Wala hautishi mkuu,muhimu uwe na kiwanja tu basi,ukishakipata hicho basi umemaliza kazi,kitakachofuata unaanza kununua tofali,huku unatafuta ramani ya nyumba unayotaka ukishakamilisha idadi ya tofali au hata nusu tafuta fundi akupe hesabu ya msingi,kupandisha kwa tofali zilizopo utashangaa mambo yanaenda,nilichogundua wabongo tunaogopa sana ujenzi kutokana na maneno ya watu utasikia "aah wewe utajenga nyumba kwa mshahara wako huo mbuzi?unamuona fulani na hela zake zote amejenga nyumba kaishia kwenye msingi"na blah blah blah nyiiingi ila ukiingia kwenye action utaona kama ulichelewa sana,imenikuta hii ila nilipiga moyo konde nikaomba Mungu nikaingia site nikiwa na mill8 ikaishia kwenye msingi,hapa napoandika nimeshapandisha nyumba ina master bedroom3,sitting room,dinning,jiko,store na public toilet2,nimeshakamilisha pesa za kuezekea Mungu akinijaalia uzima soon nataka nianze mishe za kupaua.Muhimu:kwanza uwe na nia,mwepesi wa kucheza na hesabu(i mean uithamini kila sent unayoipata)uwe mwepesi wa kuchanganua shauri unazopewa,hasa marafiki hawa ndio jipu maana wanajua ukishaanza ujenzi hutoonekana viti virefu mwisho usiwe mwoga jikubali kwamba unaweza na unalolifanya unafanya kwa ajili yako na familia yako,mwisho uwe makini kuchagua mafundi,ikiwezekana siku za ujenzi uwe site maana fundi anaweza kutaka umpe hela ya nondo ukampa pesa ya kununua nondo za kuzungusha nyumba nzima kila ukuta nondo tatu tatu ila yeye anakuwekea nondo moja moja madhara utayaona baadae nyumba inaanza kushake,kila la kheri kaka.