Baljurashi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2017
- 2,411
- 3,941
Kataa Maandamano yote, siku zote.
Mkuu umeongea vizuri sana na una ubinadamu mkubwa na busara kubwa sana.Big up.Kuna la kusherehekea?
Noel ni siku ya watoto kama usemavyo, kama mzazi unasherehekea nini kwa mtoto wako? Elimu, Afya, mazingira?
Kesho ya watoto wako unaiona?
Ni vyema uendelee kula na kufurahi kwenye noel ilihali hujui shule zikifunguliwa utafanya nini na ukosefu wa huduma kama maji
Yule mzazi aliyefiwa na familia yake wakati wa 29, anasherehekea nini? Miezi 2 baada ya kupoteza wapendwa wake?
Kwangu hakuna siku nzuri au mbaya, kama uoneevu upo ukabiliwe bila kujali siku.
Kwani maandamano hupangwa na serikali?.. halafu kumbe ni vita vya msalaba vinavyoongozwa na kanisa!?Binafsi naamini huu ni mkakati wa kudhoofisha sauti za wengi:
Kupanga maandamano siku ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya kidini ni mbinu ya kulipasua kundi la wanaodai mabadiliko, kuwapunguzia nguvu na hatimaye kulizika. Hii nii old trick, usipoweza kuwashinda kwa wingi wao basi watengenezee mpasuko wapambane wenyewe kwa wenyewe.
Harakati za kudai haki na mabadiliko zimekua zikipewa msukumo na viongozi wengi wa madhehebu ya kikristo. Kupanga D25 (siku ya Krismas) ni kulazimisha kutoungwa mkono kwa maandamano na kuyabebesha sura mbaya ya machafuko dhidi ya wale wataonyang’anywa kwa lazima haki yao ya kuabudu siku hiyo.
Najiuliza:
Kwanini maandamano haya makubwa hayajapangwa tarehe 26 ambayo pia ni siku ya mapumziko? Dec 26 (boxing day) ni ijumaa inayofuatiwa na weekend ambayo inatoa nafasi nzuri ya kuendeleza maandamano bila kukoma. Kwanini yaanze tarehe 25? logic yake ni nini?
KWA WASIOJUA:
Siku ya Noel / krismas siyo sikukuu ya kidini tu, kwa madhehebu mengi ya kikristo hii ni siku ya kiimani ya familia na sikukuu ya watoto kupitia kuzaliwa kwa Kristo.
Kwa wakatoliki, hii ni moja ya siku kubwa zaidi za ubatizo wa watoto wachanga na wale ambao wanabadili dini ili kuwa wakatoliki. Wakristo vuguvugu ambao huenda kanisani mara moja kwa mwaka, huwa wanaenda ibada ya Noel (either mkesha wa usiku au ibada kuu). Hii ni siku ambayo makanisa yanafurika na kuhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote ndani ya mwaka.
******
Kupanga maandamano siku hii kutaleta mvurugano kwa kuwalazimisha baadhi ya wenzetu kuchagua kati ya imani zao za kidini au uzalendo wao kwa taifa - Kama unaamini tofauti, niambie wewe unalionaje hili?
MUHIMU - Walio karibu na wale waliopewa jukumu la kupanga hizi tarehe wajaribu kuwashauri, unless hao wanaopanga tarehe tayari wameshawahiwa na kupangwa na wadhalimu 🙁 kwa lengo la kufanya maandamano yafeli.
Jumapili njema!
Wauaji pia waliua sana kwa sababu za udini ...hivyo maandamano yoyote yanayo tengeneza cream ya dini moja na cream ya wapinga samia ni hatari maana wauaji wakija wanafumua tu ....maandamano yanatakiwa kuwaingiza watu wote wa dini zote wa vyama vyote wa jinsia zote na ili iwe hivyo ni lazima maandamano yapangwe siku za mishemishe nyingi naya fumukie mjini hivyo watu wote watajikuta kwenye maandamanoSioni raha ya xmass kma ndugu zetu wameuliwa kwahiyo kuandamana ni sahihi
activations ya vyombo imara na vya kisasa vya ulinzi na usalama Tanzania, ilipaswa kua hivi hivi tangu tupate uhuru but hapa kua na threats za kiusalama kukaribisha hali hii.
