Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Kupangiwa kazi vijijini tayari unakuwa umeuliwa kifikra na kitaaluma

Nilikuwa nimevamia fan uwalimu ni wito. Mimi niliacha. Kama mkeo ana wito mwache afundishe. Unataka utumie nguvu ya pesa kivipi? Abadilishiwe kituo? Kama ni hilo sawa.
Ukaenda zako kujiajir.
 
kuna raia alipangiwa huko ukerewe ndanindani,sijui ni ukara...
zahanati nzima yeye ndiye dokta,mzalishaji,ushauri nasaha mpaka ulinzi,alifanya kazi wiki 2 akarudi nyumbani.
 
Mkuu kuna vijiji upatikanaji wa kila kitu ni mgumu mfano maji,huduma za fedha,chakula, na kadhalika.
Hali hiyo ndio huwa fursa kwa wenye akili za kujiongeza.
Ukiwa ni mtumishi uliyepangwa kijiji cha aina hiyo na ukalalamika maisha magumu nitakushangaaa!.
Mwaka 2012 nilipangwa kazi kijijini yaani ni kijiji chenye changamoto za kila aina -:
1.Hakuna duka linalouza unga wala mchele.
2. Hakuna huduma ya mgahawa ,badala yake kuna vilabu vya ULABU tu!
3.Hakuna huduma za kifedha zote
4. Mshahara ukiingia Watumishi wa sekta fulani mnajichanga mnampa mwenzenu kadi akawatolee pesa.
5. Hakuna maji kabisaaaa hasa msimu wa kiangazi maji pekee yaliyokuwa yakipatikana ni maji ya MVUA!
5. Hakukuwa na maduka wala magenge hata ya kuuza nyanya!
6.Hakukuwa na migahawa wala Mama na Baba lishe

7. Mboga pekee salama ya kula ni kununua kuku na kuchinja tofauti na hapo utakula chakula bila mboga !
SASA MSWAHILI MIYE NIKASOMA MAZINGIRA NIANZE NA MRADI GANI.? Maana FURSA NI NYINGI NA WALIOPO HAWAZIONI!
Watumishi walikua wakipangwa mahala hapo walikuwa ama wanahama fasta na wengine huamua kuacha kazi kabisaaa.
MRADI WA KWANZA UKAWA KISIMA CHA KIENYEJI CHA MAJI NIKAWEKA WEKA PAMPU NIKAFUNGA BOMBA NA KUANZA KUUZA MAJI.

MRADI WA 2. DUKA
Huduma ya pesa.
Mahitaji yote muhimu
Mbogamboga na nyama .
Kiukweli namshukuru MUUMBA niliweza kuanzisha miradi mingi kidogo kidogo na hatimae nikawa na miradi mikubwa ya biashara, kilimo na kadhalika .
Na bado ninaishi huku na maisha ni murua kabisaa sikumbuki ni lini mara ya mwisho kutumia mshahara wangu kwa kununua chakula mavazi na mambo madogomadogo.
KIUKWELI,

KUISHI VIJIJINI NIFURSA !
SHARTI KUU "USIFANANE NAO"!
Kamba
 
Chief hivi nikiweka 5 million siwez fanikisha uhamisho wa wife.. ndo kwanza amepangiwa huko kijijini.. ila nataka nitumie nguvu ya pesa nimrudishe nilipo.. japo sio jijiji ila kwenye halmashauri ya mji
Acha aka report mkuu walau mwaka kupata barua ya uthubitisho Cheti Cha ndoa Kiko???????? Unaweza piganisha unaumwa unahitaji support yake now huduma inafanyika online
 
Kwani wanaka kwa miaka mingapi au miezi tu? Wewe unajilinganisha na watu wanao lipwa mshahara na allowance inao zidi kipato chote cha kijiji wewe unaota, kijijini ni nusu jahanamu unaishi kama mnyama wakufuga.
Acha uongo bro
 
Asilimia 90 ya mabwana shamba/Mifugo wanaishi Mijini Sasa mwaka ujao wa Fedha Serikali imesema inaenda kujenga nyumba 4,000 Ili wajae huko huko kwenye kata zao na kumbuka wanariooti Kwa Mtendaji Kata so hatua Kwa hatua wowote wataishi Vijijini
Shida ilikuwa nyumba ?

