Hakuna namna, Watumishi wa umma hasa wa Zile taasisi zilizochoka ambazo wanategemea mishahara tu na posho kidogo tena mpaka pale wakurugenzi au watendaji wao wakuu watakapokuwa na furaha kama Ualimu, Halmashauri,GPSA, LITA, RITA,BAKITA,TMA, Ofisi za wakuu wa wilaya, TTRI,Temesa,Mamlaka za Mabonde, MAHAKAMA, na nyingine mtaziongezea WENYEWE watumishi wake wanaenda kupata shida sana na HAPA na-imagine jinsi makunyanzi yanavyoenda kuwatoka na kuongezeka usoni hasa kwa wale wakazi wa Dar kwa WALE walioko mkoani kipindi cha mzee huyu msiombe uhamisho wa mjini ni fursa kwenu kuwepo huko mlime na mfuge huku mjini wenzenu wanalia.
Huyu mzee wenu hata ongeza mishahara hakuwa na nia hiyo na corona imempa sababu maana ndio kitakuwa kisingizo na kwa uzoefu wangu wafanyakazi wa hizi ofisi na zinginezo zinazofanana na hizi wanatia huruma sana maana mshahara tu wa mtu mwenye degree haumfikii hata nusu wa mlinzi au msaidizi wa ofisi wa BOT, TPDC,msd,TCRA,Nhif ama TPA Aliye na cheti cha form four tu na wengi wao hawana Allowance zozote .... poleni sana ndugu zangu
Tasisi ambazo wafanyakazi wake hawataathirika hata kama namba one asipoongeza mishahara kwa kipindi chote atakachokuwa madarakani na ambao wataendelea kula bata hata iweje ni, TCRA, TPDC,TANAPA,NSSF,WCF,PSSSF,Majeshi yote kasoro magereza, TAKUKURU,NHIF,KADCO,TANROAD,TANESCO,TIC,TRA, NGORONGORO, TANAPA,TBS, BOT,NEC,TASAC,LATRA,TPA,EWURA,NAO,MSD,madini,TMDA... na nyingine mtaongezea watumishi wa taasisi hizi hata kama mzee asipoongeza hawa hawana shida, kuna baadhi ya taasisi wana Allowance nyingi kiasi kwamba kila wiki pesa inaingia kwenye account ya mtumishi
Cheza mbali na taasisi za mwanzo nilizozitaja, watumishi wa hizo taasisi hakuna rangi wataacha kuiona hii miaka ya utawala wa namba one na mbaya Zaidi viongozi wa hizo taasisi wengi wao wana roho mbaya wapo kwa ajili ya kujilipa miposho na allowance nyingi kwao wao tu, na ni watu wa kupenda umbeya sana kutoka kwa watumishi ambao wamewafanya baadhi yao wajipendekeze kwao ili wapate angalau visafari na semina.
Hali ni tofauti kwenye taasisi zinazolipa vizuri, viongozi wao mara nyingi hawajali umbeya, wao wanaangalia professionalism na uchapa kazi na wanawajali sana wafanyakazi wao, nimeshuhudia mara nyingi inapotokea mfanyakazi akapata matatizo ambayo yakamfanya awe na msongo wa mawazo na viongozi wakafahamu watafanya kila namna ili kumrudisha na kumsaidia mfanyakazi wao awe katika hali ya kawaida...ukiwa mmoja wa watumishi katika taasisi hizi nakupa hongera SANA, lakini kama uko kundi la kwanza Aisee pole sana lazma upambane na utindio wa ubongo katika kipindi hiki.
NA VIJANA mnaosubiri kuajiriwa tulieni kwanza...msubiri 2026 Tutajenga uchumi kwanza baada ya Corona