Kupata maendeleo ya kweli, Watanzania ni lazima tujifunze kuukubali ukweli!. Hili la CCM kutawala milele ni kweli!.

Hivi vitu lazima uviondowe mwenyewe, serikali haihusiani kabisa!
Hivi unajua Mafia wanapelekewa meli, wanaiaribu ili wabaki na ngalawa zao?
Hivi kumbe Kisiwa cha Mafia wamelekewa Meli wakaiaribu ....? ......Huo ndio ujinga....adui namba moja......
Meli kama ile Mv Kigamboni?
 
Wewe ni kilaza wa kufa mtu mkuu,mimi nimesoma bandiko lako nikitegemea kuona kama kuna sehemu utaandika sababu za CCM kutawala milele ni zipi ila wala sijaona!!
 
Inaonekana ww na mtoto wako mnakaa mnadiskasi kidemokrasia akikosea au akikukosea,
Watoto wangu sijawahi kuwaadhibu hata siku moja,Nimewapa uhuru wa kajadiliana na mimi kila kitu,kama mzee,...,Watoto wangu wamefankiwa sana kimaisha

Mtoto kama mtoto ana safari refu ya kusoma taangu anazaliwa mpaka anakuwa mkubwa wa kutengeneza familia yake mwenye sasa kama una tabia ya kumpiga na kuanza kumuadhibu mtoto atasoma nini kutoka kwako kama mzee...

Mkuu,haya ninayo kufahamisha ni tabu sana kwa wewe kufahamu,lakini kama hii habari ataisoma Muhindi,Mwarabu,Mzungu watafahamu nini ninachoongea
 
Ccm wanajua wa tz ni wapole ndio maana wanawachezea watakavyo waliosema amani haiji ila kwa ncha ya upanga hawakukosea tungechapana hata kwa wiki moja tungeheshimiana sana wanachofanya ccm ni sawa na kumtia mwanaume mwenzako kidole halafu badala ya kuchukia anachekacheka ulaya waliheshimiana baada ya vita so was Kenyans cc bado tuko usingizi wa pono ccm wasiombee wa tz waamke watatafuta mlango wa kutokea hawatauona
 
KUSEMA CCM ITAKAA MILELE NI KAMA KUMTUKANA MUNGU, kwa sababu Mungu peke yake NDIYE aliyekuwepo tangia kitambo na atakuwepo milele.
 
Hii ya kutawala milele inaukakasi kidogo Mkuu. Hao watu wametawala kwa zaidi ya miaka 50 yenye mambo mengi ya kujiuliza. Bado mpaka leo hatujaweza kuondoa maaadui watano wa Taifa letu, UMASIKINI, UJINGA, MARADHI, UNAFKI NA NJAA. Wakati mwingine huwa najiuliza maswali mengi sana kuhusu aina za siasa za nchi yetu, nadhani matumizi ya akili zetu hayana nafasi kabisa. Naomba tufanye objective analysis tuongozwe na facts na siyo ushabiki au mapenzi. Muheshimiwa Raisi anatimiza wajibu wake kama Raisi na hayo ndiyo mategemeo ya waajiri wake ambao ni sisi wapiga kura.

Miaka 50 kwa NCHI ni midogo sana. Hata kizazi kimoja hakijapita tangu Uhuru!! Angalia China na India ndo utajua uwiano wa miaka kwa maendeleo ya NCHI.
 
Mkuu angalia Korea ya kusini na Africa zilikuwa wapi 50 yrs ago na sasa tuko wapi. Miaka 50 ni mingi kama unabaki pale pale na wengine wanachapa mwendo.
 
Swala la CCM kutawala milele sikubaliani nalo. Ila ni kweli itaendelea kutawala kwa kipindi kirefu kijacho na hasa ukizingatia mikakati inayojengwa ikihinikizwa na China, kuhakikisha vyama vyote vilivyoshiriki kupigania ukombozi Afrika havipotei. Ni ukweli kuwa China ilihamanika sana kupotea kwa UNIP ya Zambia na KANU ya Kenya ikiamini ni mkakati wa nchi za magharibi kuviondoa madarakani vyama vilivyopigania uhuru barani Afrika. Ndio maana imekuja na mkakati huu wa kuvinusuru kwa kuvijengea uwezo wa kimkakati kuhakikisha havipotei. China imeamua kutumia resorcess zake kuvinusuru vyama hivi na inaelekea kufanikiwa kama si hivyo mapinduzi ya Mugabe na Zuma, ZANU PF na ANC vilikuwa inaelekea kupotea.
 