Kama kuna shida za ajira na leo ukitangaza nafasi ya Mabwana Shamba watakuja lukuki kuomba au kama watu ambao wapo vijijini wanaweza kupata crash course; kwanini tusubiri kodi zetu ziende kufanya vitu ambavyo huenda mwisho wa siku ni miradi ya watu....

Okay huyu Bwana apange nyumba ya Serikali ambayo atakuja mtu kesho au keshokutwa aseme ku-manage nyumba ni gharama hivyo ziuzwe...., Kwanini hawa watu wasiende leo kwani kwenye mishahara yao hakuna house allowance !????
 
Njoo uishi huku
Watu wanakula maisha
tu
Siwezi ng'oka MOMBA DC
[emoji16]
Huko sijii hata kwasababu gani sijiiii...

Nilikujaga kununua ufuta 2020
Kikajiuliza, ambapo na wewe nakuuliza....

"Hivi watumishi wa huko bondeni nilikonunua ufuta (Chitete, Chilulumo, Mkulwe, Mpapa na Hadi kule chinii kwenye mpunga mwingii) HAYO MAISHA WANAKULA WAPI?""

Ukiajiriwa sehemu kama hizo we ujue CONNECTION YA DUNIA HUNAAAA, Kazi yako itakuwa ni kulima, kufuga huna fursa nyengine.

#YNWA
 
Shida ilikuwa nyumba ?

Kama kuna shida na ajira na leo ukitangaza nafasi ya Mabwana Shamba watakuja lukuki kuomba au kama watu ambao wapo vijijini wanaweza kupata crash course; kwanini tusubiri kodi zetu ziende kufanya vitu ambavyo huenda mwisho wa siku ni miradi ya watu....

Okay huyu Bwana apange nyumba ya Serikali ambayo atakuja mtu kesho au keshokutwa aseme ku-manage nyumba ni gharama hivyo ziuzwe...., Kwanini hawa watu wasiende leo kwani kwenye mishahara yao hakuna house allowance !????
Duu pengine ni motisha ya kazi but pia Serikali Iko kwenye mkakati wa kuanzisha irrigation schemes huko Vijijini xinahitaji usimamizi wa karibu wa watu ambao wako site mda wote sio wanaokaa mjini Hadi wapigiwe simu Waseme hawana usafiri nk
 
Huko sijii hata kwasababu gani sijiiii...

Nilikujaga kununua ufuta 2020
Kikajiuliza, ambapo na wewe nakuuliza....

"Hivi watumishi wa huko bondeni nilikonunua ufuta (Chitete, Chilulumo, Mkulwe, Mpapa na Hadi kule chinii kwenye mpunga mwingii) HAYO MAISHA WANAKULA WAPI?""

Ukiajiriwa sehemu kama hizo we ujue CONNECTION YA DUNIA HUNAAAA, Kazi yako itakuwa ni kulima, kufuga huna fursa nyengine.

#YNWA
Mbona uli survive siku zote hizo ulizonunua mazao? Uliishije? Acha kutosha watu broo.

Harafu Kwa Sasa mambo yamebadikika sana ,ulikuja wakati Samia sio Rais Toka ameingia amejaza pesa nyingi sana kwenye Barabara za Vijijini,maji Vijiji,Huduma za Afya ,umeme nk kiasi kwamba mabadiliko ni makubwa sana kama ukienda Leo.
 
Halmashauri za Vijijini ndio Halmashauri gani? Sema kuishi Vijijini sometimes ndio mtihani lakini Ukiwa Wilayani Kuna shida gani Huduma zote zipo..

Hii kauli yako UMEITHIBITISHA?
Umefika Momba, Ileje na Tanganyika?
1. Momba huduma zao za financial na social wanazipatia Vwawa na Tunduma
2. Ileje wao ni Mpemba au Tunduma.

Hebu fanya research ndio uje kuongea.

SHAZ96 huko Momba benki mnapata wapi na huduma Bora za afya?

#YNWA
 
Kuna jamaa kapangiwa kakuta zahanati ipo kwenye lenta hakuna maji hakuna umeme.
Sasa huyo ndio raha anaenda Kwa boss wake ampangie zahanati ya jirani harafu itakuwa maxima maana hiyo Hadi ije kuishi ni mwaka wa Fedha Mwingine Ajira Mpya wengine ndio wataanza nayo 🤪🤪
 
Mbona uli survive siku zote hizo ulizonunua mazao? Uliishije? Acha kutosha watu broo.

Harafu Kwa Sasa mambo yamebadikika sana ,ulikuja wakati Samia sio Rais Toka ameingia amejaza pesa nyingi sana kwenye Barabara za Vijijini,maji Vijiji,Huduma za Afya ,umeme nk kiasi kwamba mabadiliko ni makubwa sana kama ukienda Leo.
Kada kwenye ubora wako.

Uko Momba wapi nije kukutembelea?

#YNWA
 
Kuna mwanetu alipangiwa kufundisha sekondari huko ndani ndani alienda kuripoti halmashauri wakaaanza kupelekwa na landcruiser kila mtu shule anayoenda kufika kwake wanamshusha kwamba wew utafundisha hapa mwamba aligoma kushuka kwenye gari baada ya siku 3 akarudi kitaa kwa Sasa anajiendeshea tipa la mchanga,,vijijini kusikieni tu wajomba
[emoji1787][emoji1787] kiatu Cha udongo u nailed it.
 
Kijijini fursa nyingi sana, hasa kwenye sekta ya ardhi, kilimo, ufugaji (ng'ombe wa maziwa, mbuzi...), usafirishaji, uvuvi (kwa baadhi ya maeneo), maji, na viwanda vidogo (kama kufyatua tofali, kutengeneza makochi, kushona nguo...).

Pia kijijini wana jamii wanakuwa na ushirikiano mkubwa sana kwa wataalamu wa afya, jambo linalokupatia faraja kubwa ambayo ina thamani kubwa isiyoweza kupimwa kwa kipato cha pesa.

Kijijini pia unapata muda wa kuwa karibu na familia yako kama unayo.

Kijijini unaweza kupata nyumba ya serikali bure, au ukapata nyumba nzuri kwa gharama nafuu, hivyo kusave something.

In short kijijini fursa ni nyingi kuliko mjini kwa watu wenye mshahara unaolingana, na kwa mwenye akili inachangamka zaidi nje ya your comfort zone kuliko kudumaa mjini na vijiwe (kufanya fani moja pekee).
Umeshawah kwenda huko kweli au unaropoka tu hapa!
 
Ni ujinga tuu unakusumbua,Cha maana ulichofanya hapo mjini ni kipi? Kwa kuwa unaunga unga ndio maana uliomba kazi ya chini ya 800k Kwa mwezi.

Sasa wenye akili wanataka wapangiwe Vijijini maana ni fasta unakuwa Tajiri..

Harafu mlivyo mbumbumbu mnadhani Vijiji vya Leo ni sawa na vya zamani,Kwa taarifa yenu Vijijini karibu vyote vina umeme,Barabara na issue ya Maji Ruwasa wako kazini..

Ukiniuliza Mimi Vijiji vigumu labda ni vile ambavyo Kilimo,uvuvi na ufugaji havifanyiki..vyenye Hali ya ukame
Fasta unakuwa tajiri!! asikudanganye mtu mkuu, kijijini paskie tuuuu
 
Hii kauli yako UMEITHIBITISHA?
Umefika Momba, Ileje na Tanganyika?
1. Momba huduma zao za financial na social wanazipatia Vwawa na Tunduma
2. Ileje wao ni Mpemba au Tunduma.

Hebu fanya research ndio uje kuongea.

#YNWA
Kote huko nakufahamu Mimi ni WA huko na mzazi wangu alikuwa Mwalimu hizo Wilaya amehanishwa sana hata kabla Momba haijazaliwa..

Sasa Mzee Kuna shida gani kutoka Ileje Hadi Mpemba full mkeka ,harafu Isongole na itumba Kwa Sasa Kuna nafuu sio kama zamani.

Tanganyika Iko jirani na Mpanda Mjini,Momba ndio Bado Kwa sababu Halmashauri ilijengwa Kijijini sana ila Kwa sasa Kuna nafuu kama.alivyokwambia Jamaa hapo Juu sio sawa na 2020 unayoisemea wewe..

Ni kama Vile Uyui pale Makao yya Wilaya panaitwa Isikizya ni Kijiji kabisaa ila bahati Yao wao Barabara kuu..

Tanzania hii naifahamu sana ,Mimi nafanya kazi za ukandarasi Vijijini ndio kazi tunashinda huko..

Mfano Kwa Mkoa wa Rukwa Vijiji vibaya ni vya Mwambao wa Ziwa Tanganyika tuu , vingine vyote vizuri na vinafikika safi yaani viko liveable
 
Back
Top Bottom