Kupandishwa vyeo, mishahara na mengineyo: Watumishi wa umma mna maoni gani?

Sio Mwongozo tu kasome Standing order ndivyo isemavyo. Ni Kweli umepoteza Sifa za kupata daraja mpk ufidie Muda uliosoma

Dumelang
Huu ni uonevu na uvunjifu wa haki za kibinadamu. Yaani mtu kaenda kusoma kuja kusaidia taasisi/ taifa halafu bado ananyongwa, kwa kweli Tanzania ni nchi ya vituko.
 
andamana kadai haki zako ASAP
 
Pesa haipaswi kukaa mfukoni mwa mtu asiyejielewa. Labda ipitie tu kwake na kwenda kwa anayejielewa.
Si kwamba watumishi wote ni mifuko, bali asilimia kubwa ni mifuko, hawajielewi. Na hawa mifuko ndiyo wanaowaponza wenzao.

Kiongozi anapowaangalia hawa mifukoni anapata picha ya kundi zima. Inapelekea kiongozi kuamua lolote juu ya watumishi wa umma bila woga.

- Watumishi wa idara mbalimbali walilipwa Tsh. 20000 ili wakafanye maandamano ya amani kumsifia mtu aliyerudisha kikokotoo cha zamani. Ijulikane kuwa si kikokotoo kipya wala cha zamani kinachoweza kumpa mtumishi wa umma maisha bora.

Waliweza kusahau maumivu yao ya kutoongezewa mishahara na kutokupanda madaraja kwa miaka karibu 4 wakaingia road kwa shinikizo la wanasiasa wachache kwa malipo ya fedha ambayo nikimpa mwanangu wa la kwanza Jumamosi asubuhi mapema siku anayoshinda nyumbani mpaka saa 12 mfukoni anabakiwa na buku tu (Not real).

- Mpaka leo sijapata habari ya mtumishi aliyekwenda ofisi za TUCTA au CW, TALGWU, TUGHE, TUICO kutaka ajiondoe uanachama kwakuwa anakatwa pesa ambayo hajui fedha yake inafanya nini.

Kila leo mtu anajinasibu nchi ina fedha za kutosha ila ukimgusia kuhusu maslahi ya watumishi wanaambiwa wasubiri miradi ikamilike ndipo watafikiriwa na hupiga makofi wakishangilia.

Kama watumishi wenyewe ndiyo hawa, ni bora wasubiri miradi mikubwa ikamilike ndipo walete kelele zao.
 
Japokuwa andiko lako kulielewa inabidi ufanye ibada ya maono kwanza.

Ila ni kweli Watanzania sisi ni wanafiki kinoma. Pembeni huwa tunalalamika maisha magumu na mishahara haitoshi lakni hamna hata mmoja anayeweza kuamka na kufight kwa hili.
 
Watumishi wote wenye big pay wanamuunga mkono jembe la kulimia meno, hata wasipoongeza tutaendelea kupambana na hali zetu, kama huna akili ndo utateseka, wenye shida sio wafanyakazi bali hata wananchi wa kawaida purchasing power inapopungua bidhaa zao hazinunuliwi kwa fujo.

Na ajira za vibarua tutaendelea kuwakamua, maana pesa imekuwa ngumu. Nikikupa kazi ya kujenga, basi tofali moja la block nakupa Tsh. 200/=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga bado unatusumbua Watanzania.

Kikotooo (Tatizo alilolileta kwa makusudi, akalitatua yeye) likawasahaulisha watumishi Mahitaji yao ya msingi kabisa.
 
Kundi la wanasiasa was upinzani wao wamefanya nn wenzao wanapoenda ule upande wa mtesi kila kukicha. Hapa mambo si mepesi hata kidogo serikali hii ukienda kinyume as individual hukosi kesi ya uhujumi uchumi, kwani hao viongozi wa hivyo vyama vya wafanyakazi unafikiri wao hawana familia ama hawaoni wenzao wanavyoteseka.

Tumeona Kabendera na wengine wengi wakisota peke yao. Wewe hapo ulipo umefanya nn dhidi ya haya yanayoendelea na si kwa watumishi tu kila kundi linamachungu yake ila hakuna anayenyanyua mdomo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UJAMAA WA NYERERE uliharibu sana watanzania hasa wale wa zamani lakini amini nawaambia yaliyoko mayoni mwa watumishi wa umma hasa vijana ambao ndio wengi ni mazito. Siku hasira ikiwa ya kutosha vifuani mwao watawasha moto ambapo itakuwa ni vigumu sana kuuzima.

Wajamaa wamebaki wachache ila wengi wao ndio wenye nguvu, waliberali na mapepari wapo wengi ila hawana nguvu za dola, ni swala la muda tu wajamaa wasifanye sherehe.

Landson Tz
 
Umeusema ukweli.

Kuna siku tupo kikao X, wafanyakazi wa digrii wakawa wanamchana live mwajiri, lakini cha ajabu wa certificate ambao ni wengi wakaungana na mwajiri kwenye maovu.


Asili itaamua, work as you earn
 
sinajinasasa,
Kwa kweli vibarua inabidi wavumilie, kazi ambayo angetarajia kupata laki mbili ataambulia buku 10 angalau akanunue dona na tembele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…