Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Na watumishi wanaoongoza kwa uzezeta huu (Mungu anisamehe) ni WALIMU.

Nikikumbuka walivyokuwa wananicharaza bakora kuufuta ujinga kwenye bongo yangu. Sikujua kumbe bongo zao ndo zinahitaji kufutwa ujinga zaidi.
Nilikua nasikia tu kuna watu wanaitwa wanaume suruali. Leo nimehakikisha kwamba wapo na kiongozi wao ni wewe. Hata Musiba anaufahamu wa mambo kuliko wewe.
 
hakuna kipindi ambacho napiga pesa ofisini kama hiki
 
Nilikua nasikia tu kuna watu wanaitwa wanaume suruali. Leo nimehakikisha kwamba wapo na kiongozi wao ni wewe. Hata Musiba anaufahamu wa mambo kuliko wewe.
Leo nitawajua kwa upana zaidi walimu vilaza...

Karibu sana mwalimu wa historia.
 
Katika awamu ya tano ya Raisi Magufuli ambayo inamaliza muda wake mwaka huu, BAJETI YA MISHAHARA (Trilion) ilikuwa kama ifuatavyo:
(2015/16 -JK) Trilion 6.5 -Mara ya mwisho kuongeza mshahara

1. 2016/17 = Trilion 6.6
2. 2017/18 = Trilion 7.21
3. 2018/19 = Trilion 7.41
4. 2019/20 = Trilion 7.56
5. 2020/21 = Trilion 7.76
Screenshot_20200312-073901.png


Pamoja na hivyo vibilioni kadhaa vinavyoongezeka;
-bado mishahara haiongezeki,
-ajira hakuna (zilizotolewa bado idadi haijafikia ya waliotumbuliwa kwa vyeti feki)
-kupandishwa vyeo hakuna
-kupanda madaraja ni kwa kusuasua

Watumishi wa umma na uongozi wenu wa TUCTA, mmeridhika?
 
Hakuna namna, Watumishi wa umma hasa wa Zile taasisi zilizochoka ambazo wanategemea mishahara tu na posho kidogo tena mpaka pale wakurugenzi au watendaji wao wakuu watakapokuwa na furaha kama Ualimu, Halmashauri, GPSA, LITA, RITA,BAKITA,TMA, Ofisi za wakuu wa wilaya, SIDO,Bodi ya korosho, TTRI, Temesa, Mamlaka za Mabonde, MAHAKAMA, na nyingine mtaziongezea WENYEWE watumishi wake wanaenda kupata shida sana na HAPA na-imagine jinsi makunyanzi yanavyoenda kuwatoka na kuongezeka usoni hasa kwa wale wakazi wa Dar kwa WALE walioko mkoani kipindi cha mzee huyu msiombe uhamisho wa mjini ni fursa kwenu kuwepo huko mlime na mfuge huku mjini wenzenu wanalia.

Huyu mzee wenu hataongeza mishahara hakuwa na nia hiyo na Corona imempa sababu maana ndio kitakuwa kisingizo na kwa uzoefu wangu wafanyakazi wa hizi ofisi na zinginezo zinazofanana na hizi wanatia huruma sana maana mshahara tu wa mtu mwenye degree haumfikii hata nusu wa mlinzi au msaidizi wa ofisi wa BOT, TPDC, msd, TCRA, Nhif ama TPA Aliye na cheti cha form four tu na wengi wao hawana Allowance zozote .... poleni sana ndugu zangu

Tasisi ambazo wafanyakazi wake hawataathirika hata kama namba one asipoongeza mishahara kwa kipindi chote atakachokuwa madarakani na ambao wataendelea kula bata hata iweje ni, TCRA, TPDC, TANAPA, NSSF, WCF, PSSSF, Majeshi yote kasoro magereza, TAKUKURU, NHIF, KADCO, TANROAD, TANESCO, TIC, TRA, NGORONGORO, TANAPA, TBS, BOT, NEC, TASAC, LATRA, TPA, EWURA, NAO, MSD, madini, TMDA... na nyingine mtaongezea watumishi wa taasisi hizi hata kama mzee asipoongeza hawa hawana shida, kuna baadhi ya taasisi wana Allowance nyingi kiasi kwamba kila wiki pesa inaingia kwenye account ya mtumishi