"CCM ita tawala milele, endapo hakuna kitakacho badirika, hii ni kutokana na uendeshaji wa siasa za sasa, Tuukubari kweli, magufuli kasema ukweli"

Mwaka 2015 CCM walipata kura milioni 5.5 upinzami walipata kura mikioni 4.2,
Wananchi milioni 4.2 ni wapinzani wa serikali ya CCM, hao akina mbowe, zito, Lisu, Mdee na wengineo wengi hao ni wawakilishi tu, unapozungumzia upinzani zungumzia hilo kundi hapo juu.

Haya mambo hayajaanza awamu hii, yalikuwepo tokea zamani, Ajenda ya ufisadi iliwapa nguvu wapinzani,

Ilizimika mwaka 2015 baada ya ujio wa JPM,

Ajenda inayofuata ndiyo itakayo ondoa ukweli huo ulio ueleza, hii huenda ikawa ni ajenda hatari kuliko ile ya ufisadi.

Hivyo basi, CCM haitatawala milele.
 
Wanabodi,

Leo tena naendelea na zile Makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Topic yangu ya leo ni kutuhusu sisi Watanzania, ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tujifunze kuupokea na kuubali ukweli halisi, ukweli bayana, hata huo ukweli ukiwa mchungu vipi, ukweli ni ukweli tuu, na siku zote ndio husimama mpaka mwisho. Kali ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuwa "CCM itatawala Milele " ni kauli ya ukweli kabisa kuwa ni ukweli halisi na ukweli bayana, katika mazingira ya sasa ya nchi yetu na uendeshaji wa siasa za vyama vingi, kama hakuna kitakachobadilika, then rais Magufuli yuko very right kuwa CCM itatawala milele!.

Moja kati ya sifa kubwa za rais Magufuli, ni kusema ukweli Daima tena bila kukopesha, wala kurembaremba, japo kuwa mkweli sana sometimes sio nzuri sana kidiplomasia katika baadhi ya maeneo, ambapo diplomasia hutumika, haya mambo ya diplomasia ndio yametufikisha hapa tulipo, sasa ili tutoke hapa na kusonga mbele kimaendeleo, Watanzania ni lazima tujifunze kuubali ukweli jinsi ile ulivyo, bila kurembwa rembwa. La CCM kutawala mimi ni ukweli mtupu.

Itaendelea
La CCM kutawala milele ni la kweli kwani ni agizo la rais na polisi na jeshi wanatakiwa walisimamie kama ilivyo kwa maagizo mengine.
 
mbeleko za mazuzu ya CCM hizi hapa zikipokea maagizo
 
Attachments

  • CCM.jpeg
    CCM.jpeg
    54 KB · Views: 29
Mkuu angalia Korea ya kusini na Africa zilikuwa wapi 50 yrs ago na sasa tuko wapi. Miaka 50 ni mingi kama unabaki pale pale na wengine wanachapa mwendo.

Mataifa hayo ni ya asili. Siyo kama yetu ya kutengeneza. Wenyewe 1950s walikuwa tayari ni mataifa yenye miaka lukuki.
 
Paschal Mayala,naona unatafuta nafasi ya kuteuliwa...utaipata muda siyo mrefu hakuna kilichowahi kudumu milele chini ya jua
Wengi mnashindwa kumsoma Mwanafalsafa Mayala. Ukisoma katikati ya mistari uandishi haubabaishi. Yapo mazingira ya CCM kuendelea kutawala milele, lakini hakuna mazingira ya CCM kutawala milele. Kuna kani kinzani zitakapotokea basi zinauwezo wa kubadilisha kwendo wa chombo kinachosafiri njia nyoofu, kikasimama au kubadili mwelekeo. La pili, Kama ni umilele umehesabiwa sehemu moja tu! yaani Mungu! Kwa maana hiyo, milele ya CCM inaweza kuwa kitambo kidogo tu! Kumbuka miaka 1000 mbele za Mungu ni sawa na usiku wa jana Ukishakupita!
 
Wanabodi,

Leo tena naendelea na zile Makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa. Topic yangu ya leo ni kutuhusu sisi Watanzania, ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tujifunze kuupokea na kuubali ukweli halisi, ukweli bayana, hata huo ukweli ukiwa mchungu vipi, ukweli ni ukweli tuu, na siku zote ndio husimama mpaka mwisho. Kali ya rais wetu Dr. John Pombe Magufuli, kuwa "CCM itatawala Milele " ni kauli ya ukweli kabisa kuwa ni ukweli halisi na ukweli bayana, katika mazingira ya sasa ya nchi yetu na uendeshaji wa siasa za vyama vingi, kama hakuna kitakachobadilika, then rais Magufuli yuko very right kuwa CCM itatawala milele!.

Moja kati ya sifa kubwa za rais Magufuli, ni kusema ukweli Daima tena bila kukopesha, wala kurembaremba, japo kuwa mkweli sana sometimes sio nzuri sana kidiplomasia katika baadhi ya maeneo, ambapo diplomasia hutumika, haya mambo ya diplomasia ndio yametufikisha hapa tulipo, sasa ili tutoke hapa na kusonga mbele kimaendeleo, Watanzania ni lazima tujifunze kuubali ukweli jinsi ile ulivyo, bila kurembwa rembwa. La CCM kutawala mimi ni ukweli mtupu.

Kuna wengi wanadhani siasa ni kupiga blah blah tuu, hivyo kwao, kila kinachosemwa na wanasiasa, wanakiona kama ni blah blah!, no!. Siasa sio blah blah, japo blah blah zipo, ila pia kuna ukweli bayana, dhahir, shahir!. Siasa ni sayansi, social science, hivyo sayansi ya siasa ni political science, inafuata kanuni zile zile za kisayansi za Newton laws of motion, ile kanuni ya a body in motion or a static body, itaendelea kubaki hivyo hivyo milele, hadi kutokea nguvu nyingine itakayoibadilisha, hivyo kwa hali hii ilivyo sasa, CCM is the body in motion, itaendelea kutawala milele, kwa sababu watu wenye uwezo wa Kimungu, wameishaona kuwa kwa Tanzania, hakuna kabisa uwezekano wa kutokea nguvu nyingine ya kuibadili CCM hadi isitawale Tanzania milele!.

Japo kila lenye mwanzo, huwa lina mwisho, na CCM inamwanzo lakini haina mwisho, kitu pekee ambacho kina mwanzo na hakina mwisho, ni Mungu pekee ambaye ni Alfa na Omega, hivyo pia katika utawala wa Tanzania, CCM ndio alfa na omega wa siasa zetu, huu ni ukweli bayana ambao lazima sote tuukubali na wale wote wasioukubali ukweli huu, ni kweli watapata taabu sana!.

Hizi kauli za CCM kutawala milele, hazikuanza leo, na wala hazikuanza na rais Magufuli.
Hebu tembelea bandiko hili, umsikilize mwana CCM huyu alisema nini na uangalie alisema
lini na alisema wapi!, kwa wavivu wa kufungua links, kauli hii ya CCM kutawala milele, ilitolewa na Mhe. Pinda ndani ya Bunge letu tukufu na hakuna aliyetia neno!.
PM, Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda; Sorry, You are very wrong!

Nilidhani Mhe. Pinda amekosea, kumbe mimi ndiye niliyekosea baada ya ukweli huu kuzidi kuthibitishwa.

Humu jf, mtu wa kwanza kusema kuwa CCM itatawala milele ni mwana jf huyu
Je, CCM Itatawala Milele Au?
Na nilipokutana naye, nilifanya nae mahojiano haya.
lini
Watch TBC Live!. " William Malecela na Ndoto ya CCM Kutawala Miaka 50!.

Wenye Matumaini na Upinzani Kushika Dola!, Sahauni! CCM Inajiandaa Kuua Kabisa na Kuuzika Jumla !.

Kuhusu hili la CCM kutawala milele, pia niliwahi kulisema hapa
CCM kutumia Hooks & Crooks Kushinda Chaguzi, Inajua Ikishindwa Ndio Itakufa Jumla, Itakubali?

Katika awamu hii, viongozi wa upinzani walipoamua kujiengua kwenye vyama vyao kujiunga CCM, japo walibezwa, nikasisitiza humu, wasibezwe, wanaona mbali
Trend Reading: Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je tunarejea nchi ya Chama kimoja?

Pascal

mkuu naona uminyooka unafuata mstali uleeee
 
kwa leo acha nikuite mpuuzi! milele ukiwa na maana hadi masihi anarudi au? huo ukweli wa huyu mtu ni upi? ukweli wa kuwa Saddam Husein ni wa Kuwait au?
 
Back
Top Bottom