Kupaua nyumba (Makadirio ya gharama)

Asante kaka umenipa mwangaza mzuri,kama hutojali naomba kama itawezekana uniambie hizo bati ulizinunua duka gani(kama upo Dar),pia mbao ulitumia za dawa au za kawaida?natanguliza shukrani.
 
Ujenzi unatisha kama huna roho ngumu hujengi. Ft moja bei gani mkuu!
Wala hautishi mkuu,muhimu uwe na kiwanja tu basi,ukishakipata hicho basi umemaliza kazi,kitakachofuata unaanza kununua tofali,huku unatafuta ramani ya nyumba unayotaka ukishakamilisha idadi ya tofali au hata nusu tafuta fundi akupe hesabu ya msingi,kupandisha kwa tofali zilizopo utashangaa mambo yanaenda.

Nilichogundua wabongo tunaogopa sana ujenzi kutokana na maneno ya watu utasikia "aah wewe utajenga nyumba kwa mshahara wako huo mbuzi?unamuona fulani na hela zake zote amejenga nyumba kaishia kwenye msingi"na blah blah blah nyiiingi ila ukiingia kwenye action utaona kama ulichelewa sana,imenikuta hii ila nilipiga moyo konde nikaomba Mungu nikaingia site nikiwa na mill8 ikaishia kwenye msingi,hapa napoandika nimeshapandisha nyumba ina master bedroom3,sitting room,dinning,jiko,store na public toilet2,nimeshakamilisha pesa za kuezekea Mungu akinijaalia uzima soon nataka nianze mishe za kupaua.

Muhimu:kwanza uwe na nia,mwepesi wa kucheza na hesabu(i mean uithamini kila sent unayoipata)uwe mwepesi wa kuchanganua shauri unazopewa,hasa marafiki hawa ndio jipu maana wanajua ukishaanza ujenzi hutoonekana viti virefu mwisho usiwe mwoga jikubali kwamba unaweza na unalolifanya unafanya kwa ajili yako na familia yako,mwisho uwe makini kuchagua mafundi,ikiwezekana siku za ujenzi uwe site maana fundi anaweza kutaka umpe hela ya nondo ukampa pesa ya kununua nondo za kuzungusha nyumba nzima kila ukuta nondo tatu tatu ila yeye anakuwekea nondo moja moja madhara utayaona baadae nyumba inaanza kushake,kila la kheri kaka.
 
Umeeleweka sana kaka! Hatua ulizopitia zinafanana na hatua zangu! Kwa sasa mjengo umesimama nasubiri kupaua. Mbao ndo zinasumbua kidogo navuta pumzi kwa kujenga shimo la choo ft 12 urefu duara ft 11
 
Umeeleweka sana kaka! Hatua ulizopitia zinafanana na hatua zangu! Kwa sasa mjengo umesimama nasubiri kupaua. Mbao ndo zinasumbua kidogo navuta pumzi kwa kujenga shimo la choo ft 12 urefu duara ft 11
Wengi tumepita au tunapita humohumo.
Katika Ujenzi, msingi wa nyumba ni element ngumu sana ambayo ukiimaliza na mtu ukamtajia gharama ulizotumia, anaweza kubisha. Pia kwa wenzangu na mimi wa hela za kuunga unga(stage construction-not to be confused with road stage construction) eneo lingine ambalo lazima ulikamilishe kwa pamoja ni Roof Structure and Roof Covering(yaani Kenchi na kuezeka). Ugumu wake ni pale ambapo huwezi kuweka kenchi ukaliacha muda mrefu huku ukitafuta pesa za bati, kwani mbao zitapinda zote. Ni lazima ukusanye pesa za kazi zote. Na hapo ndipo shida ya ujenzi kwa hela za kuunga unga inapoanzia. Ukivuka stage hiyo uko huru
 
Exactly mkuu,msingi&kupaua ndo hasa sehemu inayoumiza kichwa ila mtu ukifanikiwa kupita hapo kidoogo mzigo unapungua,ukiwa nyumba hujapaua huwezi kwenda site na lak5 but kama umeshapaua ukienda na hiyo hela unafanya jambo kubwa ajabu.
 
Mkuu, mabati ya ando yapo ya aina nyingi na kila aina inatofautiana na nyingine haya idadi ya mbao. Pia kuna aina ya bati inaitwa old profile, hii ina mafundi wa chache sana kwani wengi hukimbia ktkt ya kazi. Ikiwa nyumba yako huna uhakika epuka kununua bati hii japo kwa macho inavutia sana, hakikisha unapata mtu sahihi vinginevyo utajuta kununua bati hii
 
Mkuu, msingi wa nyumba ndo kila kitu. Mimi ulitafuna 8,300,000/= lakini namshukuru Mungu mambo yalikwenda nikamaliza. Niko kwenye kukusanya nguvu kwenye kupaua hapo hakuna kuunga unga ni mwanzo mwisho. Tuombeane na kutiana moyo.
 
Exactly mkuu,msingi&kupaua ndo hasa sehemu inayoumiza kichwa ila mtu ukifanikiwa kupita hapo kidoogo mzigo unapungua,ukiwa nyumba hujapaua huwezi kwenda site na lak5 but kama umeshapaua ukienda na hiyo hela unafanya jambo kubwa ajabu.
Kabisa mkuu
 
Mi nahitaji yale ya muundo wa vigae. Wanauzaje na order inatakiwa uweke mda gani?
Mkuu order inategemea uko mkoa gani na aina ya bati, ikiwa uko Dar, Arusha, mbeya nawanza hii mikoa inayo mashine ya kukunja aina mbalimbali japo mengine yanapatikana Dar tu
 
Umeeleweka sana kaka! Hatua ulizopitia zinafanana na hatua zangu! Kwa sasa mjengo umesimama nasubiri kupaua. Mbao ndo zinasumbua kidogo navuta pumzi kwa kujenga shimo la choo ft 12 urefu duara ft 11
Mbao zinaumiza kweli mkuu ila tutasonga tu kwa hatua uliyofikia si'haba...mdogo mdogo mara mtu uko kwako,nachukia sana haya mambo unalipa kodi mwaka huu kiasi hiki mwaka kesho unapandishiwa kodi mara mbili kwa madai eti gharama za ujenzi zimepanda ukiuliza " Mzee wangu wapi uliporekebisha hadi kusema gharama zimepanda?"anatishia kukupa notes...shit case dizaini hii imenilaza police post Mabatini baada ya kumgomea mwenye nyumba na yeye kunitukana alichoambulia ni makofi,Mungu atusaidie tuondokane na kadhia hii.
 
Inauma sana mkuu! Tuombe uzima kila kitu kinawezekana.
 
Asante kaka umenipa mwangaza mzuri,kama hutojali naomba kama itawezekana uniambie hizo bati ulizinunua duka gani(kama upo Dar),pia mbao ulitumia za dawa au za kawaida?natanguliza shukrani.
Kaka hii site iko Nyamhongolo mwanza, na bati nilichukua za aiba ya kiboko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…