Cheza mbali na taasisi za mwanzo nilizozitaja, watumishi wa hizo taasisi hakuna rangi wataacha kuiona hii miaka ya utawala wa namba one na mbaya Zaidi viongozi wa hizo taasisi wengi wao wana roho mbaya wapo kwa ajili ya kujilipa miposho na allowance nyingi kwao wao tu, na ni watu wa kupenda umbeya sana kutoka kwa watumishi ambao wamewafanya baadhi yao wajipendekeze kwao ili wapate angalau visafari na semina.

Hali ni tofauti kwenye taasisi zinazolipa vizuri, viongozi wao mara nyingi hawajali umbeya, wao wanaangalia professionalism na uchapa kazi na wanawajali sana wafanyakazi wao, nimeshuhudia mara nyingi inapotokea mfanyakazi akapata matatizo ambayo yakamfanya awe na msongo wa mawazo na viongozi wakafahamu watafanya kila namna ili kumrudisha na kumsaidia mfanyakazi wao awe katika hali ya kawaida...ukiwa mmoja wa watumishi katika taasisi hizi nakupa hongera SANA, lakini kama uko kundi la kwanza Aisee pole sana lazma upambane na utindio wa ubongo katika kipindi hiki.
 
Mkuu ungekuwa unajua hata hao uliowataja hawana afadhali ungekaa kimya tu.Kote huko kumeshatangazwa panga
 
Mkuu ungekuwa unajua hata hao uliowataja hawana afadhali ungekaa kimya tu.Kote huko kumeshatangazwa panga
sio kweli mkuu,..huwezi kuwalinganisha na hao wa taasisi za hapo juu hata Training watumishi wao wanazisikia tu kwenye vyombo vya habari na ikitokea zikawepo kwa sababu ya ukata viongozi wanakuwa na upendeleo kwa watu wao...mkuu huko ni Zaidi ya kilio
 
Ingekuwa uwezo wangu nchi hii bado changa sana, wafanyakazi wote wa umma wangekuwa na rate sawa za mishahara kulingana na elimu zao,..Tatizo sasa hata hiyo tume ya mishahara ni porojo tu hakuna outcome yoyote kwenye hiyo tume kwa watumishi.

na Watawala wamefanya makusudi kuweka taasisi zinazolipa vizuri ili wapate sehemu za kuwaweka watoto wao, vimada na jamaa zao….

Hivi kwa Maisha ya leo kuna watu wanalipwa 300k kwa mwezi na bila posho yoyote kwa serikali hii inayojiita ya wanyonge? …..

Kuna watumishi ukiwaona unawahurumia aiseee
 
Yaani unawashauri wabaki shamba?

Binafsi huwa nawaonea huruma wafanyakazi wa vijijini. Huku Dsm ni kama kichwa chako hakitoshi utaumia. Wale wote waliochukua mkopo na kujengea nyumba, maumivu wanayopata ni kudharirika.

Kila siku nawaambia rafiki zangu ukiishi town jione mjasiriamali zaidi kuliko mfanyakazi. Sijawahi kujuta kuwa Dsm hata siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani unawashauri wabaki shamba?

Binafsi huwa nawaonea huruma wafanyakazi wa vijijini. Huku Dsm ni kama kichwa chako hakitoshi utaumia. Wale wote waliochukua mkopo na kujengea nyumba, maumivu wanayopata ni kudharirika.

Kila siku nawaambia rafiki zangu ukiishi town jione mjasiriamali zaidi kuliko mfanyakazi. Sijawahi kujuta kuwa Dsm hata siku moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Walio chukua mikopo na kujengea nyumba wanapata maumivu gan mkuu? Changanua hapa kidogo
 
Back
Top Bottom