Hivi sasa,
kuna tishio la kiusalama hususani kutoka kwa magaidi wa nje ya nchi na kwahivyo kama taifa makini lenye uongozi madhubuti, hatuna budi kuchukua hatua za tahadhari na kuimarisha ulinzi katika kila kona ya nchi, ili kuzima majaribio ya kigaidi na ya kiharamia endapo yatatokea.
hata hivyo,
kwa kiasi kikubwa vitisho hivyo vya kigaidi hakuna tena na ndio maana jana batilion mbili za JWTZ zimekwenda kulinda amani Central Africa na DRC. Na huo ndio wajibu mkuu wa Tanzania kuhakikisha Africa ni eneo salama na tulivu la kuwekeza kiuchumi na kuishi kwa amni na usalama![]()
Tusichanganye mambo ya kiimani na mengine, huu ni mtego ambao naona tunauingia kichwa kichwa.Kuna la kusherehekea?
Noel ni siku ya watoto kama usemavyo, kama mzazi unasherehekea nini kwa mtoto wako? Elimu, Afya, mazingira?
Kesho ya watoto wako unaiona?
Watu hawaandamani sababu wanajua maisha yao yatabadilika papo kwa hapo, wengi tumaamini kwenye kujenga mifumo bora kuliko iliyopo sasa. Hata maandamano yakifanikiwa, shule zinafunguliwa January sitapata ada kutoka serikalini au kwa mtawala yoyote wa kiasiasa.Ni vyema uendelee kula na kufurahi kwenye noel ilihali hujui shule zikifunguliwa utafanya nini na ukosefu wa huduma kama maji
Kwenda ibadani siku ya Noel haimaanishi hana majonzi ya kupoteza mpendwa wake. Kwa wengi, hii ni siku ya kuomba faraja na kumshtakia Mungu kuhusu ukatili waliofanyiwa. Ukiwaambia kuandamana ni muhimu kuliko kwenda kanisani, kuna wengine waliofiwa utawakosa pia.Yule mzazi aliyefiwa na familia yake wakati wa 29, anasherehekea nini? Miezi 2 baada ya kupoteza wapendwa wake?
Sawa 👍Kwangu hakuna siku nzuri au mbaya, kama uoneevu upo ukabiliwe bila kujali siku.
Basi tusiuingie huu mtegoNi mtego kwa pande zote mbili, wanaharakati na serikali haramu
Hapo kwenye "kuelewa chapu" hapo ndiyo shida 🤣Kupitia onion browser kama torbrowser zao wakielekwezwa kama wanavyokula darasa pale tikitoku wataelewa chapu
Asante sana kwa ufafanuzi kuwa imani haina logic.....Tusichanganye mambo ya kiimani na mengine, huu ni mtego ambao naona tunauingia kichwa kichwa.
Imani haina logic, tunaamini tunavyoamini.
Watu hawaandamani sababu wanajua maisha yao yatabadilika papo kwa hapo, wengi tumaamini kwenye kujenga mifumo bora kuliko iliyopo sasa. Hata maandamano yakifanikiwa, shule zinafunguliwa January sitapata ada kutoka serikalini au kwa mtawala yoyote wa kiasiasa.
Kwenda ibadani siku ya Noel haimaanishi hana majonzi ya kupoteza mpendwa wake. Kwa wengi, hii ni siku ya kuomba faraja na kumshtakia Mungu kuhusu ukatili waliofanyiwa. Ukiwaambia kuandamana ni muhimu kuliko kwenda kanisani, kuna wenginewaliofiwa utawakosa pia.
Sawa 👍
Mpira uko kwetu, tuucheze bila kimakosa, ili wajichanganye wao na sio sisi tena.Tukifanya hivi tutakuwa tumewatia la kati serikali yetu itaishia kupiga yowe soon wataenda kujichanganya
welcome again
