Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Hujawahi kuandika kitu chochote cha maana tangu ujiunge JF.Binafsi naamini huu ni mkakati wa kudhoofisha sauti za wengi:
Kupanga maandamano siku ambayo ni sikukuu muhimu zaidi ya kidini ni mbinu ya kulipasua kundi la wanaodai mabadiliko, kuwapunguzia nguvu na hatimaye kulizika. Hii nii old trick, usipoweza kuwashinda kwa wingi wao basi watengenezee mpasuko wapambane wenyewe kwa wenyewe.
Harakati za kudai haki na mabadiliko zimekua zikipewa msukumo na viongozi wengi wa madhehebu ya kikristo. Kupanga D25 (siku ya Krismas) ni kulazimisha kutoungwa mkono kwa maandamano na kuyabebesha sura mbaya ya machafuko dhidi ya wale wataonyang’anywa kwa lazima haki yao ya kuabudu siku hiyo.
Najiuliza:
Kwanini maandamano haya makubwa hayajapangwa tarehe 26 ambayo pia ni siku ya mapumziko? Dec 26 (boxing day) ni ijumaa inayofuatiwa na weekend ambayo inatoa nafasi nzuri ya kuendeleza maandamano bila kukoma. Kwanini yaanze tarehe 25? logic yake ni nini?
KWA WASIOJUA:
Siku ya Noel / krismas siyo sikukuu ya kidini tu, kwa madhehebu mengi ya kikristo hii ni siku ya kiimani ya familia na sikukuu ya watoto kupitia kuzaliwa kwa Kristo.
Kwa wakatoliki, hii ni moja ya siku kubwa zaidi za ubatizo wa watoto wachanga na wale ambao wanabadili dini ili kuwa wakatoliki. Wakristo vuguvugu ambao huenda kanisani mara moja kwa mwaka, huwa wanaenda ibada ya Noel (either mkesha wa usiku au ibada kuu). Hii ni siku ambayo makanisa yanafurika na kuhudhuriwa na watu wengi zaidi kuliko siku nyingine yoyote ndani ya mwaka.
******
Kupanga maandamano siku hii kutaleta mvurugano kwa kuwalazimisha baadhi ya wenzetu kuchagua kati ya imani zao za kidini au uzalendo wao kwa taifa - Kama unaamini tofauti, niambie wewe unalionaje hili?
MUHIMU - Walio karibu na wale waliopewa jukumu la kupanga hizi tarehe wajaribu kuwashauri, unless hao wanaopanga tarehe tayari wameshawahiwa na kupangwa na wadhalimu 🙁 kwa lengo la kufanya maandamano yafeli.
Jumapili njema!
Pumba mwanzo mwisho.