Kupanga Maandamano siku ya Krismas ni mbinu ya watawala kuyaondolea nguvu na hatimaye kuyazika 🇹🇿

Kupanga Maandamano siku ya Krismas ni mbinu ya watawala kuyaondolea nguvu na hatimaye kuyazika 🇹🇿

Status
Not open for further replies.
Kama ni wachache na hawana madhara, kwanini vyombo vya ulinzi na usalama vinatumia nguvu kubwa hivyo kuwazuia?
activations ya vyombo imara na vya kisasa vya ulinzi na usalama Tanzania, ilipaswa kua hivi hivi tangu tupate uhuru but hapa kua na threats za kiusalama kukaribisha hali hii.

Hivi sasa,
kuna tishio la kiusalama hususani kutoka kwa magaidi wa nje ya nchi na kwahivyo kama taifa makini lenye uongozi madhubuti, hatuna budi kuchukua hatua za tahadhari na kuimarisha ulinzi katika kila kona ya nchi, ili kuzima majaribio ya kigaidi na ya kiharamia endapo yatatokea.

hata hivyo,
kwa kiasi kikubwa vitisho hivyo vya kigaidi hakuna tena na ndio maana jana batilion mbili za JWTZ zimekwenda kulinda amani Central Africa na DRC. Na huo ndio wajibu mkuu wa Tanzania kuhakikisha Africa ni eneo salama na tulivu la kuwekeza kiuchumi na kuishi kwa amni na usalama:NoGodNo:
 
Na Kwa hali ilivyo, ni Bora wakaandamana kwa kushtukiza Kila pakitikea jambo lisowaridhisha na Maandamano hayo yanaweza yasiwe ya nchi nzima.

Kwa mfano sasa hivi wakazi wa Dar walitakiwa wawe wameaandamana wakishinikiza upatikanaji wa maji huku wakitaka Samia afurushwe.
Ni kweli, kutengeneza huo utamaduni ya kutoka na kupaza sauti ni muhimu. Ila nafikiri kwa sasa watu wameamka!
Kumbuka kardri watu wanavyojiandaa kuandamana nao wanajiandaa na namna ya kuwatuliza.
Haitakiwi kua hivi, wananchi inabidi waruhusiwe kuandamana
 
Umeongea vizuri sana
Raia wanatakiwa wawe attention kwamba mda wowote kiranja wa maandamano atapuliza kipenga..

Issue nyingine je nani atakuwa master plan mbeba vision?? na sio tu kusikiliza kila mwanaharakati kama kondoo aliepoteza akili.
 
Ni kweli, kutengeneza huo utamaduni ya kutoka na kupaza sauti ni muhimu. Ila nafikiri kwa sasa watu wameamka!
Watu wanatakiwa waandamane hata umeme ukikatika bila sababu zinazoeleweka.
Haitakiwi kua hivi, wananchi inabidi waruhusiwe kuandamana
Kwa jinsi nchi yetu ilivyo kuwaruhusu watu waandamane ni ngumu, labda kama ni Maandamano ya kumeifu chura.
 
Watumie code maalum sio kupayuka tu kwenye TikTok kwamba tarehe fulani Kuna maandamano,

sasa nchi inaongozwa kwa mkono wa chuma,haizingatii katiba wala nini halafu uje uiambie tunafanya protest tarehe flani huoni ni upuuzi

na rudia anaetaka kufanya kitu huwa hatangazi.
Narudia pia kusema wazo lako ni jema, ila kaa ukielewa kuwa kulificha jambo linalotakiwa kutekelezwa na umma halafu Serikali isilielewe ni vigumu kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano!

Jambo linaloweza kufanyika kwa siri na likafanikiwa ni mashambulizi ya kijeshi yanayofanywa kwa siri kumuwin adui.
 
Kuna la kusherehekea?
Noel ni siku ya watoto kama usemavyo, kama mzazi unasherehekea nini kwa mtoto wako? Elimu, Afya, mazingira?
Kesho ya watoto wako unaiona?

Ni vyema uendelee kula na kufurahi kwenye noel ilihali hujui shule zikifunguliwa utafanya nini na ukosefu wa huduma kama maji

Yule mzazi aliyefiwa na familia yake wakati wa 29, anasherehekea nini? Miezi 2 baada ya kupoteza wapendwa wake?

Kwangu hakuna siku nzuri au mbaya, kama uoneevu upo ukabiliwe bila kujali siku.
 
Umeongea vizuri sana
Raia wanatakiwa wawe attention kwamba mda wowote kiranja wa maandamano atapuliza kipenga..

Issue nyingine je nani atakuwa master plan mbeba vision?? na sio tu kusikiliza kila mwanaharakati kama kondoo aliepoteza akili.
Ni bora zaidi watu wakawa na utamaduni wa kuandamana hata umeme ukikatika bila taarifa, na haijalishi hao watu wako wangapi.

Hii tabia ya kusubiri Maandamano ya nchi nzima yenye tarehe haisaidii.

Mkuu, wanafunzi shuleni hufanya mgomo pale tu wanapogundua uji au wali umepikwa vibaya, hivyo wananchi pia watumie njia hiyo hiyo.

Siku zote mchuzi wa mbwa hunywewa ukiwa bado wa moto.
 
Ni bora tufike huko kuliko kukumbatia amani feki inayomaliza watu kimya kimya.

Kuliko kuwa vuguvugu ni bora uwe wa moto ama wa baridi.
giphy 22.GIF
 
Exactly 💯 kwanza ilitakiwa wasiwe wanatangaza hivi hawajaona hata movie kama One Battle After Another
Kusubiri Maandamano ya nchi nzima hakusaidii mkuu, we ukiona Kuna tatizo sehemu unakokaa kwa mfano maji yakikatika, hamasisha wenzako kama 50 mkaandamane.

Tukishaweza kufanya hivyo itakuwa rahisi kufanya Maandamano ya nchi nzima 😎.
 
Narudia pia kusema wazo lako ni jema, ila kaa ukielewa kuwa kulificha jambo linalotakiwa kutekelezwa na umma halafu Serikali isilielewe ni vigumu kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano!

Jambo linaloweza kufanyika kwa siri na likafanikiwa ni mashambulizi ya kijeshi yanayofanywa kwa siri kumuwin adui.
Point yangu ni kwamba njia inayotumika kuifluence raia kuandamana sio sahihi iko wazi sana inaipa serikali alert ya kujiandaa kuzuia protest.

Inatakiwa raia wajioganizi siku maalum ya kutoka kupitia kiongoz wao master mind mbeba maono...then asubuhi tu mapema dola inashituka raia wako road.
 
Yaani inatakiwa government isijue watu wana kampango gani ni vyema wawe wana tumia hata dark web huko kuliko TikTok
Yeah, labda Tiktok ni too public ila kukosa uongozi na mtu au watu waliobeba maono ya kimkakati ya namna gani kuexecute haya maandamano, inatucost.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom