Wazo lako lina mashiko isipokua ungelijengea hoja zinazo eleweka kuhusu hususan unapo sema/taka neno utumwa
Kwa namna binadamu walivyo umbika, sio kila mmoja anaweza kufikiri kwa mfanano na mwingine. Na hii imepelekea binadam kugawanyika katika makundi tofauti ili kuweza kupata uwiano na mgawanyo mzuri katika namna ya kuishi ama kujioatia kipato.
Hapa namaanisha sio kila mtu anaweza akawa mfanya biashara ama akajiajiri.
Najaribu kumaanisha kwamba kila mtu akiwa mkulima nani atanunua chakula cha mwingine?
Ama kila mtu akiwa anajitegemea je nani atamtegemea mwingine??
Mkuu, ustaarabu ni jambo la kawaida katika maisha ya binadam, hivyo basi hata unapo kuta wengine wameweka muda wa kula ama nyumbani kwako ukipanga muda wa kula ni jambo la kistaarabu ama utaratibu wa kawaida katika maisha tunayo ishi pamoja na jamii ama maeneo tofauti tofauti
Hapa mwisho nakushauri tu upunguze kuweka umuhimu kwenye maisha ya watu wengine.