Kupanga Maandamano siku ya Krismas ni mbinu ya watawala kuyaondolea nguvu na hatimaye kuyazika 🇹🇿

Status
Not open for further replies.

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
15,052
Reaction score
36,866
Binafsi naamini huu ni mkakati wa kudhoofisha sauti za wengi:

Kupanga maandamano siku ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya kidini ni mbinu ya kulipasua kundi la wanaodai mabadiliko, kuwapunguzia nguvu na hatimaye kulizika. Hii nii old trick, usipoweza kuwashinda kwa wingi wao basi watengenezee mpasuko wapambane wenyewe kwa wenyewe.

Harakati za kudai haki na mabadiliko zimekua zikipewa msukumo na viongozi wengi wa madhehebu ya kikristo. Kupanga D25 (siku ya Krismas) ni kulazimisha kutoungwa mkono kwa maandamano na kuyabebesha sura mbaya ya machafuko dhidi ya wale wataonyang’anywa kwa lazima haki yao ya kuabudu siku hiyo.

Najiuliza:
Kwanini maandamano haya makubwa hayajapangwa tarehe 26 ambayo pia ni siku ya mapumziko? Dec 26 (boxing day) ni ijumaa inayofuatiwa na weekend ambayo inatoa nafasi nzuri ya kuendeleza maandamano bila kukoma. Kwanini yaanze tarehe 25? logic yake ni nini?

KWA WASIOJUA:

Siku ya Noel / krismas ni siku muhimu zaidi kwa imani ya kikristo, siyo maadhimisho ya kidini tu, ila kwa madhehebu mengi hii ni siku ya kiimani ya familia na sikukuu ya watoto kupitia kuzaliwa kwa Kristo.

Kwa wakatoliki, hii ni moja ya siku kubwa zaidi za ubatizo wa watoto wachanga na wale ambao wanabadili dini ili kuwa wakatoliki. 

Wakristo vuguvugu ambao huenda kanisani mara moja kwa mwaka, huwa wanaenda ibada ya Noel (either mkesha wa usiku au ibada kuu). Hii ni siku ambayo makanisa yanafurika na kuhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote ndani ya mwaka.

******
Kupanga maandamano siku hii kutaleta mvurugano kwa kuwalazimisha baadhi ya wenzetu kuchagua kati ya imani zao za kidini au uzalendo wao kwa taifa - Kama unaamini tofauti, niambie wewe unalionaje hili?

MUHIMU - Walio karibu na wale wenye jukumu la kupanga hizi tarehe wajaribu kuwashauri, unless hao wanaopanga tarehe tayari wameshawahiwa na kupangwa na wadhalimu 🙁 kwa lengo la kufanya maandamano yafeli.

Jumapili njema!
 
Naomba mwenye kuelewa anieleweshe, mojawapo ya vikwazo vilivyoibuka D9 ni kutokuwepo kwa usafiri wa umma.
Siku za krisimasi huwa barabara ni nyeupe sana. Kwa nini watu wanarudia kwenye mtego uleule?!
Siku za mapumziko watu wataambiwa wapumzike ndani na familia zao!
Kwa nini maandamano yasifanyike siku za kazi?!
 
Binafsi naamini huu ni mkakati wa kudhoofisha sauti za wengi:

Kupanga maandamano siku ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya kidini ni mbinu ya kulipasua kundi la wanaodai mabadiliko, kuwapunguzia nguvu na hatimaye kulizika. Hii nii old trick, usipoweza kuwashinda kwa wingi wao basi watengenezee mpasuko wapambane wenyewe kwa wenyewe.

Harakati za kudai haki na mabadiliko zimekua zikipewa msukumo na viongozi wengi wa madhehebu ya kikristo. Kupanga D25 (siku ya Krismas) ni kulazimisha kutoungwa mkono kwa maandamano na kuyabebesha sura mbaya ya machafuko dhidi ya wale wataonyang’anywa kwa lazima haki yao ya kuabudu siku hiyo.

Najiuliza:
Kwanini maandamano haya makubwa hayajapangwa tarehe 26 ambayo pia ni siku ya mapumziko? Dec 26 (boxing day) ni ijumaa inayofuatiwa na weekend ambayo inatoa nafasi nzuri ya kuendeleza maandamano bila kukoma. Kwanini yaanze tarehe 25? logic yake ni nini?

KWA WASIOJUA:
Siku ya Noel / krismas siyo sikukuu ya kidini tu, kwa madhehebu mengi ya kikristo hii ni siku ya kiimani ya familia na sikukuu ya watoto kupitia kuzaliwa kwa Kristo.

Kwa wakatoliki, hii ni moja ya siku kubwa zaidi za ubatizo wa watoto wachanga na wale ambao wanabadili dini ili kuwa wakatoliki. 

Wakristo vuguvugu ambao huenda kanisani mara moja kwa mwaka, huwa wanaenda ibada ya Noel (either mkesha wa usiku au ibada kuu). Hii ni siku ambayo makanisa yanafurika na kuhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote ndani ya mwaka.

******
Kupanga maandamano siku hii kutaleta mvurugano kwa kuwalazimisha baadhi ya wenzetu kuchagua kati ya imani zao za kidini au uzalendo wao kwa taifa - Kama unaamini tofauti, niambie wewe unalionaje hili?

MUHIMU - Walio karibu na wale waliopewa jukumu la kupanga hizi tarehe wajaribu kuwashauri, unless hao wanaopanga tarehe tayari wameshawahiwa na kupangwa na wadhalimu 🙁 kwa lengo la kufanya maandamano yafeli.

Jumapili njema!
Rais alishasema njooni hata kesho, msisubiri Xmas, vyombo vya dola viko kamili gado.
 
Naomba mwenye kuelewa anieleweshe, mojawapo ya vikwazo vilivyoibuka D9 ni kutokuwepo kwa usafiri wa umma.
Siku za krisimasi huwa barabara ni nyeupe sana. Kwa nini watu wanarudia kwenye mtego uleule?!
Siku za mapumziko watu wataambiwa wapumzike ndani na familia zao!
Kwa nini maandamano yasifanyike siku za kazi?!
Maandamano yanaweza kifanyika hata kesho, kikubwa watu wahamasushane mitandaoni. Hakuna haja ya kusubiri sikukuu za kitaifa.
 
kuna kitu wanakosea ndo maan wanafeli,

anaetaka kufanya kitu huwa hatangazi.
Nchi yetu raia bado wachanga kwenye haya mambo so kuwapata watu kwa surprise bila kutangaza na kuhamasisha kwa muda mrefu ni ngumu hii inawalazimisha wanaharakati kutumia muda mwingi kuwabembeleza na kuwaelimisha raia
 
Naomba mwenye kuelewa anieleweshe, mojawapo ya vikwazo vilivyoibuka D9 ni kutokuwepo kwa usafiri wa umma.
Siku za krisimasi huwa barabara ni nyeupe sana. Kwa nini watu wanarudia kwenye mtego uleule?!
Siku za mapumziko watu wataambiwa wapumzike ndani na familia zao!
Kwa nini maandamano yasifanyike siku za kazi?!
Siku ya Krismasi hawatokata usafiri kabisa kwa ajili ya wanaoenda makanisani, labda na zile outing za sikukuu.
Ila kwa hali ilivyo sijui kwa mwaka huu itakuwaje.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom