagine jinsi makunyanzi yanavyoenda kuwatoka na kuongezeka usoni hasa kwa wale wakazi wa Dar kwa WALE walioko mkoani kipindi cha mzee huyu msiombe uhamisho wa mjini ni fursa kwenu kuwepo huko mlime na mfuge huku mjini wenzenu wanalia.

Huyu mzee wenu hata ongeza mishahara hakuwa na nia hiyo na corona imempa sababu maana ndio kitakuwa kisingizo na kwa uzoefu wangu wafanyakazi wa hizi ofisi na zinginezo zinazofanana na hizi wanatia huruma sana maana mshahara tu wa mtu mwenye degree haumfikii hata nusu wa mlinzi au msaidizi wa ofisi wa BOT, TPDC,msd,TCRA,Nhif ama TPA Aliye na cheti cha form four tu na wengi wao hawana Allowance zozote .... poleni sana ndugu zangu

Tasisi ambazo wafanyakazi wake hawataathirika hata kama namba one asipoongeza mishahara kwa kipindi chote atakachokuwa madarakani na ambao wataendelea kula bata hata iweje ni, TCRA, TPDC,NSSF,WCF,PSSSF,Majeshi yote kasoro magereza, TAKUKURU,NHIF,KADCO,TANROAD,TANESCO,TIC,TRA, NGORONGORO, TANAPA,TBS, BOT,NEC,TASAC,LATRA,TPA,EWURA,NAO,MSD,madini,... na nyingine mtaongezea watumishi wa taasisi hizi hata kama mzee asipoongeza hawa hawana shida, kuna baadhi ya taasisi wana Allowance nyingi kiasi kwamba kila wiki pesa inaingia kwenye account ya mtumishi

Cheza mbali na taasisi za mwanzo nilizozitaja, watumishi wa hizo taasisi hakuna rangi wataacha kuiona hii miaka ya utawala wa namba one na mbaya Zaidi viongozi wa hizo taasisi wengi wao wana roho mbaya wapo kwa ajili ya kujilipa miposho na allowance nyingi kwao wao tu, na ni watu wa kupenda umbeya sana kutoka kwa watumishi ambao wamewafanya baadhi yao wajipendekeze kwao ili wapate angalau visafari na semina.

Hali ni tofauti kwenye taasisi zinazolipa vizuri, viongozi wao mara nyingi hawajali umbeya, wao wanaangalia professionalism na uchapa kazi na wanawajali sana wafanyakazi wao, nimeshuhudia mara nyingi inapotokea mfanyakazi akapata matatizo ambayo yakamfanya awe na msongo wa mawazo na viongozi wakafahamu watafanya kila namna ili kumrudisha na kumsaidia mfanyakazi wao awe katika hali ya kawaida...ukiwa mmoja wa watumishi katika taasisi hizi nakupa hongera SANA, lakini kama uko kundi la kwanza Aisee pole sana lazma upambane na utindio wa ubongo katika kipindi hiki.

NA VIJANA mnaosubiri kuajiriwa tulieni kwanza...msubiri 2026 Tutajenga uchumi kwanza baada ya Corona
Mbona nina mwanangu mmoja yupo KADCO analamika njaa.
 
Kwakweli hali ni mbaya,huyu mjomba sijui hajui kama watu wanateseka na ugumu wa maisha?
Kuna walimu walianza kazi mwaka 2014,hawa walimu wapo kazini miaka mitano (5) sasa,lakini hajawai kuwaongezea hata nyongeza ya mshahara ,mbaya zaidi walisomeshwa na boards ya mikopo akawalazimishwa wawe wanalipa 100,000 kila mwezi mwalimu wa degree ana katwa inarud serikalini.

Jamani awamu hii watu wanateseka sana,sema kuna watu wanautetea sana utawala huu kuwa ni mzuri,nahisi hao watu wanafaidika na mfumo au wako ndani ya system ya awamu ya tano lakini kwa mwananchi wa kawaida tu tunateseka sana,malengo hayatimii kabisa yaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona nina mwanangu mmoja yupo KADCO analamika njaa.
hebu ulizia wanaofanya taasisi nilizitaja mwanzo na malipo unaweza kuta huyo jamaa anawalipa mishahara ya miezi miwili kwa mshahara wake wa mwezi mmoja kwa mtu waliye na level sawa za mishahara
 
mkuu hawa watumishi wanahitaji faraja kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote
 
hebu ulizia wanaofanya taasisi nilizitaja mwanzo na malipo unaweza kuta huyo jamaa anawalipa mishahara ya miezi miwili kwa mshahara wake wa mwezi mmoja kwa mtu waliye na level sawa za mishahara
Mwana aliniambia take home ipo around 900,sasa sijui kanipiga kamba.
 
Bila kufanya kilimo,.biashara na ufugaji..mtumishi kutoka kimaisha Ni ndoto za alinacha..mi nlishasahau kuhusu nyongeza ya mshahara

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu tatizo ni mitaji,unaweza kukopa mara moja ukaweka ela kwenye biashara alafu biashara yenyewe isiimarike,au wengine walishakopa tangu awali sasa kukopa tena inakuwa haiwezekani,labda jamaa angeongeza mishahara hapo unaweza kukopa,lakini wapi.Take home imebaki laki 2 sasa hapo utakopa nini tena?[emoji3166][emoji3166]

kuna baadhi ya ofisi zinatambua hili so zinawafavour wafanyakazi wao kwa Allowance ili wasiwe na misongo ya mawazo.
na taasisi nyingi zinazofanya na zile zinazolipa vizuri
 
kuna baadhi ya ofisi zinatambua hili so zinawafavour wafanyakazi wao kwa Allowance ili wasiwe na misongo ya mawazo.
na taasisi nyingi zinazofanya na zile zinazolipa vizuri
Hizo kazi za maana na taasisi kubwa hizo wanaofanya kazi ni watoto wao,sisi watoto wa wakulima kazi zetu hizi hizi za ualimu,udakaktari na unesi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom