Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.

Mkuu Jidu, kwanza kuhoji jambo lolote kuhusu uendeshaji wa Chadema, sio kiherehere, bali ni haki yako kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu kwasababu Chadema ni public party na sio private party, kitu chochote ambacho kinalipwa by taxpayers money, ni public entity, the public has the right to know its affairs na hakina ile kinga ya the rights to privacy kwa public monies.

Tena kwenye nchi za wenzetu, viongozi wote wa umma, their public and private conduct is public rights, hata akionekana tuu barabarani na mdada wa mtaani, ni disgrace to public office, Bill Clinton alitaka kufanyiwa impeachment kwa kosa la ku disgrace the oval office kwa kosa dogo tuu la kumpiga busu la mapenzi, intern Monica Lewinsky kwenye ofisi ya umma. Salama yake ni Monica Lewinsky mwenyewe ndie alimkingia kifua Clinton kwa kutoa ushahidi kuwa ni yeye Monica ndiye aliyatamani busu la Clinton na kula kiapo kuwa affair hiyo iliishia kwenye busu tuu na haukumaliziwa kwenye yale mambo!. Huku kwetu public officers paid by taxpayers money, sio tuu wanapiga mabusu watu wasio wenzi wao, bali hata kuwazalisha kabisa na kitu ambacho ni immorality lakini sis hukui kwetu ni ok kabisa, halafu watu wana preach morality!.

Hili la udikiteta Usultani wa Chadema, niliuzungumza hapa katika bandiko hili.

P
 
Bwana Mayalla, ccm kutawala milele siyo kesi, kesi ni namna ambavyo wanatawala kwa DHULUMA. Wangekuwa wanatenda HAKI upinzani ungekuwepo kwa asilimia chache mno mana upinzani ni kitu kisichozuilika. Sasa hivi chuki ni kubwa mno haimithiliki. Jaribu kuwaambia viongozi wasimamie HAKI waache kutengeneza UADUI baina ya watu, tunakoelekea siyo kwema.

Tamati, KILA CHENYE MWANZO KINA MWISHO.
 
Ndipo mwenyezi Mungu alipomuuliza paskali

Ewe paskali mbona unakengeuka na kuwa mpumbavu?

Ewe paskali hata lini Cha binadamu kikadumu milele?

Mwenyezi Mungu akageuza uso wake kwa hasira na paskali akatindikiwa yote yaliyo mema machoni pa bwana!
 
Rejea matukio ya Malawi na Zimbabwe, Hastings K. Banda na Robert Mugabe hawa wote walikuwa marais wa milele na wote walibebwa sana na majeshi yao na polisi, Mugabe ilifika mke wake akasema hata maiti yake itatawala Zimbabwe! Lakini wote wawili ilichukua siku moja kuondolewa madarakani na majeshi yao ambayo hawakutegemea yangeweza kuwageuka na ndipo umilele wao ulipoishia. Kama zilivyokuwa nchi hizo ndivyo na Tanzania ilivyo kwa majeshi kuibeba CCM lakini tujue kila siku damu nzee huondoka na kuingia damu mpya na fikra mpya hivyo lolote litaweza kutokea.
Mwisho, nani aliweza kufikiria kuwa makaburu wa Afrika Kusini wangeweza kuondoka pamoja na jeshi lake la polisi lilivyokuwa katiri! Kulingana na andiko lako unamwamini mungu lakini mimi ninamwamini Mungu hii ndiyo tofauti yetu ya mawazo.
 
Kulingana na andiko lako unamwamini mungu lakini mimi ninamwamini Mungu hii ndiyo tofauti yetu ya mawazo.
Mkuu Elvis Chirwa, to a devout Catholic kumwambia anaamini mungu, is blasphemous comment.

Kwa vile ni Mungu ndiye anaweka serikali za mataifa, baada ya Tanzania kufanywa ni shamba la bibi kwa muda mrefu, tukamuomba Mungu kwa kusali, kufunga na kuomba atupatie mkombozi wa kulikomboa taifa letu, Mungu akaisikia sala yetu, akajibu maombi na kutupatia rais Magufuli, hivyo rais Magufuli ni chaguo la Mungu kwa Tanzania, hivyo Magufuli atayaweza yote katika YEYE amtiaye nguvu!.


P
 
Kweli upumbavu umetamalaki kwa wasomi dah eti huyu Ni mwanagreat thinker p
 
Ndio maana walevi hawateuliki Leo wa bluu kesho wa kijani angalia deogratius rweyunga wa itv anazeeka bichwa tu
 
Kweli upumbavu umetamalaki kwa wasomi dah eti huyu Ni mwanagreat thinker p
Ni kawaida, hata Galileo Galilei alipokundua dunia ni duara, aliuliwa kwa kumkufuru Mungu!.
Hata Archimedes alipogundua the law of flotation, alitoka bafuni mbio kama alivyozaliwa na kuingia mtaani, huku akipiga kelele "eureka eureka " watu wamdhania ni kichwa!.
P
 
P Pasko unaakili ila ni mpumbavu utanisamehe ila wewe sidhani Kama uko sawa kichwani na matangazo ya frilensa hutapata ngoo kuanzia sasa !!! Toka siku ile nakuona unaingia geti la kijitonyama mkabala na ile pub opozit a getini nilikuona kirusi.
 
P
Pasko unaakili ila ni mpumbavu utanisamehe ila wewe sidhani Kama uko sawa kichwani na matangazo ya frilensa hutapata ngoo kuanzia sasa !!! Toka siku ile nakuona unaingia geti la kijitonyama mkabala na ile pub opozit a getini nilikuona kirusi.
Mtu ambaye hayuko sawa kichwani, akafanye nini Kijitonyama, wakati huwa wanachukua the top cream?.

Sasa wewe umeniona naingia Kijitonyama tuu ukaniona kirusi, ambapo ni eneo la makazi na kuna public hospital mule, anybody can go, jee siku ukigundua ofisi yangu iko Eagle Wing pale St. Peter's, utasemaje?.
P
 
Naona niliposema ninamwamini Mungu nilikuwa ninagofautisha kati ya mungu (uliyoitumia wewe) na Mungu (niliyemsema mimi) ni vigumu kuelewa. Inawezekana jina mungu ulilitumia kimakosa badala ya Mungu.
Hilo la kufunga na kumuomba Mungu sijui tulilifanyia wapi! Na kama watanzania tulilifanya kama usemavyo sijui kwanini tuliingia kwenye uchaguzi. Haya mambo ya kudanganya eti tuliomba yako kwenye nchi za wanyonge na masikini tu, Kenya hauwezi ukayakuta.
 
milele ina maana mbili na zote ni za kidini na sio za mtu kuishi siku moja na kufa ndio kuwa milele yake acha kudanganya watu labda useme huo ni uelewa wako, unasema watu watapona kwa kuujua ukweli wakati we unadanganya watu,.
KWA TAARIFA YAKO HAKUNA MAHUSIANO YA MWANADAMU KWENDA MBINGUNI HATA AKIWA MTAKJATIFU. KAMA UNA ANDIKO NIPE NISOME. HATA MWISHO MUNGU ATAUMBA MBINGU MPYA NA NCHI MPYA WANADAMU WATAENDELEA KUKAA KWENYE NCHI MPYA KAMA HUELEWI MAMBO YA UFALME WA MUNGU USIDANGANYE WATU. WE ENEDELEA KUSAKA UTEUZI KWA KUDANGANYA WATU NA KUMFANANISHA MUNGU NA CCM. MUNGU HAFANANISHWI KWA NAMNA YOYOTE ILE
 
kama niliandika mungu badala ya Mungu, sorry ni typo!. Maombi tuliyafanya humu jf wakati tukimuita JK, dhaifu!.

Mkuu Mystery karibu mitaa hii,
Hakuna wa kuitoa CCM madarakani kwasababu Tanzania hapa tulipo hatuna upinzani kabisa, huu upinzani uliopo ni upinzani uchwara, not serious not credible hivyo CCM itaendelea kutawala milele
P
 

Mimi ni miongoni wa watu wanaochukua tahadhari sana katika kuelewa maandiko ya Pascal Mayalla sababu ndani yake huwa kuna falsafa yenye kuhitaji tafakuri ya kina. Kwa mfano U MILELE wa Mayalla unaohusishwa na imani za ki Uungu inanifanya kutambua U-Milele huu sio ule niitambuayo kwa tafsiri ya kiswahili ya Kingazija, "INFINITY" Bali yaweza kuwa ni U milele kwa maana ya muda mrefu sana.

Lakini hata Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru, akimpigia debe mgombea Urais 2015 alitoa maono juu ya mstakabali wa mabadiliko ya kisiasa nchini alipotuambia kuwa CCM isipotoka madarakani kwa vuguvugu hili la sasa haitatoka tena madarakani. Na hakika hakumaanisha Milele kwa maana hii ya tafsiri ya Kingazija.

Na tusitarajie CCM kuondoka madarakani kwa kushindwa kuwaondoa maadui zetu watatu UMASIKINI, UJINGA na MARADHI. Kwani maadui hawa wamejengwa kwa misingi ya kanuni za uumbaji. Ni maadui ambao wapo na wataendelea kuwepo isipokuwa kwa taswira tofauti kulingana na hali na wakati unaoendana na mabadiliko ya maendeleo na uumbaji. Kudhani maadui hawa iko siku watakwisha ni kujidanganya na Kwa maana hiyo ni vita ya kudumu inayobidilika kulingana na mabadiliko ya kimaendeleo.

Ndio maana napoangalia Maamuzi, mienendo na mifumo ya vyama vyetu Vikuu vya Upinzani (Mf. Chadema na CUF) vinatoa mashaka ya kutwaa madaraka siku za Karibuni. vinajiingiza kwenye migogoro inatakayo wachukulia muda wao katika kuirekebisha na hatimae kurejea kwenye malengo ya kuchukua uongozi wa nchi.

Huwezi kujitoa kwenye uchaguzi wa muhimu wa Serikali za Mitaa (Wapiga Debe) na mara ukaingia kwenye mgogoro wa Demokrasia ndani ya Chama chenyewe na muda mfupi huu uliobakia ukatarajia kuchukua uongozi wa Nchi. Haya ni majeraha yatakulia muda wa kujipanga upya kwa ajili ya miaka kumi ijayo.
 
Hiki nilichokisema kwenye bandiko hili, leo kimewekwa wazi na Katibu Mkuu wa CCM
Dkt. Bashiru katika bandiko hili

Dkt. Bashiru: Aliye na dola ndiye ananufaika nayo kubaki madarakani, hata CHADEMA ikiingia madarakani ikaondolewa kwenye dola ni uzembe wao

Dr. Bashiru amesema
Hivyo tunapo waeleza humu kuwa CCM itatawala milele, naomba mtuelewe!, huu ndio ukweli wa siasa zetu.
P
 
Mada yako Ni Moto unaounguza,nasikitika watu wa ajabu Kama mtu anejiita Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayala wangekua na wao walimsikia Bashiri Ali Katibu Mkuu wa CCM alipokua akiyatamka hayo kwa kinywa chake.Lakini bahati mbaya hawakumsikia.
Huwa ananikumbushia sana Pascal Mayalla , wamefanana sana uandishi nk.
Pascal Mayala hawezi kuja kwa uzi huu na yule mtu Mwanakijiji.

Wengi wenu ndio mmefunguliwa macho na Dr. Bashiru, angalie akina sisi hili tuliliona lini na tukalizungumza, hivyo hakuna kipya Dr. Bashiru alichozungumza, only to confirm something that was already there and already known.
CCM ni chama dola, kitatawala milele!.

P
 
Pascal naomba nikushauri kitu kimoja ndugu yangu,kwa ruhusa yako Mkuu.
 
Ndo maana hausapoti tume huru?
 
Ndo maana hausapoti tume huru?
Tume huru ipi wakati hii iliyopo ni huru?, inahitaji tuu kuwa Shirikishi. Tatizo la uchaguzi Tanzania sio Tume huru bali uwanja sawa wa kufanya siasa.

Aliyezuia mikutano ya siasa sio NEC, ni mtu kajizuilia tuu, katiba ipo, waliozuiwa kinyume cha katiba wapo na wanaangalia tuu!.

Pamoja na matatizo mengine yote, Tanzania hatuna any serious and credible opposition.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…