Kupanga Maandamano siku ya Krismas ni mbinu ya watawala kuyaondolea nguvu na hatimaye kuyazika 🇹🇿

Status
Not open for further replies.
Jumapili ya leo ni nzuri sana, ni jumapili ya furaha, jumapili ya tatu ya majilio, huwa ni nzuri sana.
Masomo ya leo ni mazuri
Wimbo wa katikati
Zab 146:6-10

Bwana huwafumbua macho waliopofuka;

Bwana huwainua walioinama;

Bwana huwapenda wenye haki;

Bwana huwahifadhi wageni;

(Kiitikio) Uje Bwana kutuokoa
Ukifika usiche kusali kwa ajili yetu
Wote tuombeane
 
Binafsi naamini huu ni mkakati wa kudhoofisha sauti za wengi:

Kupanga maandamano siku ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya kidini ni mbinu ya kulipasua kundi la wanaodai mabadiliko, kuwapunguzia nguvu na hatimaye kulizika. Hii nii old trick, usipoweza kuwashinda kwa wingi wao basi watengenezee mpasuko wapambane wenyewe kwa wenyewe.

Harakati za kudai haki na mabadiliko zimekua zikipewa msukumo na viongozi wengi wa madhehebu ya kikristo. Kupanga D25 (siku ya Krismas) ni kulazimisha kutoungwa mkono kwa maandamano na kuyabebesha sura mbaya ya machafuko dhidi ya wale wataonyang’anywa kwa lazima haki yao ya kuabudu siku hiyo.

Najiuliza:
Kwanini maandamano haya makubwa hayajapangwa tarehe 26 ambayo pia ni siku ya mapumziko? Dec 26 (boxing day) ni ijumaa inayofuatiwa na weekend ambayo inatoa nafasi nzuri ya kuendeleza maandamano bila kukoma. Kwanini yaanze tarehe 25? logic yake ni nini?

KWA WASIOJUA:

Siku ya Noel / krismas siyo sikukuu ya kidini tu, kwa madhehebu mengi ya kikristo hii ni siku ya kiimani ya familia na sikukuu ya watoto kupitia kuzaliwa kwa Kristo.

Kwa wakatoliki, hii ni moja ya siku kubwa zaidi za ubatizo wa watoto wachanga na wale ambao wanabadili dini ili kuwa wakatoliki. 

Wakristo vuguvugu ambao huenda kanisani mara moja kwa mwaka, huwa wanaenda ibada ya Noel (either mkesha wa usiku au ibada kuu). Hii ni siku ambayo makanisa yanafurika na kuhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote ndani ya mwaka.

******
Kupanga maandamano siku hii kutaleta mvurugano kwa kuwalazimisha baadhi ya wenzetu kuchagua kati ya imani zao za kidini au uzalendo wao kwa taifa - Kama unaamini tofauti, niambie wewe unalionaje hili?

MUHIMU - Walio karibu na wale waliopewa jukumu la kupanga hizi tarehe wajaribu kuwashauri, unless hao wanaopanga tarehe tayari wameshawahiwa na kupangwa na wadhalimu 🙁 kwa lengo la kufanya maandamano yafeli.

Jumapili njema!
maandamano kwa Tanzania ni upuuzi mtupu.
waTanzania wapo milioni 70, wanaoandamana ni elfu1 pekee, that is completely nonsense politically speaking :NoGodNo:
 
Endelea na mapenzi mpenzi.

Hizi mambo zinaenda kama ngazi ni hatua kwa hatua.

Hakuna haja ya kulazimisha. FYI mapinduzi yameshafanyika na umma umeshashinda kilichobaki ni umma kuchukua power na mamlaka kwa asilimia kubwa.

Jiulize swali moja, nani alitegemea na kufikiri kama Kuna siku wabongo wataweza kuandamana na kuingia barabarani?

Amini nakuambia muda waja wengi kama si wote tutaimba wimbo mmoja.

Utekaji na mauaji utakapoanza kutokea kwa tabaka la wanaojiona wapo salama na wameshika Dola ndio itakuwa mwanzo na mwisho wa utawala dhalimu.

Kwa ufupi hakuna serikali imeshajiangukia imebaki jina tu.

Bora upige stori za mapenzi hayo mengine achana nayo kazi imeshamalizika.
 
Wazo lako lina logic!

Siwezi kataa, katika msafara wa mamba na kenge hawakosi.

Ref to: harakati za wanasiasa katika mfumo wa vyama vingi.

Kuna 'wapinzanimamluki' kibao kudhoofisha wapinzani makini.
 
Sijui na mimi naona mabandiko mtandaoni kama hili

View attachment 3515346
Mi kuna uzi nilipost hapa, mama ataongoza kwa shida sana , hili la kupanga tarehe tunalo tokea siku ile leo na kesho na hata kesho kutwa, kwa hio haidhuru tarehe pangwa itaangukia wapi ila mimi naowamba wapange tena ile siku ya shule kufunguliwa walao tukae na watoto wetu siku nyingi nyingi kidogo.
 
Endelea na mapenzi mpenzi.
Mbona kama unanipangia mkuu!
Hizi mambo zinaenda kama ngazi ni hatua kwa hatua.

Hakuna haja ya kulazimisha. FYI mapinduzi yameshafanyika na umma umeshashinda kilichobaki ni umma kuchukua power na mamlaka kwa asilimia kubwa.
Umma unachukuaje power?
Jiulize swali moja, nani alitegemea na kufikiri kama Kuna siku wabongo wataweza kuandamana na kuingia barabarani?
Mimi kama mmoja wa waliosapoti maandamano, niliamini wabongo tukiamua tunaweza.
Amini nakuambia muda waja wengi kama si wote tutaimba wimbo mmoja.

Utekaji na mauaji utakapoanza kutokea kwa tabaka la wanaojiona wapo salama na wameshika Dola ndio itakuwa mwanzo na mwisho wa utawala dhalimu.

Kwa ufupi hakuna serikali imeshajiangukia imebaki jina tu.
Sawa
Bora upige stori za mapenzi hayo mengine achana nayo kazi imeshamalizika.
Kwanini niachane nayo, kwani mimi si mtanzania? au nyie mmeshajipa dhamana ya mawazo yetu wote, hivyo wengine tusiongee?

PS:
Stori za mapenzi zitarudi, usiwaze!
 
kuna kitu wanakosea ndo maan wanafeli,

anaetaka kufanya kitu huwa hatangazi.
Sasa usipoliandaa jambo la kitaifa kwa kuwatangazia wadau, umma utapataje taarifa za kushiriki maandamano?

Hilo jambo si vita kusema unapanga mbinu za kushitukiza, ili kumshinda adui, hilo jambo ni haki ya kila raia kikatiba linatakiwa kufanywa wazi.

Embu labda mkuu toa wazo lako ulitaka wafanyeje namna ya kuutaarifu umma bila jambo hilo kujulikana?
 
Ndiyo maana nafikiri kuna juhudi za kuzika movement, maana D25 ikifeli watu hawatokua na imani tena na wataachana na mambo ya maandamano kabisa.
Na Kwa hali ilivyo, ni Bora wakaandamana kwa kushtukiza Kila pakitikea jambo lisowaridhisha na Maandamano hayo yanaweza yasiwe ya nchi nzima.

Kwa mfano sasa hivi wakazi wa Dar walitakiwa wawe wameaandamana wakishinikiza upatikanaji wa maji huku wakitaka Samia afurushwe.

Kumbuka kardri watu wanavyojiandaa kuandamana nao wanajiandaa na namna ya kuwatuliza.
 
maandamano kwa Tanzania ni upuuzi mtupu.
waTanzania wapo milioni 70, wanaoandamana ni elfu1 pekee, that is completely nonsense politically speaking :NoGodNo:
Kama ni wachache na hawana madhara, kwanini vyombo vya ulinzi na usalama vinatumia nguvu kubwa hivyo kuwazuia?
 
Wazo lako lina logic!

Siwezi kataa, katika msafara wa mamba na kenge hawakosi.

Ref to: harakati za wanasiasa katika mfumo wa vyama vingi.

Kuna 'wapinzanimamluki' kibao kudhoofisha wapinzani makini.
Ni kweli, mimi nina mashaka sana na dhamira ya hii tarehe na siku ya D25, haiingii akilini kabisa.
 
Sasa usipoliandaa jambo la kitaifa kwa kuwatangazia wadau, umma utapataje taarifa za kushiriki maandamano?

Hilo jambo si vita kusema unapanga mbinu za kushitukiza, ili kumshinda adui, hilo jambo ni haki ya kila raia kikatiba linatakiwa kufanywa wazi.

Embu labda mkuu toa wazo lako ulitaka wafanyeje namna ya kuutaarifu umma bila jambo hilo kujulikana?
Watumie code maalum sio kupayuka tu kwenye TikTok kwamba tarehe fulani Kuna maandamano,

sasa nchi inaongozwa kwa mkono wa chuma,haizingatii katiba wala nini halafu uje uiambie tunafanya protest tarehe flani huoni ni upuuzi

na rudia anaetaka kufanya kitu huwa hatangazi.
 
Mi kuna uzi nilipost hapa, mama ataongoza kwa shida sana , hili la kupanga tarehe tunalo tokea siku ile leo na kesho na hata kesho kutwa, kwa hio haidhuru tarehe pangwa itaangukia wapi ila mimi naowamba wapange tena ile siku ya shule kufunguliwa walao tukae na watoto wetu siku nyingi nyingi kidogo.
Uliona mbali sana na hili andiko.
Ni kweli kwa sasa kitakachokua kinafanyika ni zuia zuia tu lakini mbegu imeshapandwa.

Kwa kweli, wengine watoto wametoka boarding, na likizo imekua na matukio, wazazi roho ziko juu juu